Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Ukiona hivyo mkono mrefu wa matapeli umemfikia raisi
 
Wizara ya Ardhi ni miongoni mwa Wizara ngumu sana maana matajiri wengi na wenye nafasi zao walishakita mizizi kuhakikisha kila ajaye kwenye Wizara hiyo haharibu mifumo yao.
Kwahiyo akitokea Waziri asiyewasikiliza ni rahisi Washauri wa Mamlaka za uteuzi kushauri Waziri huyo aondolewe kwenye Wizara hiyo.
 
Sasa kama amegusa maeneo ya vigogo waliomuweka?
 
Aliyemuweka ndiye aliyemtoa.sababu zakumuweka na kumuondoa anazo yeye na hatuna sababu yakuzijua.Sisi kama wananchi tunachotakiwa kukipambania ni tupate nchi yenye mifumo yakiuendeshaji ambayo itajiendesha ili mtu yoyote atakayehudumu kwenye nafasi yoyote awe na uwezo wakuendelea alipoishia aliyepita.Hakuna mtu muhimu zaidi kwenye ofisi ya umma watu wanakuja nakupita.
 
Kwakweli watu wengi watakuwa wamesikitishwa Jerry kutolewa ardhi.

Hata sijui kwanini huyo mama kamtoa hapo wakati alikuwa anafanya vizuri kwa mtazamo wa raia wa wakawaida.
Imagine mtu mwenye uthubutu, na uwezo wa kuwahenyesha matapeli wa ardhi kama Silaa unaenda kumtupa kwenye wizara ya hovyo ya habari ambayo ingefaa kupewa hata Mwana FA ili yeye Silaa abaki pale pale ardhi.

Alichofanya mama kimewaumiza na kuwasikitisha wengi.
 
Inasikitisha sana.
 

..Jerry Silaa kashindwa.

..William Lukuvi kashindwa.

..Ccm imeshindwa.
 
Hivi kunasababu yoyote ile iliyotolewa kwa kuhamishwa W/Ardhi kwa aliyekuwa Waziri J Slaa?!
Sababu itoke wapi mkuu. Wao wameona wamtoe eidha kwa kutofatilia kile alichokuwa anafanya, au kuna kundi la washauri wa raisi ambalo limeona kuwa masilahi yao yanakwenda kuguswa na Silaa kupitia wizara ya ardhi.

So wakaona bora wamshauri raisi amchomoe fasta fasta bila kosa wala maelezo.
 
Huyu Rais naye hata haeleweki aisee. Imagine, unamtoa mchapa kazi unamuweka jitu limejaza mahips tu.
Huyo aliemuweka atakuwa analala ofisini tu huku akisubiri watendaji wa chini wamletee taarifa.

Nakwambia toka jana matapeli wa ardhi wanafanya sherehe tu, kula na kunywa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…