Jerry Silaa kutolewa ardhi, tutarajie tena migogoro ya ardhi kuanza kuibuka upya na matapeli wa ardhi kuanza kutembea vifua mbele

Mwenye dhamana na macho mengi amemuhamisha wizara, wewe unalilia angebaki pale pale. Siku zote ukitumia ubabe kusuluhisha migogoro lazima matatizo zaidi yataibuka. Acha mwingine achukue nafasi. Tz ina watu wengi wenye uwezo wa kuendesha hiyo wizara - " hakuna mteule"
 
Hao uliokuwa unaona wanatii sheria walifanya kitu gani cha maana zaidi ya kile alichofanya Silaa. Silaa alikuta kuna watu walitapeliwa viwanja vyao tangu enzi za Nyerere. Mawaziri wote tangu enzi za Nyerere, Mwinyi mpaka Magufuli walipita bila kuwasaidia si kwa sheria wala kash kash kama ya Silaa.

Lakini Silaa alipoingia alianza kuzirudisha ardhi hizo kwa wamiliki halali na kuwafanya waliokuwa wanapanga kuendelea na utapeli kuogopa kuendelea na utapeli wao. Alaf leo unakuja kuleta habari za sheria. Hivi kuna kiongozi wa serikali au chama chochote nchi hii anaefata sheria zote kwa 100%?
 
Yule mzee aliyekuwa anajieleza kisha akamkatisha na kuita polisi wamkamate ni mwanajeshi?kwa hiyo unataka kusema yule mzee ndio ameenda kushitaki juu kwenye mfumo?
But anyway serikali yetu inafeli sana kuhamishahamisha watendaji hovyo yaani hawako strategic hata kidogo mtu ambaye alikuwa anafuatilia kwa ukaribu chanzo cha migogoro ya ardhi akawa anawashughulikia matapeli wanamtoa wanampeleka wizara nyingine ina maana kwenye Watanzania zaidi ya milioni 60 hakuna mtu wa kumuweka kwenye wizara ya habari na akafiti?
Ndio maana miaka yote tunarudi palepale.
Sasa hivi matapeli wa ardhi na nyumba wataanza kufanya sherehe
 
Wakuu wizara ya aridh sio ya mchezo ,inatakiwa tuliza akili na sio mihemuko kama ambavyo uyu waziri alikua anafanya , kwanza nimeshangaa sana why Slaa endelea kuwa katika baraza la mawaziri , pale ni uchawa tu ila hakuna tija
 
Mkuu ukichunguza kwa makini hizi comment za wanaompinga Silaa. Utagundua kwamba wanaompiga hapa wengi wao ndio wale wale waliokuwa wanatapeli watu viwanja na nyumba zao.

Hivyo wamekuja kupigilia msumari kuhakikisha kuwa Silaa harudishwi wizara ya ardhi kamwe.
 
Kutoka kuupiga mwingi mpaka mwingi kwa mwingi wanapigana...............niko pale lakini usiniite mbwa
 
Mkuu japokuwa wote tumekasirishwa na hili, lakin ingekuwa vizuri tukajadili kihekima na kwa kufuata sheria za jukwaa hili.

Tukianza ku attack watu na familia zao uzi utachafuka na kuonekana haufai kuendelea kuwepo hapa japo lengo la uzi halihusiani na hilo.
 
Hii wizara ya habari ningepewa mimi tu naimudu...anyway wacha nibakie wizara hii hii ya vituko na mambo ya ghafla.
 
Matapeli na mafisadi wamepenyesha rushwa kwa CHURA mpk kamtoa!!
Ona vilio vitaanza upya vya matapeli ya udogo kwa watanganyika.






KAZI ni kipimo cha UTU
 
Inaonekana washauri washashikishwa chao na matapeli, ili wamshauri mama amtoe Silaa ardhi na kumuweka kibonde waoambae atakuwa anashinda ofisini tu bila kutoka kwenda kutatua kero za wananchi.
 
Wwe lazima utakua tapeli la Aridhi ulie guswa na mkono wa chuma wa Jerry, sasa unatopoka kwa hasira,achaa utapeli wa Aridhi!!!
Kumbe na wewe umeshawashtukia mkuu. Mbona wako wengi humu, wamekuja kupigilia msumari hata kwa maneno ya uongo ili kuhakikisha kuwa Silaa harudishwi wizara ya ardhi.
 
NIMESHINDWA KUELEWA KWANINI WAMEMTOA KIJANA ALIYEKUWA ANAKWENDA KUMALIZA KERO ZA WIZARA HIYO,
-Isije ikawa walitegewa fedha za rushwa wakazipokea! Kigezo ambacho ni bashungwa tu alikiweza, alikataa!
Bashungwa muongo.
 
Mpaka sasa sijaelewa kwann wamemtoa pale
Wakati aneshasaidia kesi kadhaa
Na alikuwa anaenda vzr.
Duh hii nchi sijui Huwa wanawaza nn jmn kabla hawajafanya mabadiriko.

Wanirudishe slaa
Hii nchi ndomaana mtu akidondokewa na teuzi anakula bata na kusinzia tu ofisini mpaka muhula wake au muda wake wa kuhudumu katika ofisi utapoisha wamtoe au atoke akafanye mambo mengine.

Sababu ukijifanya kuacha kula bata na kuingia mtaani kutatua kero za wananchi basi muda mchache tu utang'olewa katika nafasi yako.

Naona hata Bashungwa kakalia kuti kavu. Muda wowote anaweza kutolewa au kuhamishwa kisa anajituma.
 
Sherehe mbona zimeshaanza kufanyika mkuu. Wewe hauoni hapa JF watu wanavyopongeza Jerry kuondolewa ardhi!
 
Yaani hii nchi ukitaka upendwe
Furahisha Maboss (CCM)
Au furahisha wananchi bila kuwabugudhi vigogo
Lasivyo utaondolewa au kuhamishwa wizara huku unaambiwa Umefanya kazi nzuri sana

Kama kutoa kauli tata kunamfanya mtu atoke kwenye nafasi
Nadhani hata Sir100 hatoshi hapo
 
Ku attack kwa maana gani yaani kuteka watu na kuwa tesa na kuwaua fafanua na onyesha mifano ...upumbavu ni kipaji
 
Sijui kwanini wamemtoa 🐼
Huwa unakesha humu JF halafu hujui kwamba nchi ni mifumo! Watu tumesema hapa Jerry hatengenezi mifumo, anafanya show binafsi, kisha anapata milungula. Sasa Wizara imebaki kama ilivyo, hakuna substantial system aliyotengeneza
 
Huwa unakesha humu JF halafu hujui kwamba nchi ni mifumo! Watu tumesema hapa Jerry hatengenezi mifumo, anafanya show binafsi, kisha anapata milungula. Sasa Wizara imebaki kama ilivyo, hakuna substantial system aliyotengeneza
Haya 😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…