Jengo la Freemason Posta linafanyiwa marekebisho

Jengo la Freemason Posta linafanyiwa marekebisho

Ni jumuiya ya siri yenye wanachama wa kuchaguliwa kwa uangalifu mkubwa sana na baadhi ya vigezo ni
1. Uwezo was kifedha
2. Nidhamu ya hali ya juu kwenye kila kitu
3. Cycle ya watu wako
4. Usiri
5. Ukimya
6. Imani kwa Mungu
7. Rekodi zero ya kashfa na mambo ya kesi
8. Uwezo wa akili ( hawachukui watu wajingajinga
9. Heshima na adabu kwa watu wa kaliba zote
10. Kujituma kwenye kila kitu nknk

Sent using Jamii Forums mobile app
Kigezo namba 8 ndo kinafanya Members wengi humu jukwaani hawapo🤣

Karibuni kwenye secret society
 
Unamualika GENTAMYCINE aje atoe ufafanuzi unadhani anajua ni kuhusu freemason? Bora mshana jr huyo sina shaka nae atakua anawajua viziri jamaa hao. Kwa upande wa Maxence Melo huyo tayari ameandika uzi kuwahusu freemason in and out utafute ukasome. By the way hao jamaa ni jumuiya ya watu fulani katika ushirika wao wa kusaidiana na kusaidia wengine mambo mbalimbali ya kimaisha. Usifikiri sana ni wachawi, walozi, wanga, vigagula na waganga wa kienyeji, wale ni watu smart elite wenye fani mbalimbali za kisomi. Kuna wafanyabiashara, wanasiasa, wanasheria, madaktari, walimu, wanadini na wengine wengi wenye ushawishi mkubwa katika jamii. Wana namna yao ya kupata wanachama wao wenye sifa na vigezo vya kuwa mwanajuiya. Si kila mtu anaweza kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo. Kwanza ni watu wenye akili na upeo wa hali ya juu kuhusu dunia. Hawa si wale matapeli wanaotangaza kuunganisha watu na freemason kwa kuweka matangazo yao milingotini na kwenye vipeperushi, freemason hawako hivyo. Ni jumuiya kubwa iliyopo duniani.
 
Tanzania hakuna hao freemason. Walio pata pesa za ghafla mnafikiria ni free mason ni either biashara ya unga au ufisadi wa daraja la juu kama bandarini au kwenye miradi mikubwa
 
Hawa jamaa enzi za siasa za ujamaa Nyerere hakutaifisha majengo yao licha kujua uwepo wao na hakuwa mwanachama wao. Waliomfuata walionekana wakipiga picha pamoja katika hafla zao. Kuna kitabu kiliandikwa na kiongozi wa freemason Tanzania kinaitwa Journey from Bukene, kuna mambo ya kujua kuhusu jumuiya hii.
 
Back
Top Bottom