Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Niaje waungwana

Japo hakuna mtu mwenye dhamana ya kumpangia raisi kile anachoamua, lakini katika hili la kumtoa Silaa ardhi na kwenda kumtupa huko kwenye habari kwa kweli Rais wetu amefanya kosa la kiufundi sana.

Jerry alikuwa ashaanza kuwashughulikia vibaka na matapeli wa ardhi wote, yaani mmoja baada ya mwingine hadi kupelekea wengine kutupwa ndani. Sasa leo anapotolewa na kupelekwa wizara nyingine ni kuwapa nafasi wale wote waliokuwa washaanza kurudisha ardhi walizotapeli kabla kiama hakijawashukia waendelee nazo na pengine kuendelea kutapeli na zingine kwani aliekuwa anawapa tumbo joto kaondolewa na kupelekwa kungine.

Najiuliza, kwanini hiyo wizara ya habari asingepewa hata Mwana FA, ili Silaa aendelee kuwanyoosha wezi na vibaka wa ardhi za watu!

Anyway acha tuone mwisho wa game utakuaje. Lakini mama kama unatusikia na kufanikiwa kusoma uzi huu tafadhali TUNAOMBA (kwa herufi kubwa) UMRUDISHE JERRY SILAA W/ ARDHI 🙏🙏
Mwenye dhamana na macho mengi amemuhamisha wizara, wewe unalilia angebaki pale pale. Siku zote ukitumia ubabe kusuluhisha migogoro lazima matatizo zaidi yataibuka. Acha mwingine achukue nafasi. Tz ina watu wengi wenye uwezo wa kuendesha hiyo wizara - " hakuna mteule"
 
Watanzania wengi wana uwezo mdogo sana wa kupima ufanisi wa kiongozi! Wanaridhika sana na kashkashi za kiongozi majukwaani/kwenye hadhara, na kuona kiongozi ni mchapakazi! Hizo mbwembwe!

Silaa ni kiongozi mbovu kabisa, msihadaike na mbwembwe zake. Hana weledi, hatii sheria, hana integrity wala consistency!

Amini, viongozi wa aina yake, walishafunga mkutano tu, hana muda tena na watu husika, anasepa kwenda kuibua lingine.

Akifuatwa wizarani, ndio wanashauriwa sasa watu waende mahakamani kama wana malalamiko.

Kiongozi sio kelele!
Hao uliokuwa unaona wanatii sheria walifanya kitu gani cha maana zaidi ya kile alichofanya Silaa. Silaa alikuta kuna watu walitapeliwa viwanja vyao tangu enzi za Nyerere. Mawaziri wote tangu enzi za Nyerere, Mwinyi mpaka Magufuli walipita bila kuwasaidia si kwa sheria wala kash kash kama ya Silaa.

Lakini Silaa alipoingia alianza kuzirudisha ardhi hizo kwa wamiliki halali na kuwafanya waliokuwa wanapanga kuendelea na utapeli kuogopa kuendelea na utapeli wao. Alaf leo unakuja kuleta habari za sheria. Hivi kuna kiongozi wa serikali au chama chochote nchi hii anaefata sheria zote kwa 100%?
 
Tukio baya lililomwondoa ni kuvamia wakazi wa CCT Morogoro na kuwatisha wananchi kuwaweka ndani bila kosa wakati wakielezea changamoto za ardhi yeye akadata kwa ujeuri wa madaraka akamfukuza mwanajeshi aliyekuwa akijieleza kwa dharau na hasira akishirikiana na dada mmoja mweupe hivi
Yule mzee aliyekuwa anajieleza kisha akamkatisha na kuita polisi wamkamate ni mwanajeshi?kwa hiyo unataka kusema yule mzee ndio ameenda kushitaki juu kwenye mfumo?
But anyway serikali yetu inafeli sana kuhamishahamisha watendaji hovyo yaani hawako strategic hata kidogo mtu ambaye alikuwa anafuatilia kwa ukaribu chanzo cha migogoro ya ardhi akawa anawashughulikia matapeli wanamtoa wanampeleka wizara nyingine ina maana kwenye Watanzania zaidi ya milioni 60 hakuna mtu wa kumuweka kwenye wizara ya habari na akafiti?
Ndio maana miaka yote tunarudi palepale.
Sasa hivi matapeli wa ardhi na nyumba wataanza kufanya sherehe
 
Niaje waungwana

Japo hakuna mtu mwenye dhamana ya kumpangia raisi kile anachoamua, lakini katika hili la kumtoa Silaa ardhi na kwenda kumtupa huko kwenye habari kwa kweli Rais wetu amefanya kosa la kiufundi sana.

