Jenerali Ulimwengu: Tanzania ni kama tumerudi kwenye mfumo wa chama kimoja cha siasa

Jenerali Ulimwengu: Tanzania ni kama tumerudi kwenye mfumo wa chama kimoja cha siasa

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
1776861187941.png


Licha ya Mataifa ya Afrika kuridhia mfumo wa vyama vingi kuanzia miaka 1989, baadhi yao yameshindwa kuendeleza demokrasia ya vyama vingi, huku watawala waliochaguliwa na wananchi wakiziendesha nchi zao kidikteta.

Tanzania iliyoridhia mfumo huo mwaka 1992, imepita katika milima na mabonde, lakini kwa sasa demokrasia imefika njiapanda, ambapo chama tawala CCM kimeonekana kutumia mabavu kubaki madarakani.

Akijadili suala hilo, Mwandishi wa habari mkongwe, Jenerali Ulimwengu, amechambua kitabu chao kinachoitwa Pan-Africanism: The Remembering of a Nation, alichokiandika akishirikiana na Dk Azaveli Lwaitama.

Kitabu hicho kilizinduliwa Machi 25, 2026 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau wakiwamo wanasiasa, wasomi na waandishi wa habari.

Akizungumza katika mahojiano hivi karibuni kuhusu maudhui ya kitabu hicho, Jenerali Ulimwengu anaeleza…

Swali: Nini hasa kiliwasukuma kitabu hiki na mnadhani hii mada za kitabu zinaeleweka kwa vijana sasa maana kimejaza historia za zamani kidogo?

Jenerali: Ni kweli mada hizi zinaweza zisieleweke kwa vijana wa sasa kwa sababu vijana wengi hawana ufahamu na uelewa mkubwa kuhusu dhana nzima ya Umajumui wa Afrika.

Ni dhana ambayo wanaijua labda wameisikia katika muktadha mbalimbali lakini hawaielewi vizuri. Kwa hiyo tumedhani kwamba ni muhimu sasa waielewe historia.
pan-africanism-cover2.png


Swali: Ulipataje wazo la kuandika hiki kitabu?

Jibu:
Mimi nilikuwa nafanya kazi pamoja na shirika moja la Umoja wa Mataifa ambalo lilitaka nifanye utafiti kuhusu Umajumuhi wa Afrika, halafu niandike vitu ambavyo vinaweza vikawekwa katika jumba la maonyesho Addis Ababa, Ethiopia.

Katika kufanya kazi ile, nikagundua kwamba kuna vitu vingi sana ambavyo hata vijana wetu wangevipata vingekuwa vya maana sana kwa sababu si kila mtu atapata nafasi ya kusafiri kwenda Addis Ababa na kutembelea 'Africa Hall' ambapo yale maonyesho yanaonyeshwa sasa hivi.

Kwa hiyo nikaamua nimpate Dk Azaveli Lwaitama, ambaye alikuwa akinisaidia kufanya utafiti wakati nafanya kazi hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Nikamwambia kwa nini tusitumie ujuzi huu tulioupata katika kufanya hii shughuli ili kutoa taarifa kwa vijana wetu waelewe Umajumui wa Afrika ni kitu gani na kadhalika. Akakubali.

Kwa hiyo tukakaa chini tukaamua kwamba tufanye kitu kimoja.

Kwanza tuangalie ni maeneo gani ambayo yanahusu Umajumui wa Afrika, halafu tuyaainishe kama sura hivi. Sura ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne, ya tano... tumefika hadi sasa tumefika sura kumi ambazo tumeziandikia notisi fupi fupi, lakini ambazo tutakuja kuzikuza baadaye ili kila mmoja isimame yenyewe katika kijitabu kidogo, vijitabi vidogo, kurasa zisizozidi mia moja.

Ya kwanza ambayo tumeitoa juzi, tumeichapa na iko tayari mtaani, inaitwa Pan-Africanism: The Remembering of a Nation.

Pan-Africanism: The Remembering of a Nation ina maanahiyo ni title ya jumla, yaani 're-membering' si ya kukumbuka, ni 're-membering' kwa maana ya kurudisha wanachama pamoja. 'Members' maanake ni viungo, limbs na sehemu za mwili ambazo zilikuwa zimetapakaa kila mahali, kuzikusanya na kuzileta pamoja ili kiwe kitu kimoja.

Tukaanza hii handbook namba moja, tunazungumza juu ya Origins and Philosophical Foundations. Mwanzo, chanzo kabisa misingi yake ya kifalsafa ni nini?

