Jerry Silaa: Serikali iweke Tozo ya Tsh. 100 kwenye mafuta yanayonunuliwa Dar ili Kupata Pesa za Kujenga Barabara za Jiji

Jerry Silaa: Serikali iweke Tozo ya Tsh. 100 kwenye mafuta yanayonunuliwa Dar ili Kupata Pesa za Kujenga Barabara za Jiji

Pesa zimeibiwa Sasa zichukuliwe kutoka wapi? Jerry ana hoja kumbuka hiyo ni specific Kwa Dar tuu.

Pia Vyanzo vingine sio sustainable,kama Sumbawanga wananunua bei kubwa kuliko Dar Kwa nini Dar msinunie bei sawa na wao tena Kwa faida yenu?
Sasa Kama mna shida ya pesa si mrudishe Kodi ya kichwa kwa yoyote yule anaeishi na kuingia DSM!!
 
Wabunge wa ccm hawanaga uzalendo, hasa ukichukulia hao wabunge wa magufuri ambao hata uwepo wao hapo bungeni na wao huwa wanashangaa wamefikaje fikaje hapo... wabunge walioteuliwa na kichaa lazima na wao wawe vichaa vichaa tu... Hv mafuta yakipanda bei unategemea vitu vishuke bei kweli??? Alafu unayakuta eti yamevaa na skafu yenye nembo ya bendera ya Taifa... majizi matupu

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Ni kapumbavu sana hako ka mtu!

Yani anataka kuumiza wanachi kwa ajili bilioni 130, kwa nini asiseme wabanwe hawa mambwa waliochukua hizi warudishe? [emoji116]
Screenshot_20230329-152212_Telegram.jpg
 
Wabunge wa ccm hawanaga uzalendo, hasa ukichukulia hao wabunge wa magufuri ambao hata uwepo wao hapo bungeni na wao huwa wanashangaa wamefikaje fikaje hapo... wabunge walioteuliwa na kichaa lazima na wao wawe vichaa vichaa tu... Hv mafuta yakipanda bei unategemea vitu vishuke bei kweli??? Alafu unayakuta eti yamevaa na skafu yenye nembo ya bendera ya Taifa... majizi matupu

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
Ninakuwa na mashaka makubwa sana juu ya uraia wa hawa watu.

Mtanzania halisi hawezi kuwa na roho mbaya kama huyu na mwenzake Zungu
 
Akichangia mjadala wa Bajeti ya TAMISEMI, mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza kwa Serikali iweke Tozo ya Shilingi 100 kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 kwa mwaka ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil. 130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo.

Aidha Slaa amesema Tsh 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana, akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take: Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe, nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.
Lita million 3 kwa mwaka siyo sahihi.
 
Ana logic kwa kweli! Vipi kuhusu tozo za simu na miamala? Nadhani nazo tuwasukumizie wa Dar.
 
Kuna miladi ya barabara iliopo unasuasua na pesa zilitolewa na wafadhili zote. Sasa mnageukia kukamua tena wananchi. Huyu mbunge hajui athari ya kugusa bei ya petrol, kila kitu kitapanda bei. Na kawaida kupanda bei ni rahisi kuliko kushuka, ikipanda imepanda. Vyakula vitapanda bei mpaka mikoani.
 
Yaani wapige maela zaidi ya hizo kila mwaka halafu eti waseme tozo iwekwe kwenye mafuta kupata hela ya kujenga miundombinu, hivi hawa wabunge wamelaaniwa au...
Mapaka hayo
 
Wanang'ang'ania mabarabara kwa sababu wanajua kuna hela ndefu za kuiba

Hawa watu potholes zimewashinda kuziba ila wamekazana na kodi ili waibe tu

Hebu fikiria jiji linavyonuka hilo, takataka kila kona, mizoga ya mbwa wamejaa kila sehemu
Mitaro na mifereji imeziba na mvua kidogo Mavi yanajaa barabarani

Hiyo kazi imewashinda na wenyewe wakiwa katika foleni wakiona Mavi yanaelea kila kona
 
Kwa kweli barabara hasa za jimbo la ukonga ni balaa tupu! Hii proposal nimeipenda kama itakuwa transparent ya kuonekana kilichokusanywa na matumizi yake. Kwamfano ukonga peke yake inahitaji 120 billion ya kuweka sawa barabara zake,kwa uhalisia hakutakuja kuwa na mgao wa kiwango hicho kutoka serikali kuu, wote dar walitegemea dmdp ila sasa imekuwa kizungumkuti ambacho siyo leo wala kesho.so kama ni hoja nzuri ichukuliwe na serikali
 
MBUNGE SLAA.WA JIMBO LA UKONGA,NASHINDWA HATA KUANZA NA NENO "MUHESHIMIWA",KUTOKANA NA HASIRA MANA HATA SASA HIVI NINAVYOANDIKA NIMEMBEBA MTOTO WA SHULE YA MSINGI MVUTI ALIYESHINDWA KUENDELEA NA SAFARI YA KWENDA SHULE!AKITOKEA KIBOGA,KUTOKANA NA TOPE NA MAJI YALIYOJAA KTK MADIMBWI YA YA MAJI NDANI YA BARABARA MBOVU TOKA MVUTI SENTA KWENDA MPAKA GEREZA LA MVUTI.KWA TAARIFA YAKO SIPENDI UNAFIKI.! KWA KAULI YA KUWAKILISHA WABUNGE WA DAR,YA KUONGEZA 'MIA MOJA'KWENYE MAFUTA YANAYONUNULIWA DAR IMEONGEZA CHUKI TENA NA KAULI CHAFU DHIDI YAKO TOKA KWA WANANCHI MPAKA BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA NA SERHKALI.HAWAWEZI KUKUAMBIA MKIWA PAMOJA ILA UKITOKA "WANAKUNG'ONG'A"NI HERI SIE TUNAOKUAMBIA KWA UWAZI.KWA TAARIFA YAKO HAKUNA KOSA UNALOFANYA NA LITAKALOKUSHANAZA KWENYE BOX LA KURA KAMA HII BARABARA YA KM 5 TU YA MVUTI DONDWE.
 
Back
Top Bottom