Jengeni viwanda muajiri vijana sio shule wakasome watoto

Jengeni viwanda muajiri vijana sio shule wakasome watoto

Me too

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
7,388
Reaction score
9,333
Ifahamike swala la Elimu ya msingi kwa sasa lipo vizuri sana naipongeza serikali.

Kiongozi yeyote atakae weza kutatua tatizo la ajira kwa kujenga viwanda kisha kuwaajili watu pasipo upendeleo.

Nasema Hivi huyo atashinda hata urais kwa chaguzi zijazo.

Kwa nini? Ikiwa rundo kubwa ni la vijana ndio hawapigi kura sababu ya kukata tamaaa ajira hamna wanaona muda wa kwenda kituoni kupiga kura ni bora nikauze karanga stend, au muda wa kwenda kujiandikisha / rekebisho daftari la kudumu la wapiga kura ni bora nikauze zabibu.

Sasa kiongozi anaetaka ushindi mzuri hasa kutoka kwa vijana hawa, awakomboe kwakile kinacho wa keepbusy kwa kujenga viwanda, awaajili tena kwa sharti kila mmoja lazima apate kadi ya kupiga kura (nazani uandikishaji utafanyika 2024) tena iwe karibu na eneo la kazi, ndani ya kiwanda hicho wawe wanapewa Elimu ya umuhimu wa kupiga kura Mara moja per month.

Sio tu watu mnajenga shule eti zitakuwa za misaada kwa watoto, wakati Elimu ishakuwa bure (msaada). Mnakazania kutengeneza maenjoy mengi kwa watoto nia mpate mvuto wa uongozi huku mnawaacha baba na mama wa watoto hao mnao wataka kwenye hizo enjoi zenu wakisota kutafuta mkate wa siku bila mafanikio.

Mnawadangadanganya na hizo enjoi zenu wakati watoto hao hata hawajui kadi ya kupiga kura ndo nini.

Mgomboe wazazi wa hao watoto mnao wataka kwenye maenjoi yenu ili wazazi hao wapate kuwapa Elimu ya baadae kuhusu upigaji kura na namna ya kuchagua kiongozi bora kwa Taifa, na sio BORA kiongozi.
 
Sioni hoja yenye mashiko ndugu, uwekezaji katika elimu ni muhimu sana na bado hujafikia hatua yakusema inatosha, bado Kuna idadi kubwa ya walimu inahitajika,vyumba vya madarasa, maabara za kisasa, vitabu na miundombinu kadha wa kadha kiufipi suala la elimu ni mtambuka tofauti na unavyolichukulia.

Huko viwandani tutapeleka watu gani kwaajili ya uendeshaji wa viwanda hivyo Kama wananchi wasipopewa elimu? Au unataka ajira za watanzania ziwe zile za vibarua tu.

Jambo la msingi ni serikali sasa kupitia taasisi zake waweke mazingira rafiki kwa sekta binafsi hili litasaidia sekta binafsi kuanzisha shughuli mbalimbali vikiwemo viwanda na kutatua au kupunguza kabisa tatizo la ajira nchini. Sekta binafsi ndiyo injini ya maendeleo katika taifa lolote lile.

Hivyo basi hakuna uhusiano wowote Kati ya utoaji elimu na ukosefu wa ajira nchini.
 
Sioni hoja yenye mashiko ndugu, uwekezaji katika elimu ni muhimu sana na bado hujafikia hatua yakusema inatosha, bado Kuna idadi kubwa ya walimu inahitajika,vyumba vya madarasa, maabara za kisasa, vitabu na miundombinu kadha wa kadha kiufipi suala la elimu ni mtambuka tofauti na unavyolichukulia.

Huko viwandani tutapeleka watu gani kwaajili ya uendeshaji wa viwanda hivyo Kama wananchi wasipopewa elimu? Au unataka ajira za watanzania ziwe zile za vibarua tu. Jambo la msingi ni serikali sasa kupitia taasisi zake waweke mazingira rafiki kwa sekta binafsi hili litasaidia sekta binafsi kuanzisha shughuli mbalimbali vikiwemo viwanda na kutatua au kupunguza kabisa tatizo la ajira nchini. Sekta binafsi ndiyo injini ya maendeleo katika taifa lolote lile.

Hivyo basi hakuna uhusiano wowote Kati ya utoaji elimu na ukosefu wa ajira nchini.
Level niliyoiongelea ni MSINGI ( drs 1-7). Je hamna shule za msingi kwenye kata / mtaa wako?
 
Level niliyoiongelea ni MSINGI ( drs 1-7). Je hamna shule za msingi kwenye kata / mtaa wako?
wewe wasema kwakua upo mjini tu, kwataarifa yako mpaka leo hii wadogo zetu huko vijijini wanatembea kilometer kadhaa kuzifika shule wanazosoma.
 
Back
Top Bottom