Jenerali Ulimwengu: Inanichosha kusikia sifa za Rais kila dakika

Kusema kweli inachosha sana,wanasiasa hawawezi kujenga hoja bila kutaja neo Rais........mi taarifa ya habari kwenye local channels niliacha kuangalia tangu enzi za JPM, maana DC,RC,MAWAZIRI,DAS,RAS,WAKURUGENZI etc wote wakiongea lazima neno Rais litajwe
 
Hadi kusema Rais kamtoa jalalani, yaani mtu alikuwa lecturer chuo kikuu, kumbe lile lilikuwa jalala. Watu toka JPM waliamua kujizima network kabisa, na viongozi wanabariki ujinga sasa imekuwa trend, kila mtu anasifia tu.
 
Chawa wamezidi mpaka mawaziri ni chawa,ukisimama jukwaani usipo msifu mama utaondolewa kwenye nafasi yako
 
Hizi ndio siasa za Afrika.
 
Ulimwengu yupo sahihi siku hizi sio serikali imefanya hivi, au tumetumia kodi zenu Watanzania kufanya hiki na hiki.

Nikushukuru Rais Dr kutupa hiki, kutujengea hospitali, shule barabara.

Tunakuomba Rais kama ikupendeza, chawa katika ubora wao.

Ila kuna mantiki kusifia na kujipendekeza ndio njia ya kulamba teuzi awamu hii.
 
Hata mvua ikinyesha, ni lazima kumsifu mama Dr Samia Suluhu Hassan.
Vivyo hivyo mvua ikikatika na jua likiwaka.

Pia unaweza kumsifia Rais kwa matokeo mazuri ya mitihani ya darasa la saba
 
Mbwa kabisa hii Jenerali Ulimwengu.
 
kama ambavyo inachosha kukuskia wewe Mzee Generali mtu mzima ukilalamika daily
 
Machawa wana maisha mazuri kuliko ma profesa, Machawa wapo kwenye msafara wa rais. Na rais mwenyewe alishasema chawa wake waheshimiwe. Bila uchawa hapa mjini hutoboi.

Kibaya zaid uchawa umesambaa zaid mpaka kwenye level ya kaya, Wilayan, kwenye halmashauri, Kwenye vituo vya afya, Manes wanakuwa machawa wa wabunge, sijui meya, mkurugenzi nk, kwenye makampuni hivyo hivyo.

Hii issue ya uchawa imesababisha damage kubwa sana kwenye maadili ya vijana na ile spirit tuliyojengewa na Magu, ile ya Kupambana, Kuchapa kazi, kusukuma mambo ili yaende. Awamu hii, tunafundishwa kuwa machawa. Uchawa ndo habari ya mjini, lakin uchawa una ajiri watu wangapi, ni uharibifu usio wa kawaida wa jamii.
 
1. Njaa
2. Njaa
3. Njaaa
4. Njaaa mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…