Jenerali Ulimwengu: Inanichosha kusikia sifa za Rais kila dakika

Tatizo ni vyombo vya habari Ili wakurushe hewani na kusikika ni lazima umsifu Rais.Ukizumgumza mawazo Yako tofauti na Rais hata kama ni mazuri,hutasikika na mtu,wanawaogopa wajiri wao ambao pia wanaogopa serikali kufungia vyombo vyao.Ni mfumo
 
Wanaochosha kusikiliZa ni hawa wenye vyeo. Mawaziri, RCs nk na wateulewote. Ukweli hata mimi nakerwa sana
 
Anachoka yeye kama nani??
 
akajambe
 
Hadi kusema Rais kamtoa jalalani, yaani mtu alikuwa lecturer chuo kikuu, kumbe lile lilikuwa jalala. Watu toka JPM waliamua kujizima network kabisa, na viongozi wanabariki ujinga sasa imekuwa trend, kila mtu anasifia tu.
Yaani ni aibu kwa Taifa

Kuna Kiongozi mmoja alinambia kuwa bila kufanya hivyo unaweza usiwepo kwenye mkeka wa Uteuzi.

Bora kubakia Mkulima wa kawaida kama nilivyo Mimi huku ukitunza heshima uliyonayo na maisha yanasonga 💪
 
Hata rais mwenyewe ana shida.

Kama mnakumbuka magufuli alimwambia kangi”unanitaja taja sana kumbe unafanya madudu”
Hawa UVCCM sio wajinga kama tunavyofikiri,ni watu ambao toka walipoamua kuingia huko ccm,walidhamilia kuwa wapigaji kwa njia yoyote itakayowezekana.
 
Kwa kweli inashangaza kila mbunge, kila mtendaji mkuu wa idara za serikali akisimama tu lazima amsifie rais kuwa ametoa fedha kujenga mradi fulani ashukuriwe. Mara rais katoa fedha za kujenga kituo cha afya, madarasa, barabara na mkadarasi yuko kazini. Mabango yamejaa kila sehemu rais atanapofanya ziara mikoani na wilaya, mwendo ni kumsifia tu kuwa katoa fedha za kujenga miradi ya wananchi kana kwamba si wajibu wake kufanya hivyo. Mpaka wenyeviti wa vijiji wanaimba mapambio ya kumsifia kwa kutoa fedha za kujenga miradi ya maji na vituo vya afya. Duh! hadi vijiweni wameanza kusifia rais kafanya vijiwe vyao mambo yawe mazuri
 
Muasisi wa huu upuuzi ni dhalimu ili kuhadaa umma kuwa anakubalika sana. Na kwakuwa watu wanapata ulaji kupitia hayo mapambio, hakuna namna upuuzi huo utaisha. Hadi aje kiongozi mwenye akili nzuri, au atakayeingia madarakani kwa uchaguzi halali.
True👍
 
Mimi sijawahi kusikia Hapo zamani haya maneno ya sifa zilizopitiliza !!
Mpaka sasa sijaelewa impact yake ni nini !!
 
Mpaka kero, nafikiri ni walaka unapita usipomtaja kwenye maelezo yako unaweza kuchukuliwa hatua, ila yule wa elimu sioni akimtaja hovyohovyo rais.
 
Mkuu una akili kama za Jiwe, pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…