Jengo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa - Dubai lapambwa kwa picha za Bendera ya Tanzania

Jengo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa - Dubai lapambwa kwa picha za Bendera ya Tanzania

Jengo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa pale Dubai muda huu limenakshiwa kwa Bendera ya Tanzania mwanzo mpaka mwisho lote. Dunia nzima sasa inatazama maajabu haya kwenye Jengo hilo refu zaidi Duniani huku Utalii wa Taifa letu ukizidi kutangazwa.

Yote hii ni matunda ya ziara ya siku 3 ya Rais Samia Suluhu Hassan Dubai na heshima inayopewa Taifa letu baada ya ziara hiyo iliyokuwa na mafanikio makubwa sana ya Kiuchumi na Uwekezaji.

Hiyo ni pamoja na mafanikio mengine makubwa ya ziara hiyo ambayo ni Kusainiwa kwa Hati 36 za Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta mbalimbali yenye thamani ya Shilingi Trilioni 17.1 ambayo itatoa ajira 204,575 kwa Watanzania. Ziara ya Rais Samia Dubai imetulipa kwelikweli. Kazi Iendelee.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com

View attachment 2134743
View attachment 2134474

View attachment 2134476

View attachment 2134477
Machawa mnakuja na mbwembwe humu na kibibi chenu cha kiarabu.. tukiwauliza gharama zipoje ili tujadili, mnatugeuzia makalio.. pumbavu kabisa kabisa..!
 
Tatizo la kuamka na hangover hebu kunywa supu kwanza, hizo billions alizopata mie Sina ishu nazo na siongelei hapa kabisa hizo ni mambo ya miradi mingine ambayo walishamaliza maongezi na walikuwa kwenye stage ya kusaini Ila Rais huwa anatumia lugha fulani nyepesi kwamba "kuna vijifedha amepata'. Actually sijaongelea kabisa issue hizo Zina mihemko watu Wana njaa wakisikia anatana hela wao tayari wanaweka na zao kwamba ameiba basi asitaje kabisa.

Anyway nimeongelea masuala ya kujitangaza nchi kwa kuvutia uwekezaji zaidi na utalii na madini nk. Nilichoandika ni kutokana na mleta mada alivyowasilisha na pia nilikuwa najibu kwa mtu aliyesema wametumia milioni 157 kuweka hilo tangazo. Labda uanze upya kusoma ndipo usome taratibu hii response yangu then uje Tena.

Nakuona unalohangaika kuhusu trilioni 17 hizo sio hard cash ni uwekezaji kulingana na makubaliano kadhaa waliyosaini mawaziri alioenda nao. Na hizo pesa sio amerudi nazo kwenye pochi mzee. Subirini viwanda vije watu waajiriwe hii sio vile viwanda elfu kumi kila mkoa mlidanganywa sana na ajira mkakosa maana mnaaminishwa kwenye mambo ya zinduna how possible can it be uwe na viwanda sijui elfu arobaini kila mkoa na huyu philipo mpango ndio alikuwa bingwa wa cooked data.

Tulia usome uelewe.
Na bado unajitambua kuwa 'GT' hata huwezi kuelewa maana ya nilichoandika?

Wewe ni mpiga zumari tu, ndiyo maana nikakuwekea ulaghai huo wanaoutumia wakidhani watu hawajui kitu. Sasa watu kama wewe, bado unafikiri hizo bilioni 17, eti ni uwekezaji? Uwekezaji upi, upo wapi?
 
Tambueni wakati jengo Hilo linajengwa mkurugenzi wake Dubai alikua mtu kutoka Tanzania tuseme alirudishwa kuja kua mkurugenzi NHC Tanzania ,sijui shirika lanyumba Dubai linaitwaje lakini ndivo ilivo
 
Nilikua naangalia Station moja ya nje muda huu [emoji1256] UAE na Tanzania wana mpango wa makusudi kuwaondoa wamasai ngorongoro ili kubinafsisha hiyo hifadhi. Tuendelee kuomba hali siyo nzuri huko mbeleni.
Kweli hali sio nzuri na bandari ndio inaenda kiutaniutani
 
likiwaka kwa picha ya jemedari magufuli juu yake nyerere itapendeza sana
 
Back
Top Bottom