Jerry Silaa: Kampuni ya Sino Hydro walipewa tenda nyingine ya BRT licha ya Kuboronga mradi wa awali

Pamoja na yote serikali ilitakiwa isimpe maana keshaonesha hawezi kwenye mradi wa maji....
Serikali ingeweka kipengele cha kuvunja mikataba bila wao kuathirika.

Strabag alijitahidi sana
Pengine mkataba umeifunga serikal ndio maana hwezi kuvunja wachina kwenye mikataba ni wajanja sana msipokuwa makini Na strabag alifanya kazi kubwa sio alijitahid mwendokasi leo ya kimara inakaribia miaka 7 still ipo vile vle hao upande wa pili haijaanza kutumika ishaanza kuonyesha nyufa kuna mahali tunakwama
 

One of the Best Comments in jF history..

Mfano hai...

SGR Railway inajengwa kwa section zaidi ya nne(4).. ambazo ni:-

1. Dar to Morogoro
2. Morogoro to Makutupora
3. Makutupora to Isaka
4. Isaka to Mwanza Port
5. Isaka to Uvinza
6. Isaka to Rwanda

Hizi sections zinajengwa moja baada ya nyingine. Wakati section ya Dar to Morogoro imeshakamilika unajiuliza je, hao wataalamu wetu waliokuwepo kwenye ujenzi wa section 1 hawajajifunza technology ya ujenzi huo kiasi cha kutengeneza kampuni ya ujenzi wa SGR itakayomalizia section zote zilizobakia?
 
Upo sahihi.
 
Hiyo kazi afisa mkuu wa tenda alishaenda kuzimu, na legacy inasema marehemu hasemwi!
Basi kazi iendelee!
 
Wataalam hawawezi post bakshish kwenye account za uswizi, halafu wataongea, watasambaza umbeya.
Wataalam wabakie Tu na bahasha ndogo ndogo huko ofisini.
 
Nchi inajengwa kwa tabu sana hii, nikipita hapa BP darajani hapa natamani foleni itembee first ilinisi geuze shingo kuwaona wabongo wenzangu wanavyo fanya kazi kama watumwa,nasijui wanawalipa sh ngapi hawa wafanyakaziwao.

Yani wamechoka alafu unakuta wana funga still structures za scaffolding na form works nyingine wakiwa kwenye high risk.
Hawana body harness, na safety gears nyingine ni majanga matupu sijui OSHA kama wanatembelea maeneo ya ujenzi kukagua hata PPE nk.

Wachina hawako smart kabisa.
 
Watu wa serikali wanapenda Sana wachina kwa sababu wanawahinga mapesa mengi ya Rushwa.
 
Nyote mnaonekana hampo kwenye construction industry na hamna uelewa wa baadha ya mambo ya construction hasa miradi mikubwa.
Naishia hapa.
 
Mpaka sasa nina wasiwasi sana na daraja la Nyerere Kigamboni; Kuna siku litaanguka. Huko China, wamejenga barabara na madaraja mengi sana lakini vile vile mengi yamekuwa yanaanguka mara kwa mara wala hawajaweza kubadili mbinu za ujenzi.




 
Ile fly over ya Temeke nikiangalia kama vile wanajenga kihenge cha kutunzia nafaka nina mashaka vitakaa siku mtakuta vishachuchumaa. CCM sijui kumetupiga juju la wapi
 
Aliyejenga BRT ya kimara ni Straberg wajerumani hao, mradi huo wa BRT ya kimara ulikuwa unafadhiliwa na worldbank, huu wa sasa naona unafadhiliwa na serikali ndio maana wanapewa tenda wachina, straberg ni mjerumani hawawezi kumlipa.
Straburg ni kampuni ya Austria sio Germany
 
Kabisa mkuu hapo nimekusoma Alafu kulikuwa na huyu China Civil Engineering Kwenye mwendokas ya kimara Hivi alikuwa anahusika na nini haswa!?
Alikuwa anafanya associated works pale ubungo flyover ambayo ilijumuisha kubomoa ubungo terminal na kuijenga upya
 
Tenda kubwa nchini ndio pato kuu la pesa CCM. CCM ndio shabiki mkuu wa utawala usio fuata sheria.
 
Nyote mnaonekana hampo kwenye construction industry na hamna uelewa wa baadha ya mambo ya construction hasa miradi mikubwa.
Naishia hapa.

Ni kwa sababu ya watu kama wewe ndio maana nchi za Africa haziendelei..

Niishie hapo
 
Wapigaji ni CCM na 'wapendwa' wao!
Wapanga deal ni CCM hapo Hazina!
Wanufaika ni ccm na "wapendwa" wao
Wanaoumia ni wale wanaodanganywa kila kukicha kuwa 'serikali yao ni sikivu'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…