sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
offcourse ni vizuri kijana unamkuta kapanga apartment yake ama self contained, ana usafiri wake, biashara ama kazi inamlipa fresh, ana mke na watoto wawili tayari, n. k lakini kipengere kinakuwa kwamba sehemu anayoishi ni ya malipo kwa kila mwezi bado hana pake.
Jenga kwako hata kama ni nyumba ya nyasi, ilimradi pawe pako tujue ni pako unapamiliki wewe.
Msiba ukitokea ni ngumu kuja kuomboleza ulikopanga maana si utamaduni wetu huu na hata mwenye nyumba hawezi kuruhusu maombolezo kwenye sehemu yake ya biashara, maiti itabidi isafirishwe iende kuombolezewa kwa wanafamilia au ndugu wenye nyumba zao hata kama ni za nyasi na hapa ndipo tunapojua thamani ya kwako.
Kujenga ni muhimu ili hata ikitokea umetangulia mbele za haki basi Familia (Watoto na Mama yao) wasipate usumbufu wa kodi za kila mwezi, Tena hapa mara nyingi wanahme wamewazidi wake zao vipato itakuwa ngumu sana mwanamke kubeba huu mzigo, matokeo yake atashindwa itabidi yeye na watoto wahamie nyumba za watu wengine, hapa manyanyaso huwa hayakwepeki na wataoathirika zaidi ni watoto.
Ushauri wangu tu hasa kwa vijana wenye afya mnaoweza kupata ridhki, panga sehemu ya kuishi uanzie maisha sio kukamilisha, jenga kwako kulingana na uwezo wako, hata kama ni nyumba ya matofali ya kuchoma... harufu za pilau za majirani zisikufanye ule mlo moja wa pilau kwa kujibana wakati unaweza kula kande mara 3 kwa siku.