Jerry Silaa, kama ulivyotembea kwa miguu kipindi unatafuta kura, tembelea tena uone hali ya barabara ya Kitunda

Jerry Silaa, kama ulivyotembea kwa miguu kipindi unatafuta kura, tembelea tena uone hali ya barabara ya Kitunda

Ngurukia

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2023
Posts
4,407
Reaction score
16,942
Jerry Slaa, ulitembea kwa miguu kutoka Banana mpaka Kitunda kuomba kura. Leo hii baada ya kupata hizo kura hujaonekana tena.

Ni fedheha kubwa kwa eneo ambalo ni mkabala kabisa na Airport kuwa na barabara ambazo zinatia aibu.
Kuna mahandaki ambayo mtu mwenye gari ndogo anafirikiria mara mbili kupita achalia mbali watembea kwa miguu.

Haya matatizo yamekuwa endelevu lakini kila mwaka mnajifanya kushangaa mkiona hali ilivyo.

Jerry Slaa, unapiga sana misele sasa hivi kujifanya unashughulukia mambo ya wizara, hebu njoo upige misele na jimboni kwako basi uone hali ilivyo.
 
Tumepata taarifa tutalifanyia kazi. Nitatembea Tena mwakani na 2025. Nina majukumu ya kitaifa na kichama Kwanza. Tuvumiliane Mimi sio wa Kwanza.
 
Tatizo sio Wanasiasa, tatizo ni sisi wenye nchi.
 
Si mnapewa hadi wali na bahasha kipindi kampeni?

Viongozi wetu wapo bize na mambo mengine, huko jimboni pambaneni.
 
yaani hyo barabara, kama kuna mtu aliambiwa ukijenga tu unakufa.
 
Back
Top Bottom