Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Naibu Waziri Mkuu wa Majaliwa Kasim
Kama Mrema alivyo ukwaa wakati Rais akiwa Mwinyi

Marekibishi ruksa
Nafikiri wewe unamzungumzia mhe Doto Biteko na sio Vicent Bashungwa.

Bashungwa hajawahi kuwa naibu waziri mkuu, ila Biteko amewahi na ndio naibu waziri mkuu wa Kassim Majaliwa Majaliwa kwa sasa.
 
Na kwanini raisi akubali ushauri wa hovyo kutoka kwa watu wa hovyo?
 
Kumbuka ni mwanasheria hiyo nayo ukichangany na uthubutu alikuwa naenda vizuei sana
 
Acha uwongo,,migogoro ya ardhi ipo miji miji mikubwa siyi vijijini amabpo ardhi haina thamani. We chiembe mjinga sana sbb viongozi wenginna majizi wengi wamejegemeza kwenye CCM sasa Silaa anaonaekna mbaya sbb kawapelekea moto hata wanaccm wenyewe.Mungu amubariki sana
ikubw
 
Huwa unakesha humu JF halafu hujui kwamba nchi ni mifumo! Watu tumesema hapa Jerry hatengenezi mifumo, anafanya show binafsi, kisha anapata milungula. Sasa Wizara imebaki kama ilivyo, hakuna substantial system aliyotengeneza
Hivi huoni land clinic kama ni mfumo? Waliopita miaka yote wameweka mfumo Gani.Shida siyo mifumo bali utashi wa watu kufanya kazi kuhakikisha mifumo inatendewa haki
 
Sasa wewe mbuzi, migogoro ya hifadhi za wanayama na mapori na wananchi iko mijini? Vijiji na vijiji, wilaya na wilaya, taasisi na wananchi, amepeleka moto wa konyo
 
Kumbuka ni mwanasheria hiyo nayo ukichangany na uthubutu alikuwa naenda vizuei sana
yule sio mwanasheria, hana uzoefu wowote wa mahakamani, mwanasheria ukisoma degree bila practice ni sawa na law graduate asiye na meno kabisa. tuambie, alishawahi kusimamia kesi ipi, ya nani, na wapi.
 
Hivi huoni land clinic kama ni mfumo? Waliopita miaka yote wameweka mfumo Gani.Shida siyo mifumo bali utashi wa watu kufanya kazi kuhakikisha mifumo inatendewa haki
Usitumie kichwa kubebea kamasi, land clinic sio mfumo, mifumo yote imeundiwa sheria
 
jerry ni mtovu wa nidhamu na mlevi wa madaraka, na si ukute ardhi ameondolewa kutokana na namna alivyomdhalilisha yule mwenyekiti wa kijiji morogoro. kana kiburi hadi balaa.wakipata madalaka huwa wanaamini wao hakuna kama wao.
 
Maamuzi yake mara zote yamekua yakiingilia muhimili wa mahakama...
 
Na kwanini raisi akubali ushauri wa hovyo kutoka kwa watu wa hovyo?
Ni kama vile anawaamini sana washauri wake hata kama wanampotosha. Sasa tusubiri kuona wale matapeli aliowanyang'anya ardhi za wizi wakizirudisha tena ardhi hizo katika mikono yao.
 
Amiin
 
Hivi huoni land clinic kama ni mfumo? Waliopita miaka yote wameweka mfumo Gani.Shida siyo mifumo bali utashi wa watu kufanya kazi kuhakikisha mifumo inatendewa haki
Achana nae tapeli wa ardhi huyo. Sisi tutapambana hadi kuhakikisha Silaa anarudishwa ardhi tu.
 
Maamuzi yake mara zote yamekua yakiingilia muhimili wa mahakama...
Kuna kesi ambazo zipo mahakamani kwa zaidi ya miaka 20 bila kutolewa maamuzi. Sasa kama mahakamani hawatafuti mwanya wa kupewa rushwa na matapeli ili wapindue haki ni nini?

Huyo mama pichani alikuwa katibu mkuu wakati wa serikali ya Nyerere. Alitapeliwa kiwanja toka enzi za Nyerere mpaka leo Samia. Ashafungua kesi mahakamani toka enzi za Mkapa, kaja Kikwete, kaja Magufuli na mpaka sasa Samia mahakama ilikuwa bado haijampa haki yake.

Silaa alivyoingilia kati mama kapata haki yake chini ya week moja tu. Sasa kama wewe ni mtoto au ndugu wa huyo mama bado utaamini tena mahakama?

Mambo mengine tusimnyime mtu haki yake kisa haumpendi au mtu unaemkubali hampendi basi na wewe unakimbilia kumchukua hata kama hana tatizo na wewe. Silaa amefanya mambo makubwa kwa muda mfupi kuliko waziri yoyote wa ardhi aliepita toka Nyerere mpaka Samia.
 

Attachments

  • Screenshot_20240726-154643.jpg
    297.1 KB · Views: 3

Attachments

  • Screenshot_20240726-154400.jpg
    268.9 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…