Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Akichangia bajeti ya wizara ya ujenzi na uchukuzi leo bungeni, Mbunge wa Ukonga amesema licha ya Rais Samia kuonya mkandarasi mmoja kupewa tenda nyingi kwa wakati mmoja, Wizara husika iliipa kandarasi Kampuni ya kichina ya Sino hydro, ujenzi wa awamu ya tatu ya mradi wa mwendokasi Mbagala -Magomeni licha ya kampuni hiyo kuwa na tenda 5 kwa wakati huo.
Akinukuu hotuba ya Rais Samia ya Desemba mwaka jana akizindua awamu ya pili ya mradi wa BRT chini ya Kampuni ya Sino Hydro amesema “kama viongozi wasingesimama na kusema hapa ni pabovu mkandarasi yule angeendelea kutujengea ubovu ule ule, kwa hiyo niombe sana viongozi wa halmashauri mlioko huko muwe macho, lakini wakati mwingine nasi Serikali labda tunatatizo, unaweza kukuta mkandarasi mmoja ana kazi nne au tano kwa wakati mmoja kwa hiyo mnaotoa tenda hizo muangalie nani yupo tayari kujenga kwa wakati huo”.
Ameendelea “mheshimiwa spika Sino hydro amepewa mradi wa BRT awamu ya tatu kuanzia Gongo la mboto mpaka Kariakoo, mkandarasi huyu ambaye kilomita 2.5 zimetinduka na kuleta ufa huko mbagala, asielipa wafanyakazi na wazabuni, ameenda kuongezewa kazi nyingine”.