Jeshi la Ethiopia laingia Kenya na kuua wakenya

Nyie rudini nyumbani imarisheni mipaka yenu,
Hayo mengine sijui ya kukamata miji mingine watajua wao huko hadi siku watie akili.
Rais Uhuru ameshasema jeshi halitarudi hadi Shabab wamalizwe kabisa. Lakini siamini kwamba ugaidi unaeza kumalizwa kabisa. Marekani wamepigana na Taliban huko Afghanistan kuanzia mwaka wa 2001. Yaani miaka kumi na tisa na vita bado inaendelea. Sisi tumekuwa Somalia kuanzia mwaka wa 2011. Yaani miaka tisa sasa na bado vita inaendelea. Wacha tutaona siku za usoni itakuwaje.
 
Huwa nashangaa saana mtu anaposema hakuna nchi iliyowai kuwamaliza magaidi aliyakuwa sijawai sikia magaidi wakiwaletea mchezo urusi na china

Sent using Jamii Forums mobile app
Russia walitandikwa na Taliban wakati Osama alikuwa bado kijana barobaro hadi Urusi wakatoroka Afghanistan kwa kilio kikubwa. Walipoteza wanajeshi wengi na mali nyingi. Wanahistoria wanasema kuwa vita hio ilichangia pakubwa kuvunjika kwa Soviet Union.
 
Sio Rais pekee hata wakenya wengi wanatamani jeshi lenu lirudi nyumbani,
Nadhani kuna maslahi ya Rais wenu kule ndio maana anaweka ngumu,
Basi hata ikishindikana kurudi angalau ulinzi uimarike na kitengo chenu cha inteligensia kimwage cha kutosha wawe wengi zaidi,
Mbona Uganda pako freshi tu.
 
Hamna nchi iliyofanikiwa kumaliza ugaidi. Hata Marekani wameshindwa hivi sasa wameamua kufanya mazungumzo na Taliban. Nyie Ldc ndio mtawezana na magaidi na hata hamna uzoefu huo wa kupigana nao? Wakija Tanzania watalala na nyinyi na kuzaa na nyinyi.
Kule South Sudan mlikoshindwa mkafurushwa na Ban Ki- Mon nako pia ni ugaidi?. Kama mlijua humtoweza shinda Alshabaab kwanini mlipeleka walevi wenu wa KDF huko Somalia ili wakauliwe kama kuku?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nyie mna bidii mbona nyie masikini wa kutupwa. Tukiita Waganda au Warwanda hapa na kuwauliza nani wazembe kati ya Wakenya na Watanzania basi wote watasema nyie ndio mnajulikana kwa uzembe uliokithiri.
Hahahaha, mzembe ni yule anayepewa chakula cha bure na UAE, nchi ambayo 100% ya ardhi yake ni jangwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninyi mlichofanya cha maana ni kuwapa hao rebels wa Mozambique makao ila hamkutuma jeshi lenu kupigana na Wareno. Mliwachia Frelimo hio kazi ya kupigana na Wareno.
Frelimo ilianzishwa na nani?, hapakua na kitu kilichojulikana kama Frelimo kabla, Alikianzisha Nyerere na kutoa wanajeshi wa Tanzania 100% kuingia Mozambique, walipokua wanakomboa maeneo ya Msumbiji, ndio vijana wa Msumbiji wakaanza kujiunga na jeshi la Tanzania, soma vizuri historia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uganda hawana border na Somalia kwa hivyo wanaweza winda Shabab na kuwazaba makonde na Shabab kukosa jinsi ya kulipiza kisasi. Sisi kwa bahati mbaya tuna border na Somalia ya zaidi ya kilomita mia tano na border hio haina fence wala ukuta wowote na KDF haiko katika kila eneo la border. Hapo ndio Kenya inastahili kujirekebisha na kujenga ukuta wa mawe wa mita tano na kuweza ulinzi wa kutosha hata kutumia drone. Lakini hapa Afrika mawazo chanya kama haya hayapewi uzito.
 
Warusi walipoona mambo yamekuwa magumu(mkono wa CIA) wakaamua kuondoka alafu wakajiimarisha zaidi kuepuka ugaidi

Mfano mwingine ni Iran amezungukwa na mataifa yenye magaidi ila ni vigumu magaidi kupenya na kufanya ugaidi ndani ya mipaka yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule South Sudan mlikoshindwa mkafurushwa na Ban Ki- Mon nako pia ni ugaidi?. Kama mlijua humtoweza shinda Alshabaab kwanini mlipeleka walevi wenu wa KDF huko Somalia ili wakauliwe kama kuku?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hivyo jeshi la Kenya halijapata mafanikio yoyote Somalia. Hii ni kwa mujibu wa profesa mmoja JF.
 
Huko ndio kufeli kwa shirika lenu la ujasusi halikujua kuwa mnachangia border ya kilometre 500 na Somalia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni kujenga ukuta na kuimarisha ulinzi wa nguvu tena kwa kujenga kambi ya jeshi,
Mkifanikiwa hapo itakuwa safi sana.
 
Nimesoma historia sana ila sijawahi kusoma hio story unayonipa. Nipe link nisome, pengine utanibadilisha mawazo. Hio link lazima ionyeshe kuwa jeshi la TZ lilitumika kupigana na Wareno.
 
Vipi kuhusu Ethiopia?, acheni visingizio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma historia sana ila sijawahi kusoma hio story unayonipa. Nipe link nisome, pengine utanibadilisha mawazo. Hio link lazima ionyeshe kuwa jeshi la TZ lilitumika kupigana na Wareno.
Ingio Google, tatufa kuhusu kuanzisha kwa "Frelimo" na vita vya ukombozi wa Msumbiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iran inapigana na Isis huko Syria ila Isis kwa sasa haina nguvu na pia Iran inalinda border yake kwa ujasiri sana. Hata Kenya ikilinda border yake mashambulizi yataisha lakini ugaidi Somalia hautaisha. Pia Iran imepigwa mabomu na magaidi mara kadhaa ila wamedhibiti ulinzi vizuri ndani ya border. Urusi pia wamepigwa na magaidi ila wameweza kuwadhibiti ndani ya mipaka ya nchi ila hizi nchi haziwezi kumaliza ugaidi nje ya mipaka yao.
 
Hamna nchi iliyofanikiwa kumaliza ugaidi. Hata Marekani wameshindwa hivi sasa wameamua kufanya mazungumzo na Taliban. Nyie Ldc ndio mtawezana na magaidi na hata hamna uzoefu huo wa kupigana nao? Wakija Tanzania watalala na nyinyi na kuzaa na nyinyi.
Unaifaham Russia???
Magaidi wote wanaogopa kukanyaga pale wanaelewa nn kitawakuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Low thinking capacity....!Jinga veri machiii...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…