Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

Kwani ni kila askari wa jwtz anaestaafu au kufukuzwa kazi anatendewa hayo waliyotendewa hao ex commandos?
Hao wamejiingiza kwenye vitendo viovu ndiyo maana yamewakuta hayo yaliyowakuta.
Sijui huu ujinga mtauacha lini aisee, je wameshakutwa na hayo makosa mpaka unahitimisha kwamba wamejiingiza kwenye vitendo viovu?? Na yule wa Tabora na wenziwe waliochiwa kwa kuonekana hawana hatia hayo mateso utayalipa wewe?? Mitizamo yenu finyu ya kisiasa unawapumbaza macho na kuonekana mapimbi.
 
Ipo siku utatamani kumeza haya maneno.
Mi naona tufike tu huko, hii dharau kwanza mwanamke halafu kutesa makomandoo ambao ndio icon ya jeshi lolote duniani na taarifa hizo za kudharirisha bora zingekuwa siri zinatolewa hadharani , sijui kijeshi hili limekaaje, mi nahisi JWTZ yote sasa imedharirishwa, na nahisi tuna watu ambao hawajui lolote kwenye mambo ya usalama halafu eti wanasema " , " MIPAKA YETU YOTE IPO SALAMA",
Kama ambavyo tumeona kuna watu wakifika vyeo fulani nchi hii hawaguswi ovyo, nadhani hao jamaa wangeshughulikiwa jeshini.
 
Hao walifeli mkuu, hilo lilikuwa ni test ila wao hawakujiongeza. Walikuwa wanapimwa uwezo wa kutumia maarifa yao kutatua matatizo unapokuwa huna msaada, walipaswa wafanye ukomandoo wapore mamilioni sehemu wajilipe, halafu jw na polisi wangewasiliana, hata daktari mwanafunzi anaweza kukuua akikosea,
[emoji1]
 
Nilisema mwanzoni mwa msimu huu kuwa, hata mtoto anapokuwa hamuoni baba ana lelewa na single mother kuna saikoloji yake ya kiume inafeli , na wengi hupata madhara ukubwani,
Nilisema hii ni mbaya kwa majeshi yetu, ona sasa, mpaka makomandoo wamelegea hivyo, jeshi lipo tu kimya, halafu eti mipaka yetu ipo salama, [emoji15]
Salama kwa jeshi la hivyo, watu wanawachora tu mnavyoshuka chati, ngoja muishe ndio mtaelewa dunia!
 
Nchi haina kichwa kwa sasa....
 
Awamu hii pamoja na ya Magufuli ndio awamu JWTZ imedhalilishwa kupita kisi...

Kwanza ni inflitrattion iliyofanyika ya kugawa nafasi za Kisiasa kwa senior oficers wa JWTZ... Maana yake umewa- neutralize totally ukawafanya wanasiasa...

Shame shame shame...
 
Leo hii ukipita kwenye Makambi ya Jeshi kumejaa mafremu ya biashara na ma-bar yamejengwa... Jeshi la wafanya biashara... Inasikitisha sana
 
Ni aibu sana kwa Mabeyo, anajifanya mtu wa dini kumbe 🚮 Yaani askari wake wanatekwa, wanateswa,wanatekwa,yeye kimya...hii aibu haijawahi kutokea kwa General mwingine yoyote kabla yake. Mbaya zaidi askari anafukuzwa kazi, mwaka mzima sasa hajalipwa stahiki zake, anazungushwa tu!!! Shame!!
 
Hawakushindwa jujitetea Hawa makomando. Wameheshimu uzakendo zaidi ya uvumilivu. Kama pa private tu na migambo wakizinguliwa wanauwasha moto miyaani, kweli JWTZ wameshinda kulitetea jeshi na utu wake? Au JWTZ unaowapa ujumbe wajeshi kwamba wawe kondoo wadhaifu KWA kuonewa tu?

Hata kama wamestaafishwa vita ijiibuka hamtawahitaji kweli waendelee na jungle survival law? HAPANA. Jeshi liheshimiwe. Sijawahimwona Polisi akiwadhalilisha JWTZ mitaani, tuelewe kwamba utu wa mjeshi unabisha akistaafu au kusyaafishwa tena kwa kudhurika kazini? HAPANA.

Kutafuta ajira halali baada ya kustaafu ni haramu KWA askari wa JWTZ? Mnataka watumie Mafunzo na uzoefu wa jeshini ILI KUTUNZA familia zao? Nyie viongozi wa JWTZ ingekuwa no ninyi mngetulia hivyo? Shame on you.
 
Ndio kuna Sheria, hizo Sheria zao hazijali Haki ??? Yaan kumfukuza MTU bila kumpa barua??? Wala Mafao yake aloyatumikia muda wote huo!!!?.
Yaani mtu anafukuzwa kama mbwa! Komando anaishia kwenda kulima mahindi jembe la mkono!
 
Jeshini kunasheria zao
Kama taasisi zingine zilivyo za hovyo,hata jwtz ipo hivyo,hizo posho wanakula wakubwa!hiyo nafasi ya ukomandoo inakuwa kama umefanyiwa hisani,ukipiga kelele ndio hivyo haki zako zinaminywa.jinsi Rushwa ilivyokita mizizi,ajira siku hizi zinauzwa,mpaka kwenye taasisi nyeti ajira,zinauzwa tu,
 
Akina polepole na Bashiru waharifu hawatupwi mtaani angalau wanapewa hata ubunge wa kuteuliwa lakini askari aliyepata matatizo akiwa kazini wanamtupa mikono mitupu. Inafikirisha sana
 
Inaelekea JWTZ inathamini wanajeshi wakiwa na afya njema lakini pindi wakiumia au kupata maradhi wakiwa kazini inawatelekeza!

Amiri Jeshi Mkuu anapaswa kuangalia upya jambo hili kwani halina afya kwa ustawi wa jeshi letu.
bila elimu ya degree moja kwenye haya majeshi yetu ya tanzania ni shida tupu, utaishia kupigia watu saluti wakubwa, utatumiwa vibaya kama hawa kina Goodluck then ukizeeka unatupwa huko kwenu.

Training za ukomandoo ni ngumu mno zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu, kijana anahitimu unamtumia miaka 5 then unamuacha tena kwa fedheha, hii si haki.
 
Hili jambo la hawa Makomandoo wetu linaniumiza na kufikirisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…