Jerry Silaa na Paul Makonda ni viongozi wa mfano wa kuigwa

Jerry Silaa na Paul Makonda ni viongozi wa mfano wa kuigwa

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Appreciation post to MAKONDA na SILAA

Niliwahi kuwaeleza huko nyuma kwamba kwa dunia ya sasa hivi haiwataki watu imara, yaani watu haiwataki wale waliokuwa na misimamo yao, haiwataki wale wapiga kazi, inawataka watu walegevu.

Namwangalia Paul Makonda anavyofanya kazi yake, kiukweli ni mtu anayejitoa sana, anayepambana mno. Ni mtu ambaye anatamani kuona mabadiliko makubwa, wale walioonewa wapate haki zao, pia nimeliona hili kwa waziri Jerry Silaa.

Nawapongeza sana.

Unapowaona Makonda na Silaa wanafanya hivyo kwa kutetea wanyonge, halafu ghafla ukakunja mdomo wako na kuumizwa na kile wanachokifanya, ndugu yangu, una roho ya shetani, omba sana Mungu ikutoke.

Wakati nakua Tandale, maji yalikuwa yanatoka freshi tu lakini miaka ya tisini, ni kama 1997 hivi maji yakaacha kutoka kabisa. Yaani mabomba yote yalikufa, yakaoza, watu wakachukua scrapper na kwenda kuuza.

Tandale hakukuwa na maji ya bomba, watu walikuwa wakioga maji ya chumvi, nakumbuka miaka hiyo mpaka chai wakati mwingine tulikuwa tunapikia maji ya chumvi. Unaoga maji ya chumvi mpaka mwili unazoea chumvi.

Watu waliziba mabomba kwa makusudi kabisa. Yaani waliyaziba ili watu wao walete maji kwa magari ya maji yenye matanki wauze. Ni kweli walikuwa wanapiga pesa, dumu moja mia tatu mpaka tano. Yaani mkiliona gari la maji linakuja, watu mnakimbilia.

Haya ninayoyaongea ni mwaka 2015 hapo, si miaka mingi nyuma. Yaani tupo town, lakini mabomba hayatoi maji, hebu fikiria, upo town lakini maji ya bomba kuyaona mpaka uwe na pesa.

Wasio na pesa, walikuwa wanafulia maji ya chumvi, nguo zikawa zinapauka kishenzi. Baada ya Magufuli kuingia madarakani, Paul Makonda akaja Tandale kufanya kikao na watu kuzungumzia kero zao. Zilikuwa nyingi lakini kubwa zaidi lilikuwa la maji.

Makonda alitamka maneno machache tu kwamba anataka kuona mabomba yote yanatoa maji haraka sana, nini kilitokea? Ndani ya siku tatu, mabomba yakatoa maji na mpaka leo huduma ya maji inapatikana mpaka nyumbani kwako, unavuta bomba, unachota maji na kuogelea kama kambale.

Makonda anafanya kazi kubwa ila huwezi kuiona kama tu haijakupitia wewe. Anakupambania wewe hapo, nilimsikiliza yule jamaa wa Arusha kwa namna alivyopoteza mamilioni ya pesa, ndugu zangu, inauma, yaani unamsikiliza mtu halafu unajisemea kuna watu ni mashetani ila wamejivika mwili wa binadamu.

Unajua nini? Ngoja nikwambie kitu! Watu kama akina Makonda, Jerry Silaa huwa hawawezi kupewa sapoti na watu wengi, hata watu wengine wa chama cha CCM hawawezi kuwasapoti, unajua kwa nini? Hawahitajiki kwenye dunia ya sasa hivi.

Kiongozi unayetetea wanyonge, watu wanakuondoa mara moja, tumeona hiyo tangu kipindi cha Sankara, alipowatetea wanyonge, watu wakapita naye, hiyo imeendelea duniani, sehemu zote ipo hivyo.

Watu wanataka ukiona madudu, unyamaze, ukiona watu wanaumizwa, uchukue silaha na kwenda kuwaongezea maumivu. Leo, kijana asiye na kitu, anaona Makonda na Silaa wanatetea wanyonge, anakunja mdomo. Nikikumbuka Makonda alipotutoa, ndugu zangu nitamsapoti kwa asilimia mia moja.

