Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu


Karibu sana,
Tunaweza kuja kukujengea popote pale ulipo nchini, gharama ya kututoa Dar Es Salaam ni laki5 tu (500,000) hii ni gharama ya kusafirisha mafundi, material, malazi, na inflation ya vifaa vya ujenzi kama misumari mbao nk.
Kuhusu mbao tunazotumia Nilishalijibu hili hapo juu (tunatumia Mikaratusi yaani miti ambayo Tanesco wanatumia kusambaza umeme kwa nduzo zake)
Kuhusu malipo, Yes Uko sahihi kabisa, unalipa kwanza ndio tunakuja kukujengea. Kwa nature ya biashara ilivyo, hatuwezi kupokea installments au kuleta vifaa mpaka site kwako kisha utulipe baadae. Imagine Tusafiri watu watano kutoka Dar mpaka mbeya, na kilo zaidi ya 700 za mizigo halaf tufike huko simu haipatikani itakuwaje?? Im not saying kwamba hiyo itakuwa case juu yako, lakini kuna mengi yanayosababisha hili, kama vile kupotea au kuibiwa simu nk...

Kwa maswali zaidi unaweza kupiga simu nikakuelewesha kwa kina.

Karibu sana.
 
mamaNa,

Just in summary!

2.5mil inakusanya nini?

Na nini kiko nje ya hii package ambacho nitatakiwa kuwa nacho? Mi nina shamba tu!!

In summery 2.5m ni bei ya mauzo ya material ya kujengea greenhouse bila nguzo, misumari, tank la maji na ufundi.
Kama umeshawahi kujenga au unafahamu ujenzi wa greenhouse ulivyo na unataka kujenga mwenyewe hiyo ndio bei yake.
Sasa kama unataka tukujengee na kusimamia ujenzi mzima itaongezeka mil1 tu kama uko dar na 1.5 kama uko nje ya dar.
Hii 3.5 au 4 ni gharama ya material yote ya kujengea greenhouse na ufundi.
Utakachopata baada ya kulipa 3.5/4m ni complete greenhouse inayofanya kazi na itakayokuwa tayari kupandwa chochote kulingana na mahitaji ya mteja.
Kama huna miche na unahitaji miche itoke kwetu basi unaongeza 290,000 kwa ajili ya miche 580. Kifupi ili uwe na shamba lenye mazao unahitaji roughly 4,040,000 (kama ni Dar) na 4,540,000 (kama ni nje ya Dar), hii ikiwa ni gharama ya kupima udongo, maji, kujengewa greenhouse na kuoteshewa miche.
Kitakachobaki hapo ni wewe kuisimamia na kuvuna tu, na mwaka unaofata utaingia gharama ya 290,000 kwa ajili ya miche, na hizo milioni kadhaa hazitojirudia tena kwa miaka mitano-saba.
Nadhani nimeeleweka.
Karibu tena kwa maswali zaidi.
 
Just in summary!

2.5mil inakusanya nini?

Na nini kiko nje ya hii package ambacho nitatakiwa kuwa nacho? Mi nina shamba tu!![/QUOTE]


Structure kulast miaka 10 sio tatizo, kama umesoma post za juu utaona nimeshajibu tunafanyaje ili kuhakikisha hilo. Kuna special treatment tunafanya kuzuia mchwa, wadudu na kuoza.

Karibu sana.
 
Asante kwa Ufafanuzi mzuri sana. Hapo nimeelewa kabisa.Kilichobaki ngoja nikamilishe hesabu ya hiyo hela kabisa ndio nikutafute.Shamba lipo Ruvu Kijiji cha kwala naamini hapo utafanya bei ya Dar es salaam. hahaaa!
 
Asante kwa Ufafanuzi mzuri sana. Hapo nimeelewa kabisa.Kilichobaki ngoja nikamilishe hesabu ya hiyo hela kabisa ndio nikutafute.Shamba lipo Ruvu Kijiji cha kwala naamini hapo utafanya bei ya Dar es salaam. hahaaa!
Karibu sana ndugu, Japo wilaya mpya zimeanzishwa, sidhani kama kwala nayo imeingia dar es salaam. Hahaha
 

Vipi Mbolea na Madawa??
 
Vipi Mbolea na Madawa??
We advice on organic ways of farming. Mbolea na Madawa ni vya asili. Kuhusu mbolea tunahitaji kupima udongo kwanza ili tujue ni aina gani ya mbolea na kwa kiwango kipi kinatumika. Kuhusu madawa tutadiscuss magonjwa yatakapoanza kutokea (if any), kwani kila ugonjwa na dawa zake, na muda wake wa kupuliza au kuweka.

