Jenerali Ulimwengu: Kuna Mtanzania alitufanya Mazuzu

Jenerali Ulimwengu: Kuna Mtanzania alitufanya Mazuzu

Uzuzu upo sana tu. Tuligeuka watu wa ndio mzee
Nyie wanyonge: ndio mze
Mtapata noa wote: ndio mzee.....
Haya shangilia: ulululululuu
Kabisa mkuu... Namkumbuka sana mhe Bwege bungeni kuhusu watanzania [emoji23][emoji23]
 
Huyu nae katuchosha na neno "zuzu". Yaani kila akiipata maiki hawezi kumaliza kuongea hadi amseme Magufuli, sijui alimto..bea mke....??!!
Wengine hamuwezi kuelewa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na huo uzuzu wa kihalaiki tuliyopuliziwa kwa miaka hiyo sita. Tatizo kubwa lililotupata kama taifa miaka hii ni kusambaratika kwa umoja wa kitaifa na kubomoka kwa utaifa wetu. Ingawa chimbuko la matatizo haya ni siasa mbaya hapana shaka kwamba awamu ya tano imetupeleka mbali zaidi kiasi cha kuhatarisha uhaj wa taifa letu. Jenerali alikuwa mmoja wa vijana wa Nyerere waliomuelewa sana. Kwa umri wake Jenerali, upeo wake kifikra na kwa jinsi anavyoifahamu hii nchi, muasisi wa taifa hili na misingi ya utaifa tuliyorithishwa, haachi kushangaa ajali hii mbaya iliyotupata ya kuwa na uongozi wa aina ile ya awamu ya tano, hususan rais Magufuli. Jambo la kushangaza na kusikitisha zaidi ni jinsi ambavyo aliweza kudumisha uharibifu huo kwa muda wote na hata kujipa muhula wa pili kwa njia haramu kabisa kwa kupitia kile kile chama kinachojipambanua kuwa chama cha siasa bora zaidi katika Afrika!
 
Ukimuacha Nyerere huyu Jenerali hajawahi kumsifia rais yoyote yule . JPM hajamfanya mtu kuwa zuzu kama yeye aliwahi kuwa zuzu basi ni shauri lake mwenyewe. Mbona mimi mpaka leo hii sijavaa barakoa wala kuchanja ni kwa sababu nilikataa uzuzu.... Fedha wapige wengine sisi tuishie kudungwa sindano alafu unalia anaupiga mwingiiiiii
 
Upo sawa sana mkuu.
Lakini hoja kubwa hapa ni we are not interesting na hili neno lake ambalo ndio kaligeuza kama ngazi ya kupandia kila kukicha
Ulimwengu apande kwenda wapi ndugu yangu!!!...Nani asiyemjua!!?...
 
Kama siku Tanzania tuta kaa na kugundua mdomo wetu na umbea ndio chanzo kikubwa cha kufanya tusipige hatua.. Tuta kuwa tusha chelewa Sana....

Watu Wana tumia muda mwingi kulaumu wengine kuliko kuweka nguvu kwenye nini tufanye ili jambo kama Hilo lisiwepo Rena au tupige hatua.
 
Katiba ndio inayotoa mwanya kwa KIONGOZI kuwageuza watu kuwa mazuzu na sio mtu kama anavyozungumzia huyo jenerali,MJADALA wetu ni katiba na sio mtu mmoja aliyekufa,tukiendelea kujadili mtu ambaye hayupo na hatarudi kamwe,Basi nadhani bado tutakuwa hatujajua tatizo ni nn na tutaendelea kuwa mazuzu vilevile,na tukijifanya hatuoni tatizo atakuja mwingine zaidi ya aliyekufa na atatumia katiba hii hii hapo ndipo tutakapoona ujinga wa akina jenerali wanaotaka kutupoteza kwenye njia ambayo itasaidia kuondoa tatizo ambalo ndio MSINGI wa upuuzi wote tunaoshuhudia ktk Taifa letu.HIVYO NAWASIHI NDUGU ZANGU TWENDE MSTARI WA MBELE KUDAI KATIBA MPYA AMBAYO NDIO UTAKUWA MUAROBAINI WA MATATIZO MENGI TULIYONAYO NA TUACHE KUJADILI WALIOKUFA.
 
