Jenerali Muhoozi Kainerugaba ni dhahiri sasa amelewa madaraka. Ni kweli kwamba hajui madhara ya kauli aliyotoa kuhusu kuivamia Kenya?

Jenerali Muhoozi Kainerugaba ni dhahiri sasa amelewa madaraka. Ni kweli kwamba hajui madhara ya kauli aliyotoa kuhusu kuivamia Kenya?

ankai

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2017
Posts
3,282
Reaction score
4,251
Yaaani nimeshindwa kuelewa mshauri wa masuala ya usalama katika nchi analeta utoto kama huu duuh
Screenshot_20221003-184149_Twitter.jpg
 
Tunaweza kudhani anaisema Kenya kumbe ameilenga Tanzania, hata Ile Vita ya 1978-1979 ilianzaga hivi hivi
 
Mtoto wa Rais wa Uganda Gen. Muhoozi Kainerugaba amesema yeye na vikosi vya majeshi yake vinaweza kuuteka mji wa Nairobi, Kenya kwa kutumia muda usiozidi wiki mbili kisha kuufanya kuwa sehemu ya nchi yake.

7E95B731-8642-42E0-BB43-6FCA56F0BE51.jpeg

Kupitia mtandao wa Twitter, Gen. Muhoozi amesema hajali mipaka ya nchi iliyowekwa tangu enzi za ukoloni na ametoa hakikisho kuwa ikiwa vita itatokea katika harakati za kuichukua Nairobi basi itachukua muda mfupi kuisha.

Jumbe hizi zinaweza kuleta mgogoro wa kidoplomasia kati ya nchi hizi japo bado haifahamiki kama anafanya utani, amedukuliwa au maandiko yake yana maana ipi.

Amesema kuwa wao kama Uganda hawajali Katiba au utawala bora isipokuwa mapinduzi pekee, na kama Kenya haijui yalivyo basi wasubirie kujifunza kutoka kwao.

“Baada ya majeshi yetu kuiteka Nairobi, mimi nitaishi wapi, Westlands au Riverside?” Amehoji Gen. Muhoozi.

Katika hatua nyingine ameelezea furaha yake baada ya kuzungumza na Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye amenuahidi kutembelea nchi ya Uganda siku chache zijazo. Amesikitika kwa nini Rais huyo mwenye uelewa mkubwa wa mambo, jasiri na muungwana hakugombea mhula wa tatu wa urais kwa kuwa yeye anayo imani kuwa angeshinda.

Muhoozi 1.jpg

Muhoozi 2.jpg
 
what is Muhozi drinking these days ?! Yani hayo ni matamshi ya afisa wa ngazi ya juu kabisa ya jeshi ?! Anajua madhara ya kauli zake hizo achilia mbali Uganda haiwezi kamwe kupindua hata serikali ya mtaa ya Kenya sembuse Nairobi.

Uganda is ruled by a bunch of idiots just enough to say so.
 
Anaona Kenya ni poyoyo??
Mbona hasemi Tz
Mlevi huyo tumnyooshe kama ndugu yake amini nduli

Ahame nchi yake na afie huko porini
Pumbavu kabsaaa ole wake aiguse Kenya
Yeye alewe mataputapu yake halafu amguse jiran yetu bila kosa lolote

Tutamnyoosha
 
Back
Top Bottom