Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Inaelekea JWTZ inathamini wanajeshi wakiwa na afya njema lakini pindi wakiumia au kupata maradhi wakiwa kazini inawatelekeza!

Amiri Jeshi Mkuu anapaswa kuangalia upya jambo hili kwani halina afya kwa ustawi wa jeshi letu.
Wajameni.....ya JWTZ tuwaachie peke yao.
Wao wanataka JUA lile literemke,sisi tutaweza kweli....???

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mwekeni Lema au Mbowe awe mkuu wa Majeshi kama Mabeyo hatoshi
Punguza dharau. Unaongea hivyo kwasababu hao makomandoo wamekamatwa na mbowe. Kumbuka usipolia na mwenzako ipo siku ukilia hakuna atakayekusikiliza. Juzi Lissu kapigwa risasi watu wakacheka ila Magufuri alipofariki wakaanza kulia na kudai ameuawa. Tujifunze what goes around comes around.
 
KUNA JAMAA YANGU PIA ALIPITIA HII SEKESEKE ILA MUNGU NI MKUBWA SANA.
 
So sad aisee, yaani kama waliyosema ni kweli basi kuna shida somewhere kwenye mifumo yetu au sheria zetu.
Siyo shida ya mfumo wa sheria. Tatizo hapa ni uongozi au utawala bora kutokuwepo. Komandoo wote walioifukuzwa na wanaostaafu wanatakiwa wawe na kitengo cha "Minder" jeshini chenye bajeti. Kazi ya kitengo hicho ambacho kinawaangalia askari wa kawaida waliko uraiani na pia wao wakiwa na tatizo kuweza kwenda hapo na kueleza shida zao. Siyo kuwaangalia maafande wa ngazi za juu peke yake. Huu ni utaratibu ambao nchi zilizoendelea zinafanya. Vinginevyo kuacha askari mwenye mbinu ya kuuwa watu wengi bila bunduki ajiangalie mwenyewe ni kukosa upeo wa uongozi. Naandika hapa kuisaidia Serikali kungalia hili sina nia ya kuwananga.
 
mbona tuna wakuu wa wilaya wanaitwa labda Luteni Kanali mstaafu! Ina maana hata wanapoondoka jeshini, bado vyeo vyao wanaenda navyo, Hata mimi namba yangu ya JKT bado ninayo na ukiifuatilia utaona na cheo changu.
Kuna mtu kapost humu kuwa "usimuone simba kanyeshewa, ni simba!"
 
Occupational health effects au Adverse health effect related to work zinatatuliwa na Boss/ mwajiri na kupewa compensation.
Sasa kama hatapokea mafao yoyote au pensheni atawezaje kujitibu na ku attend clinic?? Vipi mfanyakazi anapoumia kazini na kukatwa mguu au mkono?
 
Hao hawakufu hawakufukuzwa kazi kuna tofauti ya kufukuzwa na kustaafu. Kufukuzwa maana yake wana diclare kuwa hawakustahili kumwajiri mtumishi kama wewe na wanafuta kila kitu na kukurudisha katika hali uliyokuwa nayo kabla ya kuajiriwa na wao wabaki kwenye nafasi ya karibu kana kwamba hawajawahi kumwajiri mtumishi wa hovyo na.mwenye tabia mbovu kama wewe
Kutaafu ni kiwango cha juu kabisa cha heshima kwa mtumishi wa uma na mwajiri anafurahi ukilitumia jina lake baada ya kustaafu.lakini kufukuzwa ni.fedheha na hakuna mwajiri yoyote atakubali ujitambulishe kwa jina la kampuni yake baada ya kui tarnish image ya kampuni yake kwa tabia mbovu iliyosababisha kufukuzwa kwa fedheha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…