Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Tukio baya lililomwondoa ni kuvamia wakazi wa CCT Morogoro na kuwatisha wananchi kuwaweka ndani bila kosa wakati wakielezea changamoto za ardhi yeye akadata kwa ujeuri wa madaraka akamfukuza mwanajeshi aliyekuwa akijieleza kwa dharau na hasira akishirikiana na dada mmoja mweupe hivi
Kumbe

🤔🤔🤔🤔
 
Ndivyo utendaji wa serikalini mwetu ulivyo. Utendaji unategemea mtu kwa sababu mfumo uko corrupted.
Unatakiwa ujitoe muhanga ili ufanikiwe ku deal na kuwaangamiza mafisadi pamoja na matapeli wakubwa katika nchi hii.
 
Inawezekana washauri wa Rais ni matapeli wa ardhi!
Hilo linawezekana. Maana haiwezekani viongozi wa timu wamtoe mchezaji mzuri wa timu yao katika mechi ya fainal, alaf waingize mchezaji mbovu huku wakijua kwamba kufanya hivyo kutahatarisha timu yao kukosa ushindi.

Hapo katika washauri wa raisi inaonekana kuna matapeli wa ardhi ambao wametumia nafasi zao kumshauri raisi amtoe Silaa wizarani.
 
Sidhani kama hiyo ndio sababu, maana kama ni hivyo basi tungesikia ametumbuliwa kabisa na sio kuhamishwa wizara.
Nakubaliana na wewe hii haiwezi kuwa sababu, unajuwa mtu ukiwa unamuhukumu utendaji wako lazima utizame mazuri na mapungufu yake upate kujuwa anafaa au hapana. Kama mazuri uzito wake mkubwa basi lazima abaki ila mimi nashida na uteuzi ni kama unatakiwa ufanye kazi vizuri lakini usiwe mzuri sana. Kama team ya mpira kocha kamtoa mchezaji ambaye kama washabiki tunadhani anacheza vizuri lakini kocha anadhani atoke sasa sababu inabidi kocha azitoe.
 
Niaje waungwana

Japo hakuna mtu mwenye dhamana ya kumpangia raisi kile anachoamua, lakini katika hili la kumtoa Silaa ardhi na kwenda kumtupa huko kwenye habari kwa kweli Rais wetu amefanya kosa la kiufundi sana.

Jerry alikuwa ashaanza kuwashughulikia vibaka na matapeli wa ardhi wote, yaani mmoja baada ya mwingine hadi kupelekea wengine kutupwa ndani. Sasa leo anapotolewa na kupelekwa wizara nyingine ni kuwapa nafasi wale wote waliokuwa washaanza kurudisha ardhi walizotapeli kabla kiama hakijawashukia waendelee nazo na pengine kuendelea kutapeli na zingine kwani aliekuwa anawapa tumbo joto kaondolewa na kupelekwa kungine.

Najiuliza, kwanini hiyo wizara ya habari asingepewa hata Mwana FA, ili Silaa aendelee kuwanyoosha wezi na vibaka wa ardhi za watu!

Anyway acha tuone mwisho wa game utakuaje. Lakini mama kama unatusikia na kufanikiwa kusoma uzi huu tafadhali TUNAOMBA (kwa herufi kubwa) UMRUDISHE JERRY SILAA W/ ARDHI 🙏🙏
Nani alikwambia kuwa anaangalia utendaji kazi wa mtu,? Ndio maana utaona wanaofanya kazi vizuri hawadumu kwenye wizara husika, ila wanavuluga wanadumu!!
 
Nani alikwambia kuwa anaangalia utendaji kazi wa mtu,? Ndio maana utaona wanaofanya kazi vizuri hawadumu kwenye wizara husika, ila wanavuluga wanadumu!!
Kwahiyo kina Nape na Makamba walikuwa wanafanya vizuri ndiomaana hawakudumu?
 
Kuna wakubwa aliwagusa kwenye operation yake.

Utendaji km wa JPM ulishaanza kuonekana ndan yake
Ya ni kweli inawezekana kuna mzito kafinywa gololi akaamua akimbilie kwa mama kuomba kijana ahamishwe haraka sana.
 
Nakubaliana na wewe hii haiwezi kuwa sababu, unajuwa mtu ukiwa unamuhukumu utendaji wako lazima utizame mazuri na mapungufu yake upate kujuwa anafaa au hapana. Kama mazuri uzito wake mkubwa basi lazima abaki ila mimi nashida na uteuzi ni kama unatakiwa ufanye kazi vizuri lakini usiwe mzuri sana. Kama team ya mpira kocha kamtoa mchezaji ambaye kama washabiki tunadhani anacheza vizuri lakini kocha anadhani atoke sasa sababu inabidi kocha azitoe.
Ni kweli mkuu.
 
NAKwahiyo kina Nape na Makamba walikuwa wanafanya vizuri ndiomaana hawakudumu?
Sijasema wote, ila wengi wao, mfano wizara ya ardhi, lukuvi, na hata yulo slaa walijitahidi kiasi fulani, kulinganisha na wengine, lakini hawakudumu, nenda, wizara ya mambo ya ndani, afya, na jenista wanatembelea ngekewa tu
 
Back
Top Bottom