Sawa nimekuelewa. Unaweza kuleza kidogo mapato yatakayopatikana baada ya kupanda kwa mara ya kwanza?
Katika greenhouse ya 8m x 15m utapanda miche 580 ya nyanya au pilipili hoho au biringanya au matango au nyanya chungu au bamia na mazao mengine mengi ambayo yanahitaji kulimwa kwa uangalifu namna hiyo.
Kama utafuata masharti kwa umakini (kumwagilia kwa wakati, kuweka mbolea husika za kutosha - hii utajua baada ya kuwa umefanya soul test na water test), kupanda mbegu bora na zenye historia nzuri ya kuzaa sana, kuzuia magugu kwa kupalilia au kuweka mulch, kuhakikisha unachunguza mimea kila wiki au siku ili kugundua mapema kama umeingiliwa na wadudu au ugonjwa na kuutibu mara moja nk...Bila kusahau kuzuia watu kuingia kiholela kwani huwa wanajisahau na kugeuza greenhouse ukumbi wa wageni kushangaa... lol
Mfano umelima nyanya kwa kufata masharti hayo, unataraia kuanza kuvuna mwezi wa tatu baada ya kuhamishia miche kwenye matuta yako (kumbuka miche inapandwa kwa udogo maalumu (potting mix) ndani ya greenhouse na kuna masharti yake ambayo ntakufundisha pia utakaponunua kutoka kwangu...), Na utaendelea kuvuna hadi miezi kumi na mbili (mwaka mmoja), hii itakupa tani 25-30 za nyanya kwa mwaka, na pili pili hoho ni hivyo hivyo tena zenyewe zinayield zaidi japo zina masharti mengine tofauti na ya nyanya...
Tani 30 za nyanya roughly ni kama mil 17-23, Sasa ukiwa na greenhouse usiridhike na mauzo haya, jaribu kununua packaging materials na utafute sehemu ya kusupply either kwa wiki au siku chache, hii itakupa minimumum sh 100 kwa kila nyanya utakayovuna, na tani moja ya nyanya ina zaidi ya nyanya elf 50, kwa kufanya hivi unatarajia kukuza mauzo na kuweza kufikia hadi mil 40 kwa mwaka kama utakuwa makini.
NB: HAYA NI MAKADIRIO TU, SIO LAZIMA UTAYAFIKIA AU KUYAPATA... Uhalisia wa biashara na kilimo ni tofauti sana na projection za kitaalamu. Hizi ni kukupa muongozo tu lakini hupaswi kukosa nusu ya makadirio kama upo makini...
Nadhani nimeeleweka.
NB: Kuna option nyingine ya kuprocess nyanya zako mfano kutengeneza JAM, Paste, Puree nk...