FK21
JF-Expert Member
- May 27, 2019
- 8,600
- 10,760
Komandoo anapigwa Hadi kulia ilo ni jeshi?Kisa mbowe au?
Acheni mada za kijinga.
Jeshini si mahala pa siasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Komandoo anapigwa Hadi kulia ilo ni jeshi?Kisa mbowe au?
Acheni mada za kijinga.
Jeshini si mahala pa siasa
Amekwambia kastaafu halafu ww unasema amefukuzwaKuna jamaa mtaani kwetu yupo kwenye miaka 48 anasema yeye kastaafu mwaka juzi,je nae atakuwa amefukuzwa ama niamini tu kastaafu kama alivyoniambia
Mm nakwambia hawa Jamaa kukikuwa na siri nzito sana nyuma yao.Hawa hawakuwa Makomandoo wa JWTZ wakati wanakamatwa.
Walikwishafukuzwa jeshini kwa utovu wa nidhamu.
Wakaamua kuwa Makomandoo wa mbowe na hatujui alitaka kuwatumia kwa kazi ipi.
Subirini mahakama iamuwe haki. Acheni kuwewseka ovyo mitandaoni .
MazitoTatizo kujifungamanisha na vyama vya siasa.
ndo vijana wenzetu waelewe bora kukomaa tu mtaani na kazi zetu za kijungu jiko kuliko kukimbilia izo kazi unatimika kuumiza watanzania wenzako halafu ndo' kama tunayoyaona maana wakina adamoo na lingw'enya wote watoto wa wapiga kura yani wota kajamba nani unadhan mtoto wa mahita angetendewa ayo.Inaelekea JWTZ inathamini wanajeshi wakiwa na afya njema lakini pindi wakiumia au kupata maradhi wakiwa kazini inawatelekeza!
Amiri Jeshi Mkuu anapaswa kuangalia upya jambo hili kwani halina afya kwa ustawi wa jeshi letu.
Sijasema nina akili mimi ni zwazwa tu kama mazwazwa wengine,uwe na siku njema mkuuAkili hauna unafikiri ukiwa na upande shameful and pathetic
Yaani ulichoandika hata hakieleweki.Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.
Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?
Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.
Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili
Wasiojulikana sasa wamejulikana?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Na kinachoshangaza Bwire alikuwepo sana hapo O bay police zamani na ukiingia anga zake utakiona cha moto.Kwenye mkutano wa JWTZ na vyombo vya habari walisema jeshi haliajiri lakini linaandikisha,kama hujaajiriwa na umeandikishwa tu ndo chanzo cha kutelekezwa.
lakini jwtz kutelekeza komando haijakaa sawa.
pia komandoo kukamatwa/kutekwa kama kuku kuna siku hao polisi watapata wakinachokitafta,
hebu tujiulize kama makomandoo wote wako kama akina Adamoo au Bwile?
je walioko huko makambini wanachuliaje wenzao kuteswa tena na polisi?
au na wao kesho wakiwa mtaani yatawapata ya wenzao?
maswali mengi kuliko majibu
Hawa hawakuwa Makomandoo wa JWTZ wakati wanakamatwa.
Walikwishafukuzwa jeshini kwa utovu wa nidhamu.
Wakaamua kuwa Makomandoo wa mbowe na hatujui alitaka kuwatumia kwa kazi ipi.
Subirini mahakama iamuwe haki. Acheni kuwewseka ovyo mitandaoni .
We unaona anajielewa licha ya kujua chochote?Kwa akili zako unafikiri Mabeyo hajui chochote?
Niliwaahi andika humu, ila shida ni kutafutana.
Mimi Kaka yangu ( mtoto wa mama mkubwa)
Wakiwa pale kambi ya ukomandoo Morogoro...
Posho zao wakawa hawapewi, wakaamua kuja Dar makao makuu JWTZ kulalamikia.
maajabu, wakapewa Kesi za Uhaini, uhujum, uasi, uporaji wa Mali za Raia.
Walikua vijana 60 wa Mafunzo ya ukomando
30 wakasamehewa ...30 Wakafungwa jela mwaka 2015 akiwemo Kaka yangu huyo.
Waziri Mkuu anajua, Mwinyi anajua, Mwanasheria Mkuu wa wakat huo anajua,Mkuu wa Majeshi alopita anajua ..maana suala lao lilijitokeza 2013 .
WAKAFUKUZWA KAZI BILA KUPEWA BARUA YA KUACHISHWA KAZI, BILA KUPEWA MAFAO YAO, IKUMBUKE TOKA HUO MWAKA 2013 MPAKA 2015 ,MISHAHARA YAO ILISIMAMISHWA.
Walikua kuachiwa mwaka 2017 kwa msamaha
mpaka naongea hii Leo, Hawa vijana wamejitahidi kutafuta haki zao sanaaa ,wametumia wanasheria wapiiii..suala lao linaminywa chini chini.
KWA sasa wamebaki vijana 29. ..baada ya mmoja maisha kumchanganya, akaungana kwenye ujambazi,... Alipigwa risasi.
We Taga, hebu zinduka usijifanye hamnazo;Maana yake nn Mabeyo akawe jaji au una mananisha nn bwasheee?
Jeshi kwa ujumla halina business na ww ukishakuwa discharged from service.JWTZ hawana sera ya kuwalinda watu ambao wanakuwa trained kwa kiwango cha Ukomandoo, hawa jamaa walitelekezwa na wamepitia wakati mgumu mno.
Ukifukuzwa kaz hakuna mafao. Kwa sheria za nchi hii. Mafao wanapata walio staafishwa periodNdio kuna Sheria, hizo Sheria zao hazijali Haki ??? Yaan kumfukuza MTU bila kumpa barua??? Wala Mafao yake aloyatumikia muda wote huo!!!?.
Majeshi yote yako hivyo. Ukipata shida ya kiafya ambayo wanaona itakuziia kuweza kutekeleza kaz za kijeshi wana ku discharge. Au unapangiwa idara zisizo na pyhsical activity nzitoInaelekea JWTZ inathamini wanajeshi wakiwa na afya njema lakini pindi wakiumia au kupata maradhi wakiwa kazini inawatelekeza!
Amiri Jeshi Mkuu anapaswa kuangalia upya jambo hili kwani halina afya kwa ustawi wa jeshi letu.