Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 581
Ni nani huyo Jenista Joakim Mhagama?
Mbunge wa Peramiho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)?
Je, ni yule yule aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu katika kipindi cha mwaka 2000-2005?
Akiwa karibu sana na viongozi wa serikali iliyopita hususan Frederick Sumaye na wenzake?
Nani anamjua vizuri huyu? Hususan katika sherehe nyingi za pale Dodoma? Nani anamjua vizuri huyu ambaye juzi alionekana kama mtetezi wa walimu wenzake wa zamani? Kwanini hasa amemsaliti mwanamke mwenzetu Hawa Ghasia?
Kuna siri gani? Waziri huwa hafanyi kazi mikoani na alipompa orodha ya walimu wenye matatizo, alijibiwa, "nimepokea siwezi kuwa na majibu hapa, ngoja niagize huko mikoani wanipe maelezo nitakupatia, sasa subiri baada ya kumaliza bajeti nitakuwa na majibu" yeye akasema, "sitasubiri, leo leo nitakulipua".... sasa alikuwa na haraka gani?
Je, lengo ni kulipua, ama kupata ufumbuzi wa tatizo? Je, huo ndio utaratibu wa zimamoto? kama yeye alikaa na hayo majina kwa miezi mitatu bila kupata majibu, imekuaje amtake mwenzake awe na majibu ya vijiji vya Songea papo kwa papo?
Kwa maoni yangu, huu sasa ni mchezo wa kukata tamaa na kutafuta wachawi kwa matatizo ya wabunge wetu ambao wameshindwa kazi majimboni. Baadhi watatumia kiini macho cha kufuatwa fuatwa na maadui zao, wako watakaosingizia wanaotaka ubunge 'wao' lakini je, kuna mwenye HAKI MILKI YA UBUNGE? Kama wameshindwa waache wenye uwezo waingie jimboni na kama mtu ulishindwa kwa miaka minne kufanya kazi jimboni, huwezi kupiga kelele bungeni kipindi kilichobaki ukafanikiwa. Waende majimboni kufanya kazi na wananchi na si kupiga kelele