Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 8,072
- 8,942
..wakistaafu wana ruhusa ya kushiriki active politics.
..Major General Marco Mwita Marwa aliwahi kujiunga na Chadema kabla Mkapa hajambembeleza arudi Ccm.
..Major Hassy Kitine, Mkuu wa usalama wa taifa mstaafu, aligombea ubunge wa Makete kupitia Ccm.
General Robert Mboma, Cdf mstaafu, aliomba ridhaa ya Ccm kugombea ubunge baada ya kustaafu.
..Brig Gen Hassan Ngwilizi alikuwa mbunge na Naibu Katibu Mkuu wa Ccm.
..Brig.Gen, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhani, alijiunga na Ccm baada ya kustaafu, na kuomba ridhaa kugombea Uraisi kupitia chama hicho.
..Hivi General Mkunda anajua sheria na taratibu za nchi hii kuzidi watajwa hapo juu?
Kwa sasa kuna kitu wanakiita uchawa.Kuna wakati sababu ya pressure zake, huwa tunakosa muda wa kusoma na kuelewa sheria na taratibu.
Huwa tunakosa muda hata wa kuuliza kwa wengine ili tujifunze na kuelewa.
Uchawa kama ulivyo, huwa unatoa ahadi ambazo haziwezi kutekelezeka. Uchawa kwa tabia zake unatoa ahadi za maisha ya peponi, wakati bado tunaishi duniani.
Na duniani, wazee walituasa, hujafa hujaumbika......
