From my own memory; sija Google popote. Baada ya kina Ayatollah na team yake kumpindua rais/mfalme Shah pale Iran (ikumbukwe Shah alikua pro West like Egypt, Saudia etc ) USA na his allies waliona fursa la kula mafuta ya Iran imekwisha, Rafsanjani, Khomein nk walitaka kuongoza nchi kidini na kujiondoa direct from USA then team USA wakaona ni lazima kumrudisha Shah or somebody ambaye wanaweza kum remote, now kuna mwamba alikua anaitwa Saddam Hussein, huyu jamaa alijaribu kupindua mara kadhaa serikali ya Iraq na akashindwa, homework yao iliwaonesha wamtafute huyu jamaa, Saddam nadhani alikimbilia Misri, baada ya kumpa mbinu, ndio sasa akafanikiwa kuingia madarakani Iraq kwa mapinduzi; homework No 2, anzisha vita na Iran ili kuiondoa madarakani serikali iliopo ambayo ni ya msimamo mkali. Vita ikaanza, zilipigwa kwa miaka 8. Mwaka 1987, jeshi la maji la USA lilitungua ndege ya abiria aina ya Airbus mali ya Iran ilikua ikitoka Tehran to Paris, abiria 270 walipoteza maisha na wengi wao walikua raia wa Iran, USA ikakiri baadae kwamba ni wao wametungua ndege bahati mbaya, walidhani ni ndege ya kijeshi/kivita. Now vita hi ilikwishaje? Saddam Hussein baadae alikuja kujua kwamba baadhi ya silaha alizonazo Iran zilitoka USA I think na Israel hi unayoisema. Hiki kitendo kilimuudhi sana Saddam Hussein, Saddam aliona kama kasaritiwa; why anapigana vita na jirani yake kwa kuongozwa na USA, the same USA ndio tena ka provide silaha kwa adui? Finally hawa 2 wakafikia makubaliano ya kuachana na hi vita. Source of my information ni gazeti la Sauti ya Umma (SYU) kutoka Iran, baba yangu alikua kiongozi wa kidini miaka hiyo na tulikua tunaletewa hilo gazeti hilo kila mwezi; the only thing ambacho sikukitoa kwenye hilo gazeti ni habari ya hizo silaha za USA to Iran, the rest ni kutoka maktaba yangu ya kichwani, habari ambazo bado nina kumbukumbu nazo almost 40 years now.
Well, baadae niliasi dini ya baba yangu na kua Mkristo...., twende kazi.