Jeshi la Burkina Faso lasema lilizuia njama 'kuu' ya mapinduzi

Jeshi la Burkina Faso lasema lilizuia njama 'kuu' ya mapinduzi

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
17,999
Reaction score
21,560
Jeshi la Burkina Faso lasema lilizuia njama 'kuu' ya mapinduzi.

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imesema ilitibua "njama kubwa" ya kumpindua kiongozi wa kijeshi Kapteni Ibrahim Traoré, huku jeshi likidai kuwa wapangaji hao walikuwa na makao yao katika nchi jirani ya Ivory Coast.

Waziri wa Usalama Mahamadou Sana alisema jaribio la mapinduzi liliongozwa na wanajeshi wa sasa na wa zamani wanaofanya kazi na "viongozi wa kigaidi". Nia ilikuwa kushambulia ikulu ya rais wiki jana, aliongeza.

Lengo la mpango huo lilikuwa "kupanda machafuko kamili, na kuiweka nchi chini ya usimamizi wa shirika la kimataifa", Sana ilisema kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumatatu.

 
22 April 2025
Ouagadougou, Burkina Faso

Communique /Taarifa kwa Umma, serikali imenasa mawasiliano ya kundi lililopanga kupindua serikali

Vyombo vya usalama Burkina vimeweza kubaini na kuvunja njama za mapinduzi zilizoongozwa na askari mtoro Bahare Abdaraham..


View: https://m.youtube.com/watch?v=5rYlXUHfhCY
Video: waziri Mamadou Sana akitangazia umma

Njama hizo za mapinduzi zilipangwa kushawishi baadhi ya askari wa jeshi la taifa washiriki, huku viongozi wa njama hizo wakiwa wamejichimbia Abidjan Ivory Coast ... waziri Mamadou Sana wa wizara ya mambo ya usalama asema mubashara akisoma taarifa ya serikali kwa umma.

Communique inataka wananchi wote kuwa watulivu na kuwa macho kuripoti mara moja kwa vyombo vya usalama watapoona kitu au watu wanaowashuku kuwa na mienendo isiyoeleweka.

Lengo la njama hiyo lilikuwa kushambulia ikulu ya rais wiki iliyopita 16 April 2025, kwa nia ya " kuleta machafuko kamili " na kuiweka nchi chini ya usimamizi wa ushirika wa kimataifa...

Waziri wa Usalama wa Burkina Faso, Mamadou Sana, alizungumza kuhusu maendeleo hayo, akisema kwamba jaribio la mapinduzi liliongozwa na wanajeshi wa sasa na wa zamani wanaoshirikiana na " viongozi wa kigaidi ...

1745345276803.jpeg

Kiongozi wa kijeshi Captain Ibrahim Traoré wa Burkina Faso
 
22 April 2025
Ouagadougou, Burkina Faso

Communique /Taarifa kwa Umma

Vyombo vya usalama Burkina vimeweza kubaini na kuvunja njama za mapinduzi zilizoongozwa na askari mtoro Bahare Abdaraham..


View: https://m.youtube.com/watch?v=5rYlXUHfhCY
Njama hizo za mapinduzi zilipangwa kushawishi baadhi ya askari wa jeshi la taifa washiriki, huku viongozi wa njama hizo wakiwa wamejichimbia Abidjan Ivory Coast ...

Communique inataka wananchi wote kuwa watulivu na kuwa macho kuripoti mara moja kwa vyombo vya usalama watapoona kitu au watu wanaowashuku kuwa na mienendo isiyoeleweka

View attachment 3312572
Kiongozi wa kijeshi Captain Ibrahim Traoré wa Burkina Faso

Kila wiki wanatoa hizo drama

And btw, most of drama online kuhusu jamaa sio za kweli
 
Hili ni suala la muda tu

Round inayofuata huwatafanya makosa lazima watamla kichwa
 
Back
Top Bottom