PreGE2025 Jerry Muro aitisha press kumjibu Gwajima kuhusu utekaji

PreGE2025 Jerry Muro aitisha press kumjibu Gwajima kuhusu utekaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
753
Reaction score
1,699
Kwahiyo hapa huyu Jerry anamjibu Gwajima kama nani wakati wakuu wake wameufyata? Wao si ndio walikuwa waje kujibu na kutoa ufafanuzi kama wanachukua ushauri wake ama lah?

Ndio anatafuta teuzi kwa nguvu?

"Luhaga Mpina akinyimwa nafasi ya kuongea bungeni huchangia kwa maandishi, atachangia kwa maandishi na akitoka ataongea vyombo vya habari kile ambacho amechangia kwa maandishi, kwanini hata hukuchangia kwenye maandishi baba yangu haya mawazo yako?"

"Na unajua kabisa kwa mujibu wa katiba yetu, hili haliwezekani kwa sasa. Unajua kwa Katiba tuliyonayo ushauri wako hauwezekani kwa sababu Katiba ndio tunaiangalia kwa sasa. Kwanini unaleta ugumu katika mambo ambayo sio?"

"Umesema kwamba hawa vijana wetu wa majeshi hawa ambao wanafanya kazi nzuri waongezewe mishahara. Juzi tu Rais ametoka kuongeza mishahara ya kima cha chini ya watumishi wa umma. Nilidhani ungeanza kuwa kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuongeza mishahara"

"Kitu kingine ambacho hujui ni kama unamchonganisha Rais na vijana wa idara na wanajeshi pasipo kujua ni katika kipindi cha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, maslahi ya wapiganaji wetu, wanajeshi wetu yameongezeka kwa asilimia 18.4 katika kupatiwa vifaa, nyumba bora"

Pia soma Pre GE2025 - Askofu Gwajima: Wakuu wa Vyombo vya Usalama wasiondolewe kwenye nafasi zao kwa mapenzi ya mwanasiasa aliyewaweka

"Ndugu yangu Gwajima, kwanza nataka tuungane mimi na wewe, pamoja na viongozi wote wa Serikali na wananchi, tukiongozwa na Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kulaani vitendo vya utekaji, kulaani vitendo vya watu kupotea, kulaani vitendo vya watu kuuawa. Kama ulivyosema, na mimi naungana na wewe katika kuendelea kumuuomba Mungu atusaidie, damu za Watanzania wasio na hatia zisiendelee kumwagika."

"Vitendo vya utekaji na kupigwa risasi nataka nikurudishe nyuma kidogo, vitendo hivi vilikuwepo au labda kwa sababu tulikuwa hatuna maendeleo ya sayansi na teknolojia.

"Tulikuwa na viongozi wa serikali wakina Oscar kambona, Edwin Mtei, Abdulrahmin Babu na ambavyo walikimbia kwenda ughaibuni baada ya kuhitalifiana na Nyerere. Natakanikuulize hivi ukisoma sana hivi vitabu hakuna sehemu inakwambia wale ambao hawakuweza kukimbia, wale ambao hawakuweza kukimbia na kupanda, hivi walikutana na kitu gani hasa?"
 
Kwahiyo hapa huyu Jerry anamjibu Gwajima kama nani wakati wakuu wake wameufyata? Wao si ndio walikuwa waje kujibu na kutoa ufafanuzi kama wanachukua ushauri wake ama lah?

Ndio anatafuta teuzi kwa nguvu?

Wanachofanya ni kupora platform ya kujadili mabadiliko ya Sheria na Kanuni za uchaguzi ambayo ndiyo imeshika kasi nchini, wanataka waitumie kwa marumbano ya wao kwa wao, habari za 'No Reform No Election' zinakuwa zimezikwa rasmi.
 
Kwahiyo hapa huyu Jerry anamjibu Gwajima kama nani wakati wakuu wake wameufyata? Wao si ndio walikuwa waje kujibu na kutoa ufafanuzi kama wanachukua ushauri wake ama lah?

Ndio anatafuta teuzi kwa nguvu?

Kaona game za SIMBA zimeisha hajapata attention yoyote naona kaibukia kwa Gwajima. Enzi zako Jeery zimepita wewe njoo tuendelee na ile project yetu ya kuandika uliyoniachia mwenyewe
 
Hoja alizotoa gwajima ni nzito na kama tunavyojua ccm na serikali yao hawana uwezo wa kujibu hoja hata siku moja, kwa hiyo tulitegemea lazima hawa wapumbavu walio jazana mle mboga mboga waatanza kubwatuka huku na kule, alianza msukuma amefata huyo bwabwa bado na wengine watakuja

Lakini wajipange kisawa sawa maana gwajima akiliamsha dude watakosa pa kujificha hana tofauti na manara yule
 
Mzee wa vipistol 🔫 kaja leo na MiC🎤 🎙️ na Camera 📸
 
Back
Top Bottom