Jerry Silaa anatuonesha jinsi mfumo wa utoaji haki ulivyooza...

Jerry Silaa anatuonesha jinsi mfumo wa utoaji haki ulivyooza...

Kila maamuzi anayotoa Waziri wa Ardhi na Makazi na maendeleo ya Nyumba, Jerry Silaa ujumbe anaoutoa ni kwamba mifumo ya utoaji haki kwenye Taifa letu imeoza.

Mabaraza ya Ardhi mpaka mahakama zetu zinatoa maamuzi yake kuhusu migogoro ya Ardhi kwa kuegemea zaidi mambo ya kiufundi (technicalities) kuliko mantiki.

Maamuzi mengi ambayo Silaa anayatolea maamuzi yaliamuliwa kwa kushangaza sana kwenye vyombo vya kutolea haki.

Ndugu zetu "wasomi" wanasheria tasnia yenu imejaa uozo Sana kwa kuendekeza rushwa.

Kuna kesi Moja eti mlalamikiwa ndiyo anaamua kuondoa shitaka Baraza la Ardhi la Wilaya bila ya kuomba kubeba jukumu ( Judgement on Admission) la maamuzi ya kuomba kuondolewa kwa kesi barazani.

Cc:
Bush Dokta
Mimi nikiwaona wale wa haki jinai na nikikumbuka yale mambo ya sabaya mwanzo mwisho napata kichefuchefu
 
Siyo tu mfumo wa utoaji haki. Ni serikali nzima imeoza. Nenda kwa wastaafu wanaodai mafao uone. Ni kila sehemu. Cha kushangaza hakuna anayeonekana kujali na yeye mwenyewe ni kama anafanya kazi ya kukausha bahari kwa kuchota maji kwa ndoo. Hebu mwambieni ajaribu kuwashauri CCM wakubali kubadilisha mfumo na kuwe na uchaguzi huru ili tupate viongozi wanaojibika.
Waambie ukweli Hawa mapimbi! Nchi hii ni ya hovyo sana na viongozi wengi ni wahuni na majambazi makubwa sana. Kama hapo Kwa wastaafu umegusa maumivu ya wastaafu wengi sana wanahangaika miaka na miaka hawapati haki Yao. Ccm ni mafisadi makubwa sana!
 
Yap.

Maamuzi anayoyatoa yeye hutofautiana na maamuzi ya awali.

Ili kutengua maamuzi ya kisheria ni lazima yafuate mkondo wa kisheria ambapo kwenye mkondo huo Waziri wa Ardhi hatambuliki.

Lakini Kwa kutumia mkondo wa Sheria ya Ardhi chini ya mtizamo kuwa Ardhi yote ya Tanganyika Iko chini ya Rais, na Waziri wa Ardhi ni mwakilishi wake, Waziri wa Ardhi anayo mamlaka ya kuamua masuala yote yahusuyo Ardhi aonavyo yeye.
Sasa tupe mfano tafadhali.
Maana mengi anayoamua ni yale ambayo hakuna hukumu na yenye hukumu yeye hutoa maoni yake.
Mara kadhaa ameema anaamini mahakama za Tanzania zinatoa hukumu kihalai kwa asilimia kubwa sana.
 
Nimeandika hapo juu kiwanja ama namba Moja au namba nne Ngamiani Tanga.
 
Kila maamuzi anayotoa Waziri wa Ardhi na Makazi na maendeleo ya Nyumba, Jerry Silaa ujumbe anaoutoa ni kwamba mifumo ya utoaji haki kwenye Taifa letu imeoza.

Mabaraza ya Ardhi mpaka mahakama zetu zinatoa maamuzi yake kuhusu migogoro ya Ardhi kwa kuegemea zaidi mambo ya kiufundi (technicalities) kuliko mantiki.

Maamuzi mengi ambayo Silaa anayatolea maamuzi yaliamuliwa kwa kushangaza sana kwenye vyombo vya kutolea haki.

Ndugu zetu "wasomi" wanasheria tasnia yenu imejaa uozo Sana kwa kuendekeza rushwa.

Kuna kesi Moja eti mlalamikiwa ndiyo anaamua kuondoa shitaka Baraza la Ardhi la Wilaya bila ya kuomba kubeba jukumu ( Judgement on Admission) la maamuzi ya kuomba kuondolewa kwa kesi barazani.

