Interception ya makombora kwa sasa haipo kwenye vigezo vya majeshi bora duniani. Kwanza kwa huu mfumo wa Israel, umeanza kutumika majuzi tu hapa na ulitengenezwa kwa pamoja kati ya US na Israel. Na kwa upande mwingine, mfumo wenyewe sio sustainable kwa sababu, kwa mujibu wa gazeti la Guardian UK, ambao walimnukuu Afisa wa IDF, wanadai wakati Iran gharama ya kutengeneza makombora yao ni Pound 80K kwa Kombola, gharama ya Kombora la kutungua hilo kombora moja ni Pound 800K! Yaani Mara 10. Halafu kuna aina nyingine ya interceptor wanayoitumia, yenyewe ni ya muda mrefu kidogo! Hiyo gharama yake ndo balaa manake inagharimu Pound 3.5M ku-intercept kombora la Pound 80K! Baada ya kusoma hii habari ndo nikajua kwanini US always atam-support Israel kwa misaada ya kijeshi kwa sababu unatengeneza single interceptor kwa gharama kubwa hivyo, lazima uwe na practical use ya kuthibitisha ubora wake ili uweze kushawishi majeshi mengine duniani kulipa pesa nyingi yote hiyo! Ujinga ni kwamba, ukikutana na jeshi lenye missiles nyingi, kwa hiyo gharama lazima utaishiwa pumzi tu kwa sababu ni very costful kuwa kiasi kikubwa cha hizo interceptors.Nimeuliza hivi baada ya kuona jeshi la Israel ambalo ni namba 17 kwa ubora duniani linajitahidi sana kwenye upande huo.