Jenerali Ulimwengu: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina zaidi ya wanachama milioni 8, lakini kina mawazo ya kufikiri yasiyozidi matatu

Jenerali Ulimwengu: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina zaidi ya wanachama milioni 8, lakini kina mawazo ya kufikiri yasiyozidi matatu

Huyu Jenerali ni mrundi na mawazo yake ya kihutuhutu!
Yuko vizuri Sana upstairs, CCM nzima Hakuna mwenye akili Kama yeye....mtu anakuwa Hana akili akiwa kiongozi anakuwa na akili kuwazidi wote.....ndio akina Jiwe na Chief
 
MWANDISHI wa Habari Mkongwe, Jenerali Ulimwengu leo Septemba 21,2021 amezindua Kitabu chake RAI YA JENERALI jijini Mwanza na kuhudhuriwa na Askofu Benson Bagonza.

𝗛𝗔𝗬𝗔 𝗡𝗜 𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗡𝗘𝗡𝗢 𝗬𝗔𝗪𝗔𝗟𝗜𝗬𝗢𝗭𝗨𝗡𝗚𝗨𝗠𝗭𝗔 𝗪𝗔𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗪𝗔 𝗨𝗭𝗜𝗡𝗗𝗨𝗭𝗜 𝗛𝗨𝗢....

"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina zaidi ya wanachama milioni 8, lakini kina mawazo ya kufikiri yasiyozidi matatu" - Jenerali Ulimwengu

"Hakuna uwezekano wa kizazi chetu kupata maendeleo na kupiga hatua ikiwa kitaendelelea kufundishwa kwa lugha wasioijua na pia wale wanaowafundisha nao hawaijui hiyo lugha"- Jenerali Ulimwengu

"Hakuna swali la kijinga ila majibu ndo ya kijinga"- Jenerali Ulimwengu

𝗔𝘀𝗸𝗼𝗳𝘂 𝗕𝗲𝗻𝘀𝗼𝗻 𝗕𝗮𝗴𝗼𝗻𝘇𝗮

"Mwalimu Nyerere aliwahi kusema marais wazuri waongoze kwa vipindi viwili ili waondoke na uzuri wao, lakini marais wabaya wao wataondolewa na wananchi" - Askofu Bagonza

"Tabia ya watu kusifia viongozi waliopo madarakani kufanywe kama kosa la jinai ili kupunguza watu kujipendekeza kwa viongozi kupata uongozi"- Askofu Bagonza

"Watanzania wanahitaji katiba yenye uwezo wa kuweka na kuwaondoa viongozi madarakani badala ilivyo kwa sasa" - Askofu Bagonza

"Muujiza wa elimu ya Tanzania kiongozi akichaguliwa leo akiwa hajui kitu, akishaingia madarakani kesho yake anakuwa anajua kila kitu"- Askofu Bagonza

"Tunaupungufu mkubwa katika Taifa letu la watu wenye Fikra na Uthubutu; Wapo wenye Uthubutu lakini hawana Fikra, kuna watu unawaona wana Fikra lakini hawana Uthubutu. Makundi haya yanahitaji daraja kuyaunganisha" - Askofu Bagonza

"Aslimia 60 ya wabunge wa CCM waliopo bungeni kwa sasa hawakushinda kura za maoni ndani ya chama chao, hata wanachama wao wanajua na wanaona kabisa hawakuwachagua na hivyo wanaona siyo wa wabunge wao"- Askofu Bagonza

"Bunge la sasa lina utata, kuna mabunge mawili (2), moja lipo mdomoni mwa watu na lingiine lipo mioyoni mwa watu," -Askofu Bagonza

Chanzo; Nipashe Mwanga Wa Jamii #NipasheHabari
Wakati Jenerali Ulimwengu anasoma Chuo Kikuu, chuo kilikuwa na wanafunzi mamia tu. Leo hii digrii ziko kila kata ya nchi hii. Mwambieni abadirike.
Anaposema Hakuna swali la kijinga ila kuna majibu ya kijinga, muulizeni watu wanaoitwa wajinga huwa wanauliza maswali ya aina gani? Au wanapouliza ujinga unawatoka? Ni msemo wa kizamani sana!!!!
 