Napenda viongozi wanaofanya kazi, haijalishi wana maisha gani nyuma ya pazia, ninapenda wachapakazi. Najaribu kujiuliza tu, what if mawaziri wote wangekuwa kama Silaa! What if wakuu wa mikoa wote wangekuwa kama Makonda, nadhani kuna sehemu tungekuwa, ule uonevu na mambo mengine ya kijinga yangepungua.

Wakati unaona anachokifanya ni ujinga, nenda kwenye mitandao, angalia kazi anayoifanya, anavyosaidia matatizo ya watu, halafu vuta picha wale akinamama wanaosaidiwa, akinababa wangekuwa wazazi wako, ama ndugu zako. Ungejisikiaje?

Nina uhakika kama asingekuwa Magufuli na mfanyakazi wake, Makonda, mpaka leo hii mwaka wa 2024 huduma ya maji mabombani tungekuwa tunaisikia tu redioni huku kwetu.

Kama ningekuwa naongea na Makonda, ningemwambia tu hapo alipofika, aongeze kidogo halafu akazie hapohapo.

Ninachoshangaa ni kimoja, ikitokea Makonda amefanya kitu ambacho si sahihi kwa watu wenye malengo yao binafsi, kila mtu anaongea, ila anavyotatua matatizo ya watu, wajane waliotapeliwa, watu waliofanyiwa hujuma, watu hao wamekaa kimyaaaa kana kwamba hawaoni kinachoendelea.

Kwangu mimi! Waziri bora Tanzania ni Jerry Silaa na mkuu wa mkoa bora ni Paul Makonda. Kazi zao naziona.
 
Inawezekana kweli wanafanya kazi nzuri, ila wapunguze camera😆😆😆
Waliosoma management wanaelewa kwamba kiongozi bora huwa hahitaji kutumia nguvu saana ili aonekane anafanya kazi. Kazi zake zitaonekana tu. Ukiona mtu kila siku anaita waandishi wa habari ili tujue anafanya nini jua kuna shida hapo, ni red flag 🚩
 
Uko sahihi mkuu!

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!

Makonda na Slaa wanafanya kazi na kazi zao zinaonekana.
 
Inawezekana kweli wanafanya kazi nzuri, ila wapunguze camera😆😆😆
Waliosoma management wanaelewa kwamba kiongozi bora huwa hahitaji kutumia nguvu saana ili aonekane anafanya kazi. Kazi zake zitaonekana tu. Ukiona mtu kila siku anaita waandishi wa habari ili tujue anafanya nini jua kuna shida hapo, ni red flag 🚩
Mkuu, hutaki tulio mbali tupate habari? Mbona bunge mnataka liwe live?

Bora bunge lisiwe live lakini Makonda, Slaa na Mbunge Jumanne Kishimba wawe "live!'
 
Inawezekana kweli wanafanya kazi nzuri, ila wapunguze camera😆😆😆
Waliosoma management wanaelewa kwamba kiongozi bora huwa hahitaji kutumia nguvu saana ili aonekane anafanya kazi. Kazi zake zitaonekana tu. Ukiona mtu kila siku anaita waandishi wa habari ili tujue anafanya nini jua kuna shida hapo, ni red flag 🚩
Issue ya camera ni ili kuonesha mfano kwa wengine on what should be done, kuhamasisha viongozi wengine wapate ujasiri wa kutetea haki. WaTZ tumezubaishwa sana na corruption kiasi kwamba akitokea mtu anatetea haki ambazo ni basic sana anaonekana anapenda sifa.
 
Ukilitumia vema neno 'mnyonge/wanyonge' Tanzania utapita na wengi sana
 
Issue ya camera ni ili kuonesha mfano kwa wengine on what should be done, kuhamasisha viongozi wengine wapate ujasiri wa kutetea haki. WaTZ tumezubaishwa sana na corruption kiasi kwamba akitokea mtu anatetea haki ambazo ni basic sana anaonekana anapenda sifa.
✅✅✅🙏
 
Back
Top Bottom