Sukuma gang, buana... Yaani tunasoma akina Hitler, Carl Peters... na wengineo wa 1800, 1900 na kitu. Leo eti hamtaki dikteta aliye kufa 17 march 2021 asisemwe?! Hivi mna akili kweli? Kuna somo pia linaitwa historia. Wamesoma akina Nyerere na wengine. Unasemaje - lifutwe kwenye mashule?
Fact
 
Shida ni watu si katiba. katiba si mwarobaini wa matatizo ya Tanzania na Africa kwa ujumla, watu ndiyo tatizo.
Katiba tuliyonayo inamfanya Rais kuwa Demigod lakini bado Rais anaona haimtoshi na anaamua kufanya yaliyo nje yake na hakuna muhimili wa kumzuia ilhali miimili hiyo imepewa nguvu sawa na serikali.

Hata leo tukichukua Katiba Ya Us yote bado Rais wa Tanzania anaweza fanya anavyotaka na hakuna wa kumfanya Chochote.
Trump alikuwa akienda kinyume Mahakama inamwambia"STOP". Je, Tanzania tuna mahakama ya kumzuia Rais?.
Mjomba kama huelewi maana ya katiba ni afadhali usome tu post humu na isichangie chochote umetoa mfano mzuri wa katiba ya marekani alafu hapohapo unasema katiba sio muarobaini. yaani unajitekenya mwenyewe na unacheka ww mwenyewe kweli dunia inaenda kasi sana.
 
Mjomba kama huelewi maana ya katiba ni afadhali usome tu post humu na isichangie chochote umetoa mfano mzuri wa katiba ya marekani alafu hapohapo unasema katiba sio muarobaini. yaani unajitekenya mwenyewe na unacheka ww mwenyewe kweli dunia inaenda kasi sana.
SAWA
 
Katiba mpya haiwezi kuficha ujinga wetu watanzania, matatizo mengine yapo na tunashindwa kuyakibili kwa sababu ya ujinga hivyo katiba mpya haitokuwa kichaka cha huu ujinga tulionao maana hata huku kulilia katiba hadi leo ni matokeo ya ujinga wetu.
 
Kwan Ulimwengu Kama yeye na uzee wote huo alishawahi kuifanyia nini Tanzania?Au ndio story tu za kumsema marehemu wakati huna kitu cha maana ulichowahi kufanya.
Akitoa mada Kwenye Mkutano wa TCD, Generali Ulimwengu alisema, kuna Mtanzania Mmoja alikufa miaka michache iliyopita alitupulizia uzuzu na wote tukawa mazuzu.

Geberali apewe ulinzi

Tazama Video
View attachment 2182469
 
Katiba mpya haiwezi kuficha ujinga wetu watanzania, matatizo mengine yapo na tunashindwa kuyakibili kwa sababu ya ujinga hivyo katiba mpya haitokuwa kichaka cha huu ujinga tulionao maana hata huku kulilia katiba hadi leo ni matokeo ya ujinga wetu.
Kusolve tatizo lazima uwe na pa kuanzia.
Msingi wa uendeshaji wa nchi ni KATIBA!
KATIBA mbovu ndo imechangia kuwafanya hao Watanzania kuwa jinsi walivyo!!
 
JPM alishakufa, haijalishi alifanya mazuri au mabaya....hebu sasa tupambane na yetu sisi tuliohai na tuache kulialia, He has done his part, tuwe na shukrani, kama wengine mnamuona alitufanya mazuzu wapo wanaoona alikuwa the best pia, na hii ipo kwa kila binadamu..
Huo ndio ukweli. Kwasasa tupambane na mfumko wa bei had vita URUSI iishe.
 
Back
Top Bottom