Jerry Silaa anatuonesha jinsi mfumo wa utoaji haki ulivyooza...

Mimi nikiwaona wale wa haki jinai na nikikumbuka yale mambo ya sabaya mwanzo mwisho napata kichefuchefu
 
Waambie ukweli Hawa mapimbi! Nchi hii ni ya hovyo sana na viongozi wengi ni wahuni na majambazi makubwa sana. Kama hapo Kwa wastaafu umegusa maumivu ya wastaafu wengi sana wanahangaika miaka na miaka hawapati haki Yao. Ccm ni mafisadi makubwa sana!
 
Sasa tupe mfano tafadhali.
Maana mengi anayoamua ni yale ambayo hakuna hukumu na yenye hukumu yeye hutoa maoni yake.
Mara kadhaa ameema anaamini mahakama za Tanzania zinatoa hukumu kihalai kwa asilimia kubwa sana.
 
Sasa tupe mfano tafadhali.
Maana mengi anayoamua ni yale ambayo hakuna hukumu na yenye hukumu yeye hutoa maoni yake.
Mara kadhaa ameema anaamini mahakama za Tanzania zinatoa hukumu kihalai kwa asilimia kubwa sana.
Nimeandika hapo juu kiwanja ama namba Moja au namba nne Ngamiani Tanga.
 
Wanasheria mnajua jinsi ya kupindisha sheria na kupoka haki za wenye haki kwa kupewa rushwa na watu wenye tamaa na mali za watu. Jerry Silaa ni mwanasheria na anajitihadi kuirudisha haki kwa wenyewe na kwa mamlaka aliyokasimiwa na raisi. Vyombo vya kutoa haki vipo na vinatenda kazi yake lakini kuna baadhi ya watu waliyokuwa si waaminifu na ndiyo wanatumiwa katika kuona kuwa vyombo vya sheria vimeoza. Tujaribu kutengeneza taasisi imara za kutoa haki.
 
Hii nchi isikie tu. Hakuna serikali inayonuka rushwa Kama hii ya mama Samiah. Kuna mtu katapeli watu kila kitu Kwa kutumia jina la Rais Mwinyi, Waziri Mkuu na Rais Samiah na hakuna anayemgusa maana kaiweka serikali mfukoni mwake.
 
Ukweli usemwe, Jerry Silaa anafanya kazi nzuri hasa ninapomuona anashughulika na watu wasioweza kupata msaada wa kisheria. Kazi anayofanya ni nzuri na apewe maua yake.

Pili, Jerry anaonyesha matundu makubwa ya dhulma katika ardhi. Waziri ameeleza mara nyingi kwamba Mahakama inatumika kama chaka. Huo ni ukweli na ukweli mtupu. Matapeli na wenye pesa hutumia mahakama kudhulumu haki

Jerry aliwahi kusema watu wakidhulumiwa '' wasiende mahakamani'' . Kauli hii ilimuingiza katika matatizo makubwa lakini alichosema ni ukweli. Ikiwa tuna Afisa ardhi Wilaya na mkoa halafu wanamshauri 'mhanga' eti aende kudai haki mahakamani , huo ni upuuzi wa hali ya juu sana. Kazi yao ni ipi? Anayejua viwanja na haki zake ni Afisa ardhi si mahakama. Kwa kujua uchafu wa mahakama maafisa Aardhi wanashauri watu waende huko kichakani.

Naunga mkono kauli ya Jerry kwamba kwenda mahakamani ni kuhamisha mchezo ili ukachezwe '' uwanja wa nyumbani'' a.k.a Mahakamani. Hakuna shaka Mahakama zinatumika vibaya sana katika kadhia hiyo.
Hakuna sababu ya mgogoro wa ardhi kuamuliwa na mahakama maafisa Ardhi wakiwa watazamaji! nonesense

Lakini pia Jerry ni mmoja wa wanaopinga Katiba mpya kupitia CCM.
Mfumo mzima wa kutoa haki umegubikwa na rushwa na unahitaji ''overhauli''., Jerry aungane nasi kudai katiba
 
Bila Sharia hakuna haki duniani inayokuja kiulaini.
 
Hii nchi isikie tu. Hakuna serikali inayonuka rushwa Kama hii ya mama Samiah. Kuna mtu katapeli watu kila kitu Kwa kutumia jina la Rais Mwinyi, Waziri Mkuu na Rais Samiah na hakuna anayemgusa maana kaiweka serikali mfukoni mwake.
Unailinganisha na nchi pi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…