Jemedari Said: Simba anacheza mashindano bora kuliko Yanga, Magoli yake yana thamani kubwa kuliko ya Yanga

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Mchambuzi mahiri wa michezo nchini, Jemedari Said amesema Simba na Yanga wanacheza mashindano yenye ubora tofauti, Simba ligi ya mabingwa Afrika, na Yanga kombe la Shirikisho.

Kutokana na kutofautiana ubora kufunga goli kwenye ligi ya mabingwa ni vigumu zaidi kuliko Shirikisho hivyo magoli ya Simba yalipaswa kuthaminiwa zaidi kuliko ya Yanga na sio kupewa thamani ya milioni 5 yote.

Jamaa kasema timu zinazofanya vibaya Champions League (mfano Yanga na TP Mazembe) hupelekwa kucheza Shirikisho kitu ambacho kinathibitisha utofauti wa ubora.
 
TAAHIRA huyo. Anadhani timu alizopangiwa YANGA ingepangiwa timu lake bovu na kinyume chake angetoboa?
Labda wangemfunga yule ZALAN tu hata haya MAKUNDI YA LUZA wasingefika.
 
Jamani hata cha kupewa na chenyewe tunakilalamikia,Wakati Mh.Rais katoa kwa Upendo wake tu angetaka asingetoa hamna sheria inayombana na hata asingetoa mngecheza tu mashindano.!
 
Sehemu gani? Kuwa shirikisho ni kombe dogo na Yanga aliingia baada ya kushindwa au m5 kwa kila goli?
Soma hapo juu utaelewa hoja yake ni nini sasa
 
Ukweli ni kwamba mashindano ya mabingwa ni magumu kuliko shirikisho.
Na sababu iko wazi: ukikwama mabingwa unaingizwa shirikisho
Ugumu pia unategemea na kundi ulilopo na ubora wa timu yako.
 
Tatizo huyo jamaa ni Polisi wa Zenji
 
Ukweli ni kwamba mashindano ya mabingwa ni magumu kuliko shirikisho.
Na sababu iko wazi: ukikwama mabingwa unaingizwa shirikisho
Shida yake huyo huyo ungemsikiliza juzi Simba walivyocheza na vipers alichokiongea na leo ni vitu viwili tofauti..kama ameiona Simba kama alivyoiona anataka waongezewe hela za nini?
 
Shida yake huyo huyo ungemsikiliza juzi Simba walivyocheza na vipers alichokiongea na leo ni vitu viwili tofauti..kama ameiona Simba kama alivyoiona anataka waongezewe hela za nini?
Alisema Simba haichezi kama ilivyozoeleka kucheza
 
Sasa yanga mnapanic nini, mbona amezungumza ukweli tu, utopolo champions league ili wapalia mkaangukia kwa malosers, sasa iweje magoli yetu yapewe thamani sawa, hii sio haki.

NB: 7 points obtained in cafcc equals to 2 points in cafcl .. famasiala nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…