Tukaona na tumeandika kwamba ni kutokana na wale Waafrika walioibwa katika nchi zetu za Kiafrika na wakasafirishwa kwenda nje kwa kulazimishwa na watekaji wa nje katika utumwa tunaita Trans-Atlantic Slave Trade—ambao walijikuta Marekani Kaskazini na Kusini, na Caribbean na kwingine kote walikopelekwa duniani.

Wakatumikishwa kama punda, kama wanyama wa kubeba mizigo na kujenga nchi za watu wengine. Huko ndio wakagundua kwamba wana kitu kinawaunganisha; wanafanana fanana katika tabia zao, tamaduni zao, nyimbo zao, ngoma zao, fikra zao, na jinsi wanavyoona mizimu yao na wanavyoiabudu na kadhalika.

Ilikuwa lazima baada ya kuwa wametolewa nje ya Afrika ndio wamejitambua, kwa sababu walivyokuwa Afrika walikuwa ni watu mbalimbali sana.

Kulikuwa na Bakongo, kulikuwa na Bandundu au kulikuwa na Wayoruba, kulikuwa na Waashanti, kulikuwa na Wolof... Lakini walivyojikuta katika wamekuwa wametolewa nje ya Afrika, ndio kwa mara ya kwanza wakajitambua kwamba wana vitu vinafanana.

Sasa vizazi vilivyofuata baada ya hapo hapo tunazungumza mwaka 1890, 1900 na kadhalika—ndio katokea kizazi sasa cha wajukuu wa hawa watumwa ambao walianza wamesoma kidogo, wamepata uelewa wa dunia, wamepata maelezo kwa nini walikamatwa wakauzwa kama samaki na wakafanyishwa kazi kama punda, ndio wakajua kwamba kuna umuhimu wa kujiunga tena na Afrika.

Kwanza waijue vizuri Afrika kama chimbuko lao na warudishe ile link kati yao na Afrika yenyewe.

Hivyo wakaanza, walikuwa hawa walioanza miaka ya 1900 walikuwa ni watu wa Caribbean na Marekani, na wengine walikuwa Ulaya kama Uingereza au Ufaransa na kadhalika.

Lakini zimekwenda hivi ilivyofika mwaka 1945, ikawa sasa Congress zile zimeshafanyika karibu tatu nne, ile ya mwaka '45 iliyofanyika Manchester ikawa na Waafrika wengi sasa. Waafrika waliotoka kwenye bara la Afrika—ndio Jomo Kenyatta alikuwepo, George Padmore alikuwepo, W.E.B. Du Bois alikuwepo, nani Nkrumah Kwame alikuwepo, Nnamdi Azikiwe alikuwepo na kadhalika.

Hiyo harakati ikaendelea mpaka ilivyokuja Congress ya sita iliyofanyika Dar es Salaam kama inavyoelezwa kwenye kitabu hicho mwaka '74, na halafu mwaka '79 ikawa ipo Congress ya saba iliyofanyika Kampala, Uganda.

Kwa hiyo hiyo ndio scheme nzima ya juhudi hizi za kutengeneza hizi handbooks ambazo zinaweza zikasomwa na vijana ambao wapo high school, tuseme A-Level na junior university au junior college.

Nadhani baadaye mwaka huu tutatafsiri kile kijitabu cha kwanza katika Kiswahili, na vile vile tutakiweka kwenye e-books ili kiweze kusambaa kwa watu wengi zaidi.

Swali: Miaka 60 ya uhuru wa nchi za Afrika ni kama vile haijaleta maana kwa wananchi, maana wale walioleta ukombozi ni kama wamejenga tawala za kidikteta, je mtaeleza kwenye matoeo mengine ya vitau vyenu?

Jibu: Ni kweli. Tutavieleza kwamba matarajio ya Waafrika baada ya Afrika kama sisi Tanzania na nchi nyingine ziizofuata kama Zimbabwe mwaka 1980, Namibia na baadaye Afrika Kusini mwaka 1990, mambo hayajawa sawa.

Baadhi ya nchi za Afrika zilipopata uhuru zilijikuta zinawapeleka watu wao utumwani. Tusifanye kosa la kudhani kwamba uhuru ulikuwa ni jambo baya, hapana. Uhuru ulikuwa ni jambo jema na tulilisherehekea na ulitupa nafasi ya kufanya mambo mengi mema.

Kwa bahati mbaya baadhi yetu katika wazazi wetu na vizazi vilivyotangulia, wakawa hawajashibishwa vya kutoka juu ya maana ya uhuru, kwamba uhuru huu unatakiwa kuwa wananchi sio wa watawala.

Uhuru wa Taifa unatakiwa upelekwe kwenye uhufu wa wananchi.

