Jenerali Mabeyo amuaga Rais Mwinyi. Ajiandaa kustaafu June 2022

Jenerali Mabeyo amuaga Rais Mwinyi. Ajiandaa kustaafu June 2022

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo leo amefika Ikulu ya Zanzibar kwaajili ya kumuaga Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ikiwa ni maandalizi ya kustaafu mwishoni mwa mwezi huu.

Jenerali Mabeyo 65, amelitumikia jeshi kwa miaka 42 sasa na muda wake wa utumishi unaenda ukingoni mwezi huu.

Jenerali Mabeyo amehudumu nafasi ya Mkuu wa Majeshi kwa miaka 6 sasa baada ya kuteuliwa mwaka 2016 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli.

Katika uongozi wake kama CDF, alishuhudia kukabidhiwa kwa madaraka kwa Rais wa kwanza mwanamke, Samia Suluhu Hassan baada ya kifo cha mtangulizi wake.

Daima utumishi wake uliotukuka utaendelea kukumbukwa ndani ya JWTZ na Nchi kwa ujumla. Nikutakie maandalizi mema ya kustaafu Jenerali Mabeyo

View attachment 2252170

View attachment 2252706


---
Jenerali Venance Mabeyo ni Mkuu wa Majeshi wa nane kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tangu alipoteuliwa Februari 6, 2017 na aliyekuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Alizaliwa Julai 1, 1956 wilayani Magu mkoani Mwanza na kupata elimu ya msingi katika shule ya Namibu mkoani Mara kuanzia 1965 hadi 1971.

Alianza elimu ya Sekondari katika Seminari ya Nyegezi kuanzia 1972 hadi 1975, kisha akaendelea na kidato cha tano na sita Mzumbe Sekondari kuanzia 1976 hadi 1977.

Jenerali Venance Mabeyo alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Januari 1, 1979 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1980 kuwa Luteni Usu.

Safari ya Jenerali Venance Mabeyo JWTZ
Julai 1980: Luteni Usu
Agosti 1981: Luteni
Januari 1987: Kapteni
Oktoba 1991: Meja
Juni 1998: Luteni Kanali
Mei 2006: Kanali
Septemba 2010: Brigedia Jenerali
Septemba 2014: Meja Jenerali
Juni 2016: Luteni Jenerali
Februari 2017: Jenerali

Jenerali Venance Mabeyo alihudhuria kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadhi ya nchi hizo ni Kenya, India, Canada na Marekani

Jenerali Venance Mabeyo katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwambata Jeshi nchini Rwanda, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi , Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ.

Jenerali Venance Mabeyo ametunukiwa medali mbalimbali;
Miaka 20 ya JWTZ
Medali ya utumishi mrefu.
Medali ya miaka 40 ya JWTZ.
Medali ya utumishi uliotukuka.
Medali ya Comoro na Anjouan.
Medali ya miaka 50 ya uhuru
Medali ya miaka 50 ya Muungano
Miaka 50 ya JWTZ
Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara
Mbona elimu yake ndogo sana, au ndio kuwa na busara nyingi na hekima ya juu?!
 
Akipewa huyo Poti wangu ( kutoka Kwetu Mara ) Sibuti ambaye pia ni Mkristo na Mkatoliki Mwenzangu nitampenda Rais Samia mpaka basi.
Kiwango chake cha juu cha elimu ni kipi? Inaonekana wenye elimu ndogo ndio wanapewa hicho cheo!
 
..Natumai CDF anayekuja ataachana na maonyesho ya askari kuvunja MATOFALI kwa kichwa.
 
18 March 2022
Kunduchi, Dar-es-salaam.

1654609857803.png

Rear Admiral Ramson Godwin Mwaisaka, who is the Commander of the Tanzanian Navy, presided over the closing ceremony held at the Peacekeeping Operations Training Center in Kunduchi, Dar-es-salaam.

ustz2-1024x768.jpg

Brigadier general Nkambi was joined by Senior Defense Official at the American Embassy in Tanzania as well as members of U.S. Special Operations Command Africa
 
10 June 2022

Mkuu wa operesheni wa JWTZ meja jenerali J.J Mnkuda azungumza na wapiganaji waliomaliza mazoezi ya utayari

 
14 Juni 2022
Dodoma, Tanzania

SIKU YA BAJETI

Jenerali Venance Mabeyo na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wafika Bungeni kusikiliza bajeti ya serikali mwaka 2022/ 2023

 
..wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wana chombo chao ambacho kinaongozwa na Cdf.

..Sasa najiuliza kwanini WATU WASIOJULIKANA walikuwa wanatamba huku tunaye Cdf tunayesema uongozi wake umetukuka?
Swali lakipumbavu kwaiyo unazani wasiojulikana ni kikundi tu Kama panya road?

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
Mteuwaji asisahau kuwa Wakristo ( tena wa Katoliki ) ndiyo huwa CDF ( japo katika Madhehebu mengine ) anaweza Kuokoteza okoteza lakini asiwekwe hapo wa Dini yake Mteuwaji.

Najua kuna mtakaonishangaa na Kunishambulia ila GENTAMYCINE nasisitiza ni lazima CDF aje ( kwa sababu ambazo ni za Ndani kabisa ) awe ni Mkristo kutoka Dhehebu lenye Nguvu na Ushawishi Tanzania na Duniani la Katoliki.

Ukikereka na nilichokiandika Koroga Sumu ya Panya unywe na Ukishainywa jipige Kofi la Kutukuka na jiite Popoma.

Hahah! 😂
 
Back
Top Bottom