Jeshi la Kenya dhidi ya M23: Je, Kenya itaweza kufanya kile ilichofanya Tanzania mwaka 2013?

Haya maelezo ndio yanaonyesha KDF itapigwa na M23?

Yani natafuta justification ya kuidharau KDF sioni. Mnaleta story tu, Kenya nayo ianze leta story za Somalia au namna gani. Aliyewaambia ukidharau jeshi la jirani jeshi lako linakuwa bora nani
 
Timeline ya Kenya na mission wanapanga wao. Huwezi wapangia au kutaka uwalinganishe eti ndani ya dakika moja wawe wameanza operation. Hata wakiamua kuondoka vitani bila kuwafanya chochote M23 bado haiakisi uwezo wao kijeshi bali matakwa ya kisiasa.

Marekani mwaka 2020 iliondoka Afghanistan kwa makubaliano na Taleban, miaka michache hapo nyuma Russia ilikuwa Syria inapigana na ISIS na waasi wengine. Ukitaka kusema Marekani ni dhaifu kwa kulinganisha na kuondoka kwake Afghanistan na Russia ni strong kupambana Syria utakuwa unakosea maana malengo ya kisiasa ni tofauti kabisa kabisa.

Kwa hiyo mmekaa mkaipa deadline KDF ikizidisha zaidi ya dakika moja bila kuanzisha msako mseme ni jeshi dhaifu
 
Nawaombea radhi vijana Kwa niaba maana wanakuona kama kijana mwenzao. Wakati JF tunakutumainia na tunategemea sana mchango wako katika masuala ya kimedani.
 
Mzee baba hata kama madhaifu yapo ila hiyo brigedi ina zaidi ya hayo unayoyasema.
 
Alitupiga mkwara gani mzee? Na mim nifaham
Kuna watu wanatufatafata,muda muafaka ukifika tutawanyoosha......kilichofuata tukapeleka jeshi kongo,tukamnyoosha,Kisha tukarudi home kupitia mpaka wake japo mwanzo alizuwia, sisi ndo sisi kmaaamake!!
 
Kama hilo Jeshi kuna Uganda hakuna watakachofanikiwa.

Ndani ya jeshi la Uganda hao tutsi wamejaa na information zote lazima zifike kwa baba yao.
General muhoozi nasikia alikuwa anagoma kupeleka askari kule , anasema ni NDUGU zao
 
Kenya wanajeshi Zuli tuu uwezo wa kuwapiga m23 wanao , ila ni uwamuzi wao kuamua kuondoka au kupigana.
 
Ila TPDF ni dhaifu kweli
1) TPDF imempa kipigo Idi Amin na jeshi lake, hadi kusababisha raisi huyo wa Uganda kuwa mkimbizi katika nchi nyingine.

2) TPDF imempa mafunzo ya kijeshi raisi Yoweri Kaguta Museven. Mafunzo hayo yamemsaidia Museven kumng'oa raisi wa wakati huo hayati Obote.

3) TPDF imewapa mafunzo waasi wa Zimbabwe wa wakati huo wakiongozwa na mh Robert Mugabe, kama haitoshi pia TPDF ikawaongoza waasi hao wa Zimbabwe katika vita vilivyoung'oa utawala wa wazungu na hatimae mh Mugabe kuapishwa kuwa raisi wa Zimbabwe chini ya usimamizi wa jeshi hilo la TPDF.

4) TPDF imetoa tena mafunzo kwa waasi wa Msumbiji wakiongozwa na Samora Michel, pia kama haitoshi TPDF wakawaongoza waasi hao wa Msumbiji kumchapa mzungu (mreno) hadi mreno akaomba poo na Samora Michel akatangazwa kuwa raisi wa msumbiji.

5) TPDF imepeleka jeshi lake Namibia kupambana na wajerumani hadi wajeruman wakaomba poo na dunia ikashuhudia wajeruman wakitoa uhuru kwa wazawa weusi huku TPDF ikisimamia mchakato mzima wa kupeana madaraka.

6) TPDF ilituma jeshi Angola kumsaidia raisi wa nchi hiyo hayati Dos Santos asipinduliwe na waasi walioongozwa na hayati Savimbi.

7) TPDF imemrudisha raisi wa Burundi hayati Piere Ngurunziza madarakani, baada ya raisi wa nchi hiyo kupinduliwa na jeshi lake mwenyewe. Japo TPDF haikushiriki moja kwa moja, lakini ilitoa onyo kwa wanamapinduzi hao kurudisha utawala huo kwa Ngurunziza kabla kiama chao hakijawaangukia, na kweli waasi walitii baada ya kuijua historia nzima ya TPDF.

8) TPDF ilienda kufanya oparation ya siku 2 tu ambayo ilimrudisha madarakani raisi wa Comoros aliekuwa na yeye amepinduliwa na jeshi lake.

9) TPDF iliwachapa waasi wa M23 pamoja na waasi wengine waliokaidi kuweka silaha chini hadi kupelekea waasi hao kukimbilia Rwanda na Uganda kuomba hifadhi.

List ya oparation bora kabisa zisizoshindwa zilizofanywa na jeshi la TPDF ni kubwa nikisema niendelee siwezi kumaliza.

Sasa na wewe nipe list ya oparation za KDF ambazo zilifanikiwa na dunia ikaelewa. Achana na hiyo ya alshabab ambayo walisaidia kwa kiasi kikubwa na majeshi ya Marekani yaliopo huko Somalia.

Imagine jeshi ambalo linadharauliwa hata na mtoto wa Museven!!!
 
Nimejaribu kuwafuatilia M23 sana nimegundua sio wale wa 2013 sasa hivi wana silaha Nzito na wako well organized nimeona wakishambulia possitions za Jeshi la DRC kwa Grad Missille launchers.
Mkuu, m23 ya 2013 ilikuwa ya moto sana tena walikuwa ni wengi, coz na walizamilia kwenda mpaka Kinshasa.
