Unatakiwa ujue kabla US akija kukushambulia anafanya aerial denial kwanza. Zile B-2 na B-1B Lancer hazipo kwa ajili ya kutalii angani.
1. Anashambulia kwa B-2 ambazo ni stealth anaua air defence batteries za Iran.
2. B-1B zinakuja kushambulia bases na vituo muhimu vya jeshi.
3. B-52 ndo zinakuja na tani za mabomu ya kutosha kuharibu factories za silaha na vituo vya umeme.
Hizo ndege zote hapo zina uwezo wa kutokea nyumbani kwenye airbases kibao kama Andersen na Guam.
Kuhusu b2 mkuu nina mashaka hata nikiangalia mission zake, b2 imekwenda Afghanistan, Libya kupiga Isis 2011 na pia Serbia kwenye kosovo war 1999, sijaona cha ajabu hapo kwenda kupiga watu wana RPG na AK-47.
Kumbuka rq-170 ilikuwa stealth na USA walijidanganya hivyo hivyo kwamba isingeonekana, they were wrong, hawakuipiga hata missile, wali intercept mawasiliano wakakiteremsha chini kama cha kwao, ilikuwa ni aibu kubwa mnoo kwa USA.
Hapo unajua hao jamaa sio tu kwenye radar systems wapo vizuri bali hata electronic warfare wapo far away.yaani ili kuwa detected halafu ikawa hacked,
shikamoo Iran.
Shangaa rq 170 ilivyo shushwa na ilikuwa stealth right?
kitendo cha USA kurusha stealth drone kama ile nchini Iran ilikuwa wana jiamini asilimia zote hakitoonekana right?
kumbuka hio rq 170 ilisha tumiwa afghanistan na pia Pakistan kwenye ile mission ya kumsaka Osama, USA walifanya pia jamming kwenye radar za Pakistan na Pakistan hawakujua nini kinaendelea.
Hio b2 inakwenda altitude ya 50000 feet kama ilivyo rq 170 pia ni 50000 feet, kwa kuwa waliona imefanikiwa hio aircraft kuingia sehemu mbali mbali kwenda kupiga picha za kishu shu shu, wakaona sasa ni wakati murua wa kuingiza Iran, guess what? nakumbuka tu USA ilisema hio ndege ilikuwa operated na CIA na sio USAF 😂 😂 😂 .
Sasa na hio b2 tusubiri tu ifike na yenyewe kwenye anga la Iran ushuhudie mwenyewe, Iran sio Serbia,Iraq au Libya.Tegemea kukutana na challenge nzito sana ikiwemo kuipoteza hio b2 wakati zipo 21 tu kama sikosei.
So its not easy tukizungumzia kwa mifano hai.
rq 170
b2 bomber
Kwa hio wazo lako la kutuma b2 Iran hata USA hawaliwazii plus kumbuka stealth aircraft haina maana haionekani bali hata radar za bongo zinaweza kuona b2, ipo hivi.
Radar ina uwezo hadi wa ku detect drops za maji, yaani mvua ikiwa inanyesha radar inaona vizuri tu zile drops na vitu vingine kama ndege wa angani ila vinakuwa vidogooo mno, ndio maana utasikia kuna radar za hali ya hewa.
Kwa kesi ya stealth bomber kama b2 zimetengenezwa ku absorb radar waves au pengine kuzi direct pengine, tazama vizuri b2 muundo wake, hivyo kwa kufanya hivyo waves zinarudi kidogo kwenye radar, radar inaona ni kadude kadogo tuseme ndege wa angani na ina ignore, kwa maana ukisema utazame kila kitu kwenye radar utaanza kuona kama zile tv za visogo zinapokosa channel sisi tulikuwa tunasema inaonyesha mchele.
Ili kuleta maana wataalamu wana seti aina fulani za waves tu ziweze kuonekana kwenye radar na hapo ndipo stealth aircraft ina ichanganya radar kwa kuwa inarudisha waves sawa na mwewe anapaa angani, hivyo wana ignore, lakini b2 hata radar ya bongo inaona vizuri tu, hakuna stealth ya kui confuse radar 100%, beleive it or not.
Kuna bomber ilikuwa inaitwa f-117 ilipigwa huko serbia ikashuka ilikuwa ni stealth kama hio b2 ilikuwa ni mwaka 1999 na kipindi hicho f-117A ilikuwa ni mtambo hasa na USA alikuwa ana bomber ambayo ni stealth na advanced sana, but guess what? ilipigwa na s-125 missile😂😂😂.Yugoslavia hao waliiteremsha vizuri mno.
f-117a
Sasa USA hakutegemea s-125 ingepiga f-117a right? so tegemea b2 kupigwa hata na s-300.
