Jerry Silaa: Serikali iweke Tozo ya Tsh. 100 kwenye mafuta yanayonunuliwa Dar ili Kupata Pesa za Kujenga Barabara za Jiji

Hatakiwi kurudi bungeni 2025. Wananchi wa Ukonga mpumzisheni huyo mpumbavu
 
Mbunge wa kupendekeza wapiga kura wake wakamuliwe kodi zaidi badala ya kuibana Serikali wezi wa Mali ya umma wabanwe warudishe walichokwiba huyo hafai, akasimamie biashara yake ya bar tu atuachie ubunge.
 
Hilo la kupiga ni hoja pia ila umewahi sikia Tarura pesa imepigwa? Hizo pesa zinaenda Tarura sio Jiji la Dar vinginevyo endeleeni kuongelea kwenye mashimo maana Kwa Sasa Serikali Haina pesa kwenye regular budget na ule mradi wenu wa DMDP umeyeyuka
Mnafikiria Tozo! Tozo! Tozo! Hivi kwa nini nia yenu ni kumuumiza mtanzania tu!! Kwa nini msifikirie na kuhoji fedha toka migodi ya madini inaingia ngapi serikalini na inatumikaje? Nini mchango wa migodi ya madini kwenye uchumi wetu na inampa unafuu gani mtanzania masikini huyu ambaye anabebeshwa Tozo kila kona? Ni wazo tu lakini!
 
Sina uhakika kama hawa ni watanzania.

Jerry Slaa hata bila aibu anasimama na kuomba bei ya mafuta iongezwe?

Maumivu ya tozo hayajapona kwa watanzania, tunatakiwa tena tupigwe tena kwenye mafuta.

Mishahara na marupurupu kwa wabunge vingepunguzwa naamini tungekuwa na wabunge wenye akili timamu.View attachment 2591931
Zirejeshwe zile za China na za Credit suisse,zitatosha kujenga mabarabara na sio barabara 😂
 
Akichangia mjadala wa Bajeti ya TAMISEMI, mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza kwa Serikali iweke Tozo ya Shilingi 100 kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 kwa siku ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil. 130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo.

Aidha Slaa amesema Tsh 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana, akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take: Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe, nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.

Tatizo huu sio ubunifu! kuweka kodi ni rahisi zaidi ya kuweka miradi ya kuleta mapato
 
Akichangia mjadala wa Bajeti ya TAMISEMI, mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza kwa Serikali iweke Tozo ya Shilingi 100 kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 kwa siku ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil. 130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo.

Aidha Slaa amesema Tsh 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana, akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take: Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe, nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.
Hawa ndio wabunge Magufuli alio tuletea akidai upinzani ulituchelewesha.
Majinga haya hayalipi kodi hayana maumivu yako na pesa za wananchi zinaliwa kila kona yenyewe yamerundika kama Mazuzu pale yanalipwa mishahara kwa kodi zetu na bado yanapenxekeza wananchi tuumizwe zaidi.
Kwa nini wasipunguze mishahara ya wabunge ili pesa hizo zitumike kujenga hizo barabara?
 
Tumuonee huruma mwanachi.
 
Lini uliwahi sikia pesa imeibiwa Tarura? Nyie ni kuwaacha hivyo hivyo kwenye mashimo yenu.

Jiji gani mvua ikinyesha Jiji liko paralysed?

Pesa zimepigwa, ila mwananchi ndio abebe mzigo wa kuongezewa Bei kwenye mafuta?. Nani anamuonea huruma mwanachi wa kawaida.
 
Pesa zilizopigwa sio za Barabara ni za Miradi mingine,wapi umesikia Tarura wamepiga pesa ya tozo ya mafuta?
 
Hawa ndio wabunge Magufuli alio tuletea akidai upinzani ulituchelewesha.
Majinga haya hayalipi kodi hayana maumivu yako na pesa za wananchi zinaliwa kila kona yenyewe yamerundika kama Mazuzu pale yanalipwa mishahara kwa kodi zetu na bado yanapenxekeza wananchi tuumizwe zaidi.
Kwa nini wasipunguze mishahara ya wabunge ili pesa hizo zitumike kujenga hizo barabara?
Hawalipi Kodi namna gani?
 
Tumuonee huruma mwanachi.
Mbona humuonei huruma mwananchi wa Mkoani ila wa Dar tuu ndio aonewe huruma?

Silaa ana Hoja,haiwezekani bei ya mafuta Dar na mikoani Ina tofauti Kati ya 200-700 kutegemea na sehemu..

Serikali Iweke Tozo zaidi Kwa wanunuzi wa Dar Ili ipate pesa za kujenga Barabara Dar na pia kuleta walau uwiano na mnunuzi wa Mkoani..

Mbona Jasho la watu wa Mkoani ndio linajengwa huko Dar?
 
Yaani wapige maela zaidi ya hizo kila mwaka halafu eti waseme tozo iwekwe kwenye mafuta kupata hela ya kujenga miundombinu, hivi hawa wabunge wamelaaniwa au...
Hoja mzuri,ispokuwa hakuna udhibiti wa matumizi ndani ya serikali,hivyo wazo lake linakufa kibudu.
 
Pesa zimepigwa, ila mwananchi ndio abebe mzigo wa kuongezewa Bei kwenye mafuta?. Nani anamuonea huruma mwanachi wa kawaida.
Mbona unalazimisha upuuzi wako? Nimekuuliza umesikia wapi CAG akisema pesa ya tozo ya mafuta inayoenda Tarura kujenga Barabara imepigwa?

Hiyo pesa itaenda Tarura na Barabara zitajengwa tofauti na hapo mtaogelea kwenye madimbwi Hadi mkome..

Jiji la hovyo mvua ikinyesha linakuwa paralysed.
 
Itategemea huyo mkandarasi atalipwa kwa sarafu ipi; kama atalipwa kwa sarafu ya kigeni, ni kumtesa tu mlipa kodi; kama atalipwa kwa sarafu ya kwetu suluhisho ni ku-print fedha inayotakiwa.​
 
Wabunge wanapokea zaidi ya 12m kwa mwezi, tozo ya 100 kwa kila litre siyo issue. Tatizo kwetu sisi! Aliyeshiba kuachia mashuzi ni haki yake.
 
Back
Top Bottom