Area 56
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,555
- 4,085
Mitano tena kwa Jesca Magufuli
===============
Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi ameendelea kufanya mikutano yake ya kampeni ambapo leo Alhamisi Septemba 4, 2025 ameanza katika eneo la Isaka katika Jimbo la Msalala mkoani Shinyanga.
Pamoja na Nchimbi kunadi sera za chama chake chini ya uongozi wa mgombea Urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan shangwe iliibuka pale Jesca Magufuli alipokuwa akizungumza na kukiombea kura chama hicho.
Jesca ni mtoto wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli, ambaye pia mgombea ubunge mteule wa viti maalumu kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Jesca amewaambia wananchi wa Isaka waendelee kukiamini Chama cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan anayepambana kuliletea taifa maendeleo.
Jesca amesema CCM ndio chama kinachojali na kusikiliza vilio vya Watanzania hivyo ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kwenda kumpigia kura mgombea wao wa urais, Rais Samia, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa maendeleo ya maeneo yao.