Akimaliza anakuja majini.
1. Analeta aircraft carriers maeneo ya ghuba ya Aden na Mediterranean sea.
2. Akitoka hapo anatoa ndege zake kina E-2D kwa ajili ya early warning kulinda carrier group. Ndege zinatrack kila missile, boat, warship, na takataka yoyote iliyo umbali wa kutosha around carrier group.
Iran ina speed boats zenye kubeba cruise missiles, submarines ambazo ni stealth zinabeba torpedoes, pia kwenye radar technology usiwapimie, wana boats zinakimbia sana kuliko hizo ships na boats za US navy hapo nazungumzia boat zinaitwa seraj ambazo zinashikilia record kwa kasi.
USA wamekuwa wakijaribu sana kutengeneza silaha ya kuzikabili hizo boats lakini gharama inakuwa kubwa sana kuweka hizo laser weapon kwenye kila meli na mpaka sasa wanayo 1 tu.
Range ya hio laser ni 2km wakati missile za kwenye speed boats za Iran ni cruise missile, hivyo zitatumwa boats za kutosha hapo na missile ambazo hazina idadi zitaanza kumiminwa kuelekea kwenye hilo li carrier kwa mbali kabisa, pia hizo warships zitaweza kukabili mashambulizi toka speed boats kwa kuzishambulia au kulinda hilo li carrier?
Hapo unaona warships zitazidiwa kabisa, hazitoweza hilo battle.
Iran wana anti ship missile kama vile noor, halafu mmevamia Iran kwenye eneo lake bado USA ana kibarua.
Ukizingatia Iran ita target military za base ya USA hapo middle east kwa missile za ballistic
3. Wakati huo ndege kama Poseidon na Sentry zipo angani karibu na Iran kucheki usalama, zina powerful sensors na systems za kutrack submarines na viboti vyao hivyo. Usinambie air defence systems zitazidondosha, zina range ya mbali ambako ground to air missiles hazifiki.
Hizo ndege ni za kawaida sana sijui unatumia kigezo gani kusema haziezi dondoshwa, ipo hivi.
Hio Poseidon ni imetokana na boeing 737 na hio Sentry ni boeing 707, uwezo wao wa kuruka juu ni wa kawaida kama ndege za kawaida tu, 12km above au 40000 feet, kumbuka bomber huwa zinakwenda mpaka 50000 feet na bado zinatandikwa tu, niseme hakuna tofauti na ile boeing 747 ya raisi wa USA, ikiwa imeongezewa mifumo ya ulinzi na mengineyo, lakini hizo ni boeing 737 na nyingine ni boeing 707, sasa how comes SAM itashindwa kufika?😂😂
Hizo ndege za Poseidon zinatoa taarifa kwa carrier group kwamba kuna base flani inarusha ndege angani, carrier group inatoa air fighter kina F-16 na F-15, Iran ana ndege gani za kupambana na hizi?
Wakati huo E-2D Advanced Hawkeye inatoa taarifa kwa missiles zinazoifata carrier group, pale kwenye group lazima destroyers kama Arleigh Burke ziwepo. Kazi yake ndo hiyo, kazi ya Arrow 3 ni kutungua anti-ship missiles hizo. Ikishindwa kuna clone-in weapon system (CIWS) kazi yake ni ya mwisho kabisa. Hapa sijazungumzia kabisa masuala ya electronic warfare, F-16 na E-2D ndo kazi yake. Katika ndege zote tuachane na F-22 na F-35, hizi zitawaliza sana maana ni stealth.
Unadhani hata hapo watafika? sidhani!! Hizo Poseidon zipata nafasi gani kufanya surveillance angani? how?
Hapo Iran kaishasambaza base zote middle east, hilo li carrier limepiigwa na speed boats na war ships zimezamishwa, hizo f16 na f15 zinatokea wapi? kumbuka narudia tena mmeivamia Iran.
Kiu halisia ingekuwa simple hivyo USA kutaka kuikabili Iran sio leo, Iran imepiga mkono miaka 8 akiwa na wanaompatia misaada ni Syria na Libya can you imagine?
Iraq iliyokuwa ina pigana na Iran ilikuwa na msaada toka USA, USSR, Saudia, Kuwait, European countries n.k, kumbuka Iran ilikuwa katika kipindi kigumu cha vikwazo katika manunuzi ya silaha n.k, so wale wa Persia waone vile tu, USA inawajua vizuri, in short Iran ilichangiwa na licha ya Iraq kupewa modern tools zote, haikufua dafu.
Respect to Iran
Hata troops hawatoingia Iran, plus Iran ni kubwa 3x ya Iraq, so usichukulie ita ile ya Iraq uje ufananishe na vita ya Iran.