Kwahiyo hapa huyu Jerry anamjibu Gwajima kama nani wakati wakuu wake wameufyata? Wao si ndio walikuwa waje kujibu na kutoa ufafanuzi kama wanachukua ushauri wake ama lah?
Ndio anatafuta teuzi kwa nguvu?
"Luhaga Mpina akinyimwa nafasi ya kuongea bungeni huchangia kwa maandishi, atachangia kwa maandishi na akitoka ataongea vyombo vya habari kile ambacho amechangia kwa maandishi, kwanini hata hukuchangia kwenye maandishi baba yangu haya mawazo yako?"
"Na unajua kabisa kwa mujibu wa katiba yetu, hili haliwezekani kwa sasa. Unajua kwa Katiba tuliyonayo ushauri wako hauwezekani kwa sababu Katiba ndio tunaiangalia kwa sasa. Kwanini unaleta ugumu katika mambo ambayo sio?"
"Umesema kwamba hawa vijana wetu wa majeshi hawa ambao wanafanya kazi nzuri waongezewe mishahara. Juzi tu Rais ametoka kuongeza mishahara ya kima cha chini ya watumishi wa umma. Nilidhani ungeanza kuwa kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuongeza mishahara"