Jerry alikuwa ashaanza kuwashughulikia vibaka na matapeli wa ardhi wote, yaani mmoja baada ya mwingine hadi kupelekea wengine kutupwa ndani. Sasa leo anapotolewa na kupelekwa wizara nyingine ni kuwapa nafasi wale wote waliokuwa washaanza kurudisha ardhi walizotapeli kabla kiama hakijawashukia waendelee nazo na pengine kuendelea kutapeli na zingine kwani aliekuwa anawapa tumbo joto kaondolewa na kupelekwa kungine.

Najiuliza, kwanini hiyo wizara ya habari asingepewa hata Mwana FA, ili Silaa aendelee kuwanyoosha wezi na vibaka wa ardhi za watu!

Anyway acha tuone mwisho wa game utakuaje. Lakini mama kama unatusikia na kufanikiwa kusoma uzi huu tafadhali TUNAOMBA (kwa herufi kubwa) UMRUDISHE JERRY SILAA W/ ARDHI 🙏🙏
Wakuu wizara ya aridh sio ya mchezo ,inatakiwa tuliza akili na sio mihemuko kama ambavyo uyu waziri alikua anafanya , kwanza nimeshangaa sana why Slaa endelea kuwa katika baraza la mawaziri , pale ni uchawa tu ila hakuna tija
 
Amekaa muda gani huko ardhi mpaka awe na mipango miji? Wacha hizo wewe! Kwa muda mfupi tu anashughulikia migogoro mingapi? Silaa apewe maua yake! Namtaka mama amrudishe haraka kwenye hiyo wizara awanyooshe! Ndejembi ndiye angepewa wizara hiyo ya Nape!
Mkuu ukichunguza kwa makini hizi comment za wanaompinga Silaa. Utagundua kwamba wanaompiga hapa wengi wao ndio wale wale waliokuwa wanatapeli watu viwanja na nyumba zao.

Hivyo wamekuja kupigilia msumari kuhakikisha kuwa Silaa harudishwi wizara ya ardhi kamwe.
 
Kutoka kuupiga mwingi mpaka mwingi kwa mwingi wanapigana...............niko pale lakini usiniite mbwa
 
Biden wamemzuia kugombea urais kutokana na matatizo ya akili ila cha ajabu hapa tz tunaje mgonjwa wa akili kuliko biden ila tuna msifu kuwa anaupiga mwingi ...ukitazama kwa makini teuzi zake utagundua tatizo kubwa sana kwenye kichwa cha huyo mjalaana ....NO LOGIC KWENYE KILA HATUA ANAYO CHUKUA NI UPUMBAVU MTUPU HADI UNASHINDWA KUMUELEWA LENGO LAKE NI NINI HASA AU ANA SHIDA GANI AU ANATAKA NINI ...mfano ni kama hapo kumuondoa waziri wa ardhi...inajenga taswila gani kwa taifa ? Kwamba anapendezwa na dhuruma ndiyo maana kamuondoa huyo waziri ?.....jibu ni moja tu nalo ni ili nililo lisema sana hapa
👇
LAANA... SAMIA UMELANIWA KULIKO WANAWAKE WOTE NA ABDUL MZAWA WA TUMBO LAKO KALAANIWA ....TOKEA SASA VIZAZI VYOTE VITAKUITA MLAANIWA.

Niwazi kuwa tunaongozwa na MJALAANA NDIYO MAANA YUPO KUWA FURAHISHA WAHUNI NA MAFISADI NA WAARABU NA MABEBERU DHIDI YA WANANCHI ...PITIA HATA MAMBO YA CHANJO FEKI ZA KORONA.
Namna alivyo tumia nguvu kuwa tii mabeberu.
Mkuu japokuwa wote tumekasirishwa na hili, lakin ingekuwa vizuri tukajadili kihekima na kwa kufuata sheria za jukwaa hili.

Tukianza ku attack watu na familia zao uzi utachafuka na kuonekana haufai kuendelea kuwepo hapa japo lengo la uzi halihusiani na hilo.
 
Niaje waungwana

Japo hakuna mtu mwenye dhamana ya kumpangia raisi kile anachoamua, lakini katika hili la kumtoa Silaa ardhi na kwenda kumtupa huko kwenye habari kwa kweli Rais wetu amefanya kosa la kiufundi sana.

Jerry alikuwa ashaanza kuwashughulikia vibaka na matapeli wa ardhi wote, yaani mmoja baada ya mwingine hadi kupelekea wengine kutupwa ndani. Sasa leo anapotolewa na kupelekwa wizara nyingine ni kuwapa nafasi wale wote waliokuwa washaanza kurudisha ardhi walizotapeli kabla kiama hakijawashukia waendelee nazo na pengine kuendelea kutapeli na zingine kwani aliekuwa anawapa tumbo joto kaondolewa na kupelekwa kungine.

Najiuliza, kwanini hiyo wizara ya habari asingepewa hata Mwana FA, ili Silaa aendelee kuwanyoosha wezi na vibaka wa ardhi za watu!

