Tony254 babayao255 Rich Ze Best Kosugi joto la jiwe
Msumbiji
Vita isiyojulikana sana wakati wake ilikuwa kuingilia kwa JWTZ katika nchi jirani ya
Msumbiji kwa shabaha ya kusaidia serikali ya chama cha
Frelimo. Kulikuwa na vipindi viwili vya usaidizi huu.
Kipindi cha kwanza kilikuwa 1977-78 wakati jeshi la
Rhodesia iliingia ndani ya Msumbiji. Rhodesia (leo:
Zimbabwe) ilitawaliwa wakati ule na serikali ya walowezi Wazungu chini ya
Ian Smith. Warhodesia walijaribu kuangamiza vikundi vya wapinzani kutoka kwao waliotafuta kupindua serikali ya walowezi wakijificha katika Msumbiji na kushambulia kutoka huku. Hapo vikosi vya Rhodesia viliingia mara kadhaa ndani ya Msumbiji halafu Rhodesia ilianzisha harakati ya
Renamo kwa kukusanya wapinzani dhidi ya Frelimo na kuwapa silaha. Baada ya kuenea kwa vita ndani ya Rhodesia jeshi lake lilishambulia kambi kubwa ya wapinzani chini ya
Robert Mugabe katika
Mkoa wa Manica wa Msumbiji. Hapo Tanzania ilituma wanajeshi wake kwa shabaha ya kuimarisha utawala wa Frelimo wakarudi kwao mwaka ufuatao 1978.
[10]
Baada ya
Mapatano ya Lancaster House ya mwaka 1979 vita ya Rhodesia - Zimbabwe ilikwisha. Sasa ilikuwa serikali ya
apartheid ya
Afrika Kusini iliyochukua nafasi ya mdhamini wa Renamo. Miaka iliyofuata iliona vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji kati ya Frelimo iliyosaidiwa na
Urusi ikifaulu kutetea miji na Renamo iliyosaidiwa na Afrika Kusini ikifaulu kutawala sehemu kubwa ya mashambani na vijiji vingi. Mwaka 1982 maraisi Machel wa Msumbiji na Nyerere walipatana kutumwa kwa kikosi kidogo cha askari 200 wa JWTZ kwa kazi ya washauri kwenda Msumbiji.
[11] Mwaka 1987 Tanzania iliamua tena kutuma askari wengi wa JWTZ hasa kwa kusudi la kutetea
Mkoa wa Zambezia dhidi ya Renamo. Waliondoka tena mwaka 1988.
[12]