Jerry Slaa aanza kulewa madaraka , adai watakaoshindwa kutatua migogoro ya ardhi atawatatua wao

Jerry Slaa aanza kulewa madaraka , adai watakaoshindwa kutatua migogoro ya ardhi atawatatua wao

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Lukuvi alijitahidi sana kuingoza hii wizara kwa weledi kwa kiasi kukubwa. Alitatua migogoro mingi sana tena kwa yeye mwenyewe kufika eneo la tukio na pale wizarani alipunguza sana urasimu na rushwa. Nilihangaika miaka mingi sana na kutumia gharama kubwa kutafuta hati ya ardhi lakini nilikuja kuipata wakati wa Lukuvi akiwa waziri bila gharama yoyote.

Kama kuna kete CCM ingeweza kuwasaidia walau kidogo basi wangemrudishia huyo Lukuvi hiyo wizara maana baada ya yeye kuondolewa kwenye hiyo wizara hakuna asiyejua kinachofanywa na mafisadi wa ardhi nchi nzima kuanzia mabwepande, bagamoyo, mbarali, kigamboni kwa kutaja tu hayo maeneo machache lakini kiukweli sasa hivi kilio cha unyangányi wa ardhi ni Tanzania nzima.
 
Back
Top Bottom