Machawa wana maisha mazuri kuliko ma profesa, Machawa wapo kwenye msafara wa rais. Na rais mwenyewe alishasema chawa wake waheshimiwe. Bila uchawa hapa mjini hutoboi.
Kibaya zaid uchawa umesambaa zaid mpaka kwenye level ya kaya, Wilayan, kwenye halmashauri, Kwenye vituo vya afya, Manes wanakuwa machawa wa wabunge, sijui meya, mkurugenzi nk, kwenye makampuni hivyo hivyo.
Hii issue ya uchawa imesababisha damage kubwa sana kwenye maadili ya vijana na ile spirit tuliyojengewa na Magu, ile ya Kupambana, Kuchapa kazi, kusukuma mambo ili yaende. Awamu hii, tunafundishwa kuwa machawa. Uchawa ndo habari ya mjini, lakin uchawa una ajiri watu wangapi, ni uharibifu usio wa kawaida wa jamii.