Jenga kwako, usiridhike na vyumba / apartment za kupanga! ukifariki msiba utaombolezwa kwenye apartment? watoto wataishi wapi kodi ya mwezi ikiisha?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
offcourse ni vizuri kijana unamkuta kapanga apartment yake ama self contained, ana usafiri wake, biashara ama kazi inamlipa fresh, ana mke na watoto wawili tayari, n. k lakini kipengere kinakuwa kwamba sehemu anayoishi ni ya malipo kwa kila mwezi bado hana pake.

Jenga kwako hata kama ni nyumba ya nyasi, ilimradi pawe pako tujue ni pako unapamiliki wewe.

Msiba ukitokea ni ngumu kuja kuomboleza ulikopanga maana si utamaduni wetu huu na hata mwenye nyumba hawezi kuruhusu maombolezo kwenye sehemu yake ya biashara, maiti itabidi isafirishwe iende kuombolezewa kwa wanafamilia au ndugu wenye nyumba zao hata kama ni za nyasi na hapa ndipo tunapojua thamani ya kwako.

Kujenga ni muhimu ili hata ikitokea umetangulia mbele za haki basi Familia (Watoto na Mama yao) wasipate usumbufu wa kodi za kila mwezi, Tena hapa mara nyingi wanahme wamewazidi wake zao vipato itakuwa ngumu sana mwanamke kubeba huu mzigo, matokeo yake atashindwa itabidi yeye na watoto wahamie nyumba za watu wengine, hapa manyanyaso huwa hayakwepeki na wataoathirika zaidi ni watoto.

Ushauri wangu tu hasa kwa vijana wenye afya mnaoweza kupata ridhki, panga sehemu ya kuishi uanzie maisha sio kukamilisha, jenga kwako kulingana na uwezo wako, hata kama ni nyumba ya matofali ya kuchoma... harufu za pilau za majirani zisikufanye ule mlo moja wa pilau kwa kujibana wakati unaweza kula kande mara 3 kwa siku.
 
Kikubwa mjengee mke wako mazingita ya kuingiza pesa Pia waandalie watoto mazingira mazuri ya kusoma kama kuwawekea akiba ya ada kwenye account. .

ukifa huna kitu mke wako atatembea na mashemeji zake wote😞 Nishawahi tembea na mke wa marehemu rafiki yangu hili swala linanitafuna sana.
 
Hebu ngoja tupate maoni mengine kutoka kwa "baba mwenye gari" akimjibu baba mwenye nyumba.🤔
 
Kujenga ni akili za kimaskin maisha sio nyumba tu na maitaji ya familia ni meng zaid ya iyo nyumba unayofikili

Mawazo ya kuwaza kufa ni mawazo ya kifukala sana sabu unaweza ukafa na iyo nyumba ulojenga watoto wakauza na wakarudi upangajini nazan kuna haja ya kuwekeza ktk familia somesha watoto shule nzuri lea watt ktk maadili mema wape chakula bora na jali afya zao na etc , ata ukifa watajiogoza wenyewe
 
Huwa nashangaa unawezaje kupanga sehemu kubwa na nzuri afu ushindwe kujenga kwako?nyumba ni muhimu au wenye nyumba ni wachawi wanaloga wapangaji wasijenge?
 
Tatizo unawaza kufa tu. Fikiria umeishi na upo kwenye hali ambayo huwezi tengeneza kipato cha kulipa kodi.

Ukiwa na nyumba hapo nje utalima mchicha, ikipatikana elfu mbili utanunua unga na mtalala. Kasheshe ni ukiwa huna pa kulala, mkeo utamlaza kwa marafiki?
 
Kwani mtu akifa ana lingine la ziada?

Mkitaka mumzike mkitaka mumuache hilo halimhusu na halitobadili chochote kwake mfu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…