Ulimwengu anapaswa astaafu na apumzike. Yeye alishakuwa kiongozi mkubwa serikalini na hakuna alichofanya na vizazi vya eneo husika kumkumbuka. Ni sawa na Jaji Waryoba..wapiga kelele. Askofu anapenda kick na makofi.
Ulimwengu bado anazungumzia Panafricanism yake. Bahati mbaya ktk nchi aliishia kuwa DC. Akajaribu kutumia udini kwa kujiita Twaha, wapi? sasa akubali tu yamekwisha.
 
Wakati Jenerali Ulimwengu anasoma Chuo Kikuu, chuo kilikuwa na wanafunzi mamia tu. Leo hii digrii ziko kila kata ya nchi hii. Mwambieni abadirike.
Anaposema Hakuna swali la kijinga ila kuna majibu ya kijinga, muulizeni watu wanaoitwa wajinga huwa wanauliza maswali ya aina gani? Au wanapouliza ujinga unawatoka? Ni msemo wa kizamani sana!!!!
Watu wanaoitwa wajinga ni wenye majibu na hoja za kijinga
 
"Aslimia 60 ya wabunge wa CCM waliopo bungeni kwa sasa hawakushinda kura za maoni ndani ya chama chao, hata wanachama wao wanajua na wanaona kabisa hawakuwachagua na hivyo wanaona siyo wa wabunge wao"- Askofu Bagonza

Hii ni kweli kabisa, na pia kwa kuongezea kwa hao 60% na hata wale wengine 40% waliobakia, wapo walioingia kwa kutokupigiwa kura na wanachi kutokana na mapingamizi ya kihuni, wapo wengi wameshinda kupitia wizi uliofanywa na kuratibiwa na vyombo vya dola, na pia wapi waliotangazwa kuwa ni washindi hata kama hawakushinda.

Bunge la sasa ni uchuro na kinyaa mbele ya watu wenye kuujali na kuushika ukweli. Ni aibu na fedheha kwa taifa letu. Ni sawa na jipu kubwa na baya lililovia kwenye naniliu, macho pima kwa woga, jaribu tu kufikiria "combination" ya harufu mbaya inayotoka hapo!

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Wakati Jenerali Ulimwengu anasoma Chuo Kikuu, chuo kilikuwa na wanafunzi mamia tu. Leo hii digrii ziko kila kata ya nchi hii. Mwambieni abadirike.
Anaposema Hakuna swali la kijinga ila kuna majibu ya kijinga, muulizeni watu wanaoitwa wajinga huwa wanauliza maswali ya aina gani? Au wanapouliza ujinga unawatoka? Ni msemo wa kizamani sana!!!!
Wewe achana na Jenerali, size yako ni Polepole.... na Shaka[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Wewe achana na Jenerali, size yako ni Polepole.... na Shaka[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Nani? Ulimwengu! Miaka ya 70 ni sawa, siyo TZ ya leo. Muulizeni alipoingia Kikwete, yeye na mwenzake Tibaijuka waliendesha kipindi cha Ulimwengu on Monday, wakizomea utawala wa Mkapa. Ilikuwaje Tibaijuka akapewa Uwaziri na yeye akaachwa pembeni? Tunamjua kuliko wewe mwenye digrii ya JF, boss!
 
Yuko vizuri Sana upstairs, CCM nzima Hakuna mwenye akili Kama yeye....mtu anakuwa Hana akili akiwa kiongozi anakuwa na akili kuwazidi wote.....ndio akina Jiwe na Chief
Hiyo akili umeipimaje? Kilichomtuma kusoma kiingereza badala ya Physics ni nini? Mwanaume mzima!
 
Back
Top Bottom