Kama unavyoona baada ya uhuru yakafuata mapinduzi kwa baadi ya nchi za Afrika. Ni wale wababe walioona kwa nini waanye kazi kwa watawala wa kiraia kushika madaraka na sasa Umoja wa Afrika unakataa matumizi ya jeshi kuchukua madaraka ya kisiasa.

Yamekuwa ni malumbano makubwa sana, wengine wanasema kama hawa watawala wa kiraia wanatumia nguvu za kijeshi kwa nini tusiwaachie jeshi wenyewe waendeshe kwa sababu hata hawa waliovaa nguo za kiraia matendo yao ni ya kijeshi tu.

Huo mjadala uendelee, kwamba unapotumia Jeshi kugandamiza watu wako na kuwanyima uhuru na kile wanachohisi kuwa wanakikosa, hatimaye unakaribisha jeshi.

Ni somo linguine tutakaloliweka katika orodha ya vitabu hivi. Tutaangalia jinsi tulivyopata uhuru, jitihada zote tulizopitia na utawala huu ulivyoshindwa katika nchi nyingi na hatimaye kukawa na mapinduzi ya kijeshi katika nchi nyingi, ukiangalia Nigeria, Ghana, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati na nchi nyingine za Afrika na jinsi watu wanavyosika kusema sasa imetosha, tutafute njia mbadala ya kuendesha nchi zetu.

Ndio maana ukiangalia Afrika katika miaka ya 1990, nchi nyingine zilianza mmwaka 1989, kukawa kuna jitihada za kuangalia tawala za Afrika na jinsi zinavyyoendesha nchi zetu na kubadilisha kutoka utawala wa chama kimoja na kwenda vyama vingi.

Pamoja na kwamba ukiangalia nchi kama Tanzania tulitoka kwenye chama kimoja kwenda vyama vingi, sasa ukiangalia ni kama tumerudi tena kwenye mfumo wa chama kimoja, lakini hii kuonyesha kuwa haijanyooka, kuna kupanda na kushuka.

 

Attachments

  • pan-africanism-cover2.png
    pan-africanism-cover2.png
    215 KB · Views: 28
Hii ni hatua kubwa sana kwao. Kuandika kitabu au kutoa machapisho mbalimbali kunayafanya mawazo ya mwandamu kuendelea kuishi hata baada ya yeye mwenyewe kufa.
 
View attachment 3577415

Licha ya Mataifa ya Afrika kuridhia mfumo wa vyama vingi kuanzia miaka 1989, baadhi yao yameshindwa kuendeleza demokrasia ya vyama vingi, huku watawala waliochaguliwa na wananchi wakiziendesha nchi zao kidikteta.

Tanzania iliyoridhia mfumo huo mwaka 1992, imepita katika milima na mabonde, lakini kwa sasa demokrasia imefika njiapanda, ambapo chama tawala CCM kimeonekana kutumia mabavu kubaki madarakani.

Akijadili suala hilo, Mwandishi wa habari mkongwe, Jenerali Ulimwengu, amechambua kitabu chao kinachoitwa Pan-Africanism: The Remembering of a Nation, alichokiandika akishirikiana na Dk Azaveli Lwaitama.

Kitabu hicho kilizinduliwa Machi 25, 2026 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau wakiwamo wanasiasa, wasomi na waandishi wa habari.

Akizungumza katika mahojiano hivi karibuni kuhusu maudhui ya kitabu hicho, Jenerali Ulimwengu anaeleza…

Swali: Nini hasa kiliwasukuma kitabu hiki na mnadhani hii mada za kitabu zinaeleweka kwa vijana sasa maana kimejaza historia za zamani kidogo?

Jenerali: Ni kweli mada hizi zinaweza zisieleweke kwa vijana wa sasa kwa sababu vijana wengi hawana ufahamu na uelewa mkubwa kuhusu dhana nzima ya Umajumui wa Afrika.

Ni dhana ambayo wanaijua labda wameisikia katika muktadha mbalimbali lakini hawaielewi vizuri. Kwa hiyo tumedhani kwamba ni muhimu sasa waielewe historia.
View attachment 3577416

Swali: Ulipataje wazo la kuandika hiki kitabu?

Jibu:
Mimi nilikuwa nafanya kazi pamoja na shirika moja la Umoja wa Mataifa ambalo lilitaka nifanye utafiti kuhusu Umajumuhi wa Afrika, halafu niandike vitu ambavyo vinaweza vikawekwa katika jumba la maonyesho Addis Ababa, Ethiopia.
P
 
Back
Top Bottom