Cc:
Bush Dokta
Wanasheria mnajua jinsi ya kupindisha sheria na kupoka haki za wenye haki kwa kupewa rushwa na watu wenye tamaa na mali za watu. Jerry Silaa ni mwanasheria na anajitihadi kuirudisha haki kwa wenyewe na kwa mamlaka aliyokasimiwa na raisi. Vyombo vya kutoa haki vipo na vinatenda kazi yake lakini kuna baadhi ya watu waliyokuwa si waaminifu na ndiyo wanatumiwa katika kuona kuwa vyombo vya sheria vimeoza. Tujaribu kutengeneza taasisi imara za kutoa haki.
 
Hii nchi isikie tu. Hakuna serikali inayonuka rushwa Kama hii ya mama Samiah. Kuna mtu katapeli watu kila kitu Kwa kutumia jina la Rais Mwinyi, Waziri Mkuu na Rais Samiah na hakuna anayemgusa maana kaiweka serikali mfukoni mwake.
 
Ukweli usemwe, Jerry Silaa anafanya kazi nzuri hasa ninapomuona anashughulika na watu wasioweza kupata msaada wa kisheria. Kazi anayofanya ni nzuri na apewe maua yake.

Pili, Jerry anaonyesha matundu makubwa ya dhulma katika ardhi. Waziri ameeleza mara nyingi kwamba Mahakama inatumika kama chaka. Huo ni ukweli na ukweli mtupu. Matapeli na wenye pesa hutumia mahakama kudhulumu haki

Jerry aliwahi kusema watu wakidhulumiwa '' wasiende mahakamani'' . Kauli hii ilimuingiza katika matatizo makubwa lakini alichosema ni ukweli. Ikiwa tuna Afisa ardhi Wilaya na mkoa halafu wanamshauri 'mhanga' eti aende kudai haki mahakamani , huo ni upuuzi wa hali ya juu sana. Kazi yao ni ipi? Anayejua viwanja na haki zake ni Afisa ardhi si mahakama. Kwa kujua uchafu wa mahakama maafisa Aardhi wanashauri watu waende huko kichakani.

Naunga mkono kauli ya Jerry kwamba kwenda mahakamani ni kuhamisha mchezo ili ukachezwe '' uwanja wa nyumbani'' a.k.a Mahakamani. Hakuna shaka Mahakama zinatumika vibaya sana katika kadhia hiyo.
Hakuna sababu ya mgogoro wa ardhi kuamuliwa na mahakama maafisa Ardhi wakiwa watazamaji! nonesense

Lakini pia Jerry ni mmoja wa wanaopinga Katiba mpya kupitia CCM.
Mfumo mzima wa kutoa haki umegubikwa na rushwa na unahitaji ''overhauli''., Jerry aungane nasi kudai katiba
 
Kila maamuzi anayotoa Waziri wa Ardhi na Makazi na maendeleo ya Nyumba, Jerry Silaa ujumbe anaoutoa ni kwamba mifumo ya utoaji haki kwenye Taifa letu imeoza.

Mabaraza ya Ardhi mpaka mahakama zetu zinatoa maamuzi yake kuhusu migogoro ya Ardhi kwa kuegemea zaidi mambo ya kiufundi (technicalities) kuliko mantiki.

Maamuzi mengi ambayo Silaa anayatolea maamuzi yaliamuliwa kwa kushangaza sana kwenye vyombo vya kutolea haki.

Ndugu zetu "wasomi" wanasheria tasnia yenu imejaa uozo Sana kwa kuendekeza rushwa.

Kuna kesi Moja eti mlalamikiwa ndiyo anaamua kuondoa shitaka Baraza la Ardhi la Wilaya bila ya kuomba kubeba jukumu ( Judgement on Admission) la maamuzi ya kuomba kuondolewa kwa kesi barazani.

Cc:
Bush Dokta
Bila Sharia hakuna haki duniani inayokuja kiulaini.
 
Hii nchi isikie tu. Hakuna serikali inayonuka rushwa Kama hii ya mama Samiah. Kuna mtu katapeli watu kila kitu Kwa kutumia jina la Rais Mwinyi, Waziri Mkuu na Rais Samiah na hakuna anayemgusa maana kaiweka serikali mfukoni mwake.
Unailinganisha na nchi pi?
 
Back
Top Bottom