NB: Most ya haya maswali yameshajibiwa hapo juu.
Karibu sana.
 

Ila kusema ukweli mamaNa bei yako kidogo iko juu,
Maana kwa Tshs 2.5Million napata vifuatavyo tu kutoka kwako;

  1. 1/8 of an acre drip lines,
  2. Polythene Cover (UV400 Protected sheets),
  3. 70% Micron insect Netting...(Sijaelewa tofauti yake na ya #2)

Vingine vyote nanunua mwenyewe, huoni Mkuu wangu hizi hapo juu nikiungaunga mitaani kimoja kimoja mbona kama inakua cheaper Mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Bei iko juu ukilinganisha na ya nani? on each comparison there must be atleast two to compare. Unajua Mita moja ya mraba ya Poly cover inagharimu kiasi gani mpaka inaingia nchini?
Kama kuna cheaper option I suggest you go for it, every penny counts!!. Lakini kumbuka hii ni sayansi (inasomewa) na sio tu ushindani wa bei au kutaka kujilimbikizia faida.
Ikiwa umeshindwa kutofautisha no 2 na 3, sidhani kama utaweza kujenga mwenyewe kwa "Ku unga unga".
 
Ahsante mamaNa, ndio nimeuona leo huu uzi, lakini nimehamasika sana kuimplement huu mradi. Naomba ushauri wako, kama namudu gharama za kuwa na 2 greenhouses za ukubwa wa 30m x 15m..je, unanishauri nijenge zote kwa wakati mmoja na kuanza kilimo, au nianze na moja at a time ili kujifunza na kupata experience kisha ndio niongeze greenhouse nyingine? Je, katika shamba la hekari moja, naweza jenga greenhouse ngapi za ukubwa wa 30m x 15 ukizingatia spacing between greenhouses kitaalamu? NB: Ningependa kutembelea shamba lako la mfano Kigamboni jumamosi, unapatikana siku hiyo?
 

Karibu sana Riwa, katika shamba tambarare la hekari moja unaweza kujenga greenhouses 4 za 15*30, lakini kwa mkulima ambaye hajawa na utaalamu wa kutosha ni vema akaanza na size ya 8*30, na hizi zitaingia nane kwenye hekari moja. kuna kuwa na spacing ya mita mbili btwn kila greenhouse parallel na 5m spacing horizontal.
Unaweza kumudu greenhouse 2 kwa kuanzia kisha kadri unavyokuwa kiukulima utakuwa ukiongeza kadri ya mahitaji.
Je ungependa kuziweka wapi greenhouses zako?
Hakikisha una uhakika na soko la kutosha kabla hujajaza heka yako kwani mazao ya heka moja ni ziaidi ya tani 400 kwa mwaka.
Nipigie simu tufanya mpango wa kuonana ana kwa ana nikushauri zaidi.

Karibu sana.
 

Ahsante tena mamaNa, nimeshachukua namba yako nitapiga kuconfirm. Quick question..kwa hiyo greenhouse ya size ya 8*30, inagharimu kiasi gani mkinijengea up to full functional greenhouse?
 
Last edited by a moderator:
Ahsante tena mamaNa, nimeshachukua namba yako nitapiga kuconfirm. Quick question..kwa hiyo greenhouse ya size ya 8*30, inagharimu kiasi gani mkinijengea up to full functional greenhouse?

Itakugharimu 7.4m kwahiyo kwa 8 utagharimika almost 60m.
Karibu sana.
 
Last edited by a moderator:
 
 
 
Last edited by a moderator:
Nunavutiwa na huu mradi,hebu tueleweshe kidogo hii greenhouse...and how effective it is!
 
Mamana naomba unisaidie, mi nna kiwanja heka moja huko kigamboni lkn ardhi yake ni kichanga na nnataka kununua greenhouse huku uingereza. ..je naweza watumia nyie kwa kuifunga na kufanya tathmini nyingine za ulimaji? Gharama zake hapo zinaweza kuwa kiasi gani kwa kukisia?
 
 
Nunavutiwa na huu mradi,hebu tueleweshe kidogo hii greenhouse...and how effective it is!
Mkuu nadhani Kila unachotaka kufahamu kipo katika uzi huu huu. Pitia post zote utaelewa kinaga ubaga. Nimejibu maswali mengi sana na hili ni moja wapo.

Karibu sana.
NB: Kama unahofia muda wa kuisoma yote basi naomba tuwasiliane kwa simu 0714881500, tutaeleweshana vema kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…