Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Umeenda Kihonda, umetaka wananchi waeleze kero zao za ardhi. Mwananchi anakueleza wewe unamuinterrupt kwa kejeli na dharau kuwa "Hutaki kuhutubiwa".
Huyo mwananchi pengine ana watoto, ana mke, ana ndugu na jamaa wanaoheshimiana naye- Wewe unamjibu kwa nyodo na kumuitia Polisi wamchuke. Hii maana yake nini?
Kwanza nataka nikueleze kuwa wewe huna Mamlaka juu ya wananchi, bali wananchi indirectly wana mamlaka juu yako.
Kama ni mahojiano ya kuwekana kitimoto basi ilibidi wananchi wakuweke wewe kitimoto badala ya wewe kuwaweka wao kitimoto. Lakini kama kwa dhati kabisa ulitaka kuwasikiliza basi ni juu yao kukueleza kwa jinsi wanavyojua wao, siyo wewe kuwavimbia wakueleze shida zao kwa namna unavyotaka wewe.
Natambua, na ninajua kuwa nia yako ni njema, na ninaunga mkono hilo Lakini hii tabia ya kuproject mamlaka na kuvimba mbele ya wananchi inaonyesha bado hujajua kuwa wewe unaserve hapo kama waziri indirect kwa sababu ya hisani yao
Hebu muombe radhi huyo mzee na uwe mvumilivu pale wananchi wanapoongea mambo yao. Kama huwezi kuwasikiliza na kuwapa time wananchi basi tafuta mbinu nyingine ya kufanya majukumu ya uwaziri, badala ya kubagaza watu, kutweza watu na kuwaitia polisi pale unapokereka namna wanavyowasikisha kero zao kwako!
Naweka video ya tukio hapa: