Jeshi la Burkina Faso lasema lilizuia njama 'kuu' ya mapinduzi

Jeshi la Burkina Faso lasema lilizuia njama 'kuu' ya mapinduzi

Ibrahimu Traore amekuwa role model hata kwa wasio wanajeshi wanatamani atokee mwanajeshi kama huyo apindue nchi zao zenye demokrasia za kimagumashi kwa chaguzi za kidanganyifu
 
Hii ni communique kutoka serikali ya Burkina Faso kuthibitisha tetesi zilizokuwa zimeenea. Sasa ni rasmi ndiyo maana communique officiel imetolewa kutaja wahusika, nchi zinazofadhili, kuwezesha mipango iliyofeli.
Hakuna kitu kama hiko. Hizi ni propaganda tu za kujaribu kuwatoa mchezoni wenye mawazo ya kujaribu kupindua serikali yake. Ni lazima kila baada ya muda fulani walete hizo porojo ili kuwakatisha tamaa maadui.
 
Duh si anapendwa how come wanataka kumpindua
 
Huyo kumpindua itachukua muda kidogo mpaka ule upande wa Putin uzembeee 😂😂😂 sasa HV n ngumu Sana kama ngamia kupenya tundunu la sindano
Putin huyo huyo aliyeshindwa kumsaidia Assad asitolewe mkuku pale Syria.! Au luna Putin mwingine!? Putin huyo huyo anayetegemea askari wa kukodi toka Korea Kaskazini na China huko Ukraine!? Ndio amsaidie Traore!?
 
Hata Assad mrusi alikuwa nyuma na mbele yake. Na pembeni yake alikuwa Ayatollah.
Hawa watu wanamtaja taja Mrusi naamini huwa hawafatilia habari, au kama wanafuatilia, basi wana memory ya kuku. Eti Putin!
 
Capitalist NI wanafiki Sana na ndio maana jamaa alisusia mualiko WA trump .

Traore NI mfano WA kuigwa Africa nzima


DENI la Taifa NI trillion Mia .


Kuna siku NCHI yetu ITAUZWA .

Capitalist NI wanafiki Sana na ndio maana jamaa alisusia mualiko WA trump .

Traore NI mfano WA kuigwa Africa nzima


DENI la Taifa NI trillion Mia .


Kuna siku NCHI yetu ITAUZWA .
Hata kama haitauzwa ila uhuru wa kiuchumi ndio bye bye milele
 
Putin huyo huyo aliyeshindwa kumsaidia Assad asitolewe mkuku pale Syria.! Au luna Putin mwingine!? Putin huyo huyo anayetegemea askari wa kukodi toka Korea Kaskazini na China huko Ukraine!? Ndio amsaidie Traore!?
Asadi ameanza kutafutwa lini na wamemnasa lini?
 
Hivi hawa viongozi wa mapinduzi wa Kiafrika hawawezi kujifunza kwa Jerry Rawlings?

Umepindua Nchi ukakuta mifumo mibovu kwanini usiibadili hiyo mifumo na kutengeneza mifumo bora zaidi ambayo itaondoa ubadhirifu, ufisadi,wizi na rushwa kwenye serikali?.

Tatizo la viongozi na wananchi wa kiafrika wanaamini kwenye mtu kuliko kwenye mifumo bora. Kinachotakiwa ni mfumo bora, Hayo matrekta anayonunua bila kutengeneza mifumo bora ya kiuongozi ni kama hekaya za abunuasi kwani akiondoka yeye basi kila kitu kitarudi kama zamani.


Afanye kama Jerry rawlings alivyofanya baada ya mapinduzi kwa kutengeneza katina iliyo bora, mifumo mizuri ya ukusanyaji wa mapato, atengeneze mifumo bora ya haki jinai kwa kuwawajibisha wale wote wataofanya ubadhirifu wa mali za uma ikiwemo yeye mwenyewe.

Mifumo mizuri huzaa watu na viongozi bora, kuendelea kuamini katika mtu ni wendawazimu, watu huja na kuondoka ila mifumo bora huuisha Taifa bora.
 
Jeshi la Burkina Faso lasema lilizuia njama 'kuu' ya mapinduzi.

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imesema ilitibua "njama kubwa" ya kumpindua kiongozi wa kijeshi Kapteni Ibrahim Traoré, huku jeshi likidai kuwa wapangaji hao walikuwa na makao yao katika nchi jirani ya Ivory Coast.

Waziri wa Usalama Mahamadou Sana alisema jaribio la mapinduzi liliongozwa na wanajeshi wa sasa na wa zamani wanaofanya kazi na "viongozi wa kigaidi". Nia ilikuwa kushambulia ikulu ya rais wiki jana, aliongeza.

Lengo la mpango huo lilikuwa "kupanda machafuko kamili, na kuiweka nchi chini ya usimamizi wa shirika la kimataifa", Sana ilisema kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumatatu.

Sometimes ili kuweka mambo sawa na kuwatisha wapinzani, wana mapinduzi kama Ibrahim Traore wanaweza kujiandalia mapinduzi hewa ili kujiimarisha kijeshi na kiulinzi. Ni mawazo yangu tu. Japo namkubali sana huyo dogo mtata.
 
Back
Top Bottom