Anyway acha tuone mwisho wa game utakuaje. Lakini mama kama unatusikia na kufanikiwa kusoma uzi huu tafadhali TUNAOMBA (kwa herufi kubwa) UMRUDISHE JERRY SILAA W/ ARDHI 🙏🙏
Hii wizara ya habari ningepewa mimi tu naimudu...anyway wacha nibakie wizara hii hii ya vituko na mambo ya ghafla.
 
Matapeli na mafisadi wamepenyesha rushwa kwa CHURA mpk kamtoa!!
Ona vilio vitaanza upya vya matapeli ya udogo kwa watanganyika.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Kwa kweli wala si uongo.

Inasikitisha mno.
Unaweza kuzani Pengine labda hakuna seriousness ktk kuweka misingi ya haki kwenye maswala ya ardhi wakati hata Rais mstaafu JK aliwahi kusema kule ni shida kubwa,
Sasa kapatikana mwenye moyo wa utayari kujitoa mhanga kushughulikia anaondolewa?!
Maana yake ni nini?
Inaonekana washauri washashikishwa chao na matapeli, ili wamshauri mama amtoe Silaa ardhi na kumuweka kibonde waoambae atakuwa anashinda ofisini tu bila kutoka kwenda kutatua kero za wananchi.
 
Wwe lazima utakua tapeli la Aridhi ulie guswa na mkono wa chuma wa Jerry, sasa unatopoka kwa hasira,achaa utapeli wa Aridhi!!!
Kumbe na wewe umeshawashtukia mkuu. Mbona wako wengi humu, wamekuja kupigilia msumari hata kwa maneno ya uongo ili kuhakikisha kuwa Silaa harudishwi wizara ya ardhi.
 
Mpaka sasa sijaelewa kwann wamemtoa pale
Wakati aneshasaidia kesi kadhaa
Na alikuwa anaenda vzr.
Duh hii nchi sijui Huwa wanawaza nn jmn kabla hawajafanya mabadiriko.

Wanirudishe slaa
Hii nchi ndomaana mtu akidondokewa na teuzi anakula bata na kusinzia tu ofisini mpaka muhula wake au muda wake wa kuhudumu katika ofisi utapoisha wamtoe au atoke akafanye mambo mengine.

Sababu ukijifanya kuacha kula bata na kuingia mtaani kutatua kero za wananchi basi muda mchache tu utang'olewa katika nafasi yako.

Naona hata Bashungwa kakalia kuti kavu. Muda wowote anaweza kutolewa au kuhamishwa kisa anajituma.
 
Yule mzee aliyekuwa anajieleza kisha akamkatisha na kuita polisi wamkamate ni mwanajeshi?kwa hiyo unataka kusema yule mzee ndio ameenda kushitaki juu kwenye mfumo?
But anyway serikali yetu inafeli sana kuhamishahamisha watendaji hovyo yaani hawako strategic hata kidogo mtu ambaye alikuwa anafuatilia kwa ukaribu chanzo cha migogoro ya ardhi akawa anawashughulikia matapeli wanamtoa wanampeleka wizara nyingine ina maana kwenye Watanzania zaidi ya milioni 60 hakuna mtu wa kumuweka kwenye wizara ya habari na akafiti?
Ndio maana miaka yote tunarudi palepale.
Sasa hivi matapeli wa ardhi na nyumba wataanza kufanya sherehe
Sherehe mbona zimeshaanza kufanyika mkuu. Wewe hauoni hapa JF watu wanavyopongeza Jerry kuondolewa ardhi!
 
Yaani hii nchi ukitaka upendwe
Furahisha Maboss (CCM)
Au furahisha wananchi bila kuwabugudhi vigogo
Lasivyo utaondolewa au kuhamishwa wizara huku unaambiwa Umefanya kazi nzuri sana

Kama kutoa kauli tata kunamfanya mtu atoke kwenye nafasi
Nadhani hata Sir100 hatoshi hapo
 
Mkuu japokuwa wote tumekasirishwa na hili, lakin ingekuwa vizuri tukajadili kihekima na kwa kufuata sheria za jukwaa hili.

Tukianza ku attack watu na familia zao uzi utachafuka na kuonekana haufai kuendelea kuwepo hapa japo lengo la uzi halihusiani na hilo.
Ku attack kwa maana gani yaani kuteka watu na kuwa tesa na kuwaua fafanua na onyesha mifano ...upumbavu ni kipaji
 
Sijui kwanini wamemtoa 🐼
Huwa unakesha humu JF halafu hujui kwamba nchi ni mifumo! Watu tumesema hapa Jerry hatengenezi mifumo, anafanya show binafsi, kisha anapata milungula. Sasa Wizara imebaki kama ilivyo, hakuna substantial system aliyotengeneza
 
Haya 😂😂
 
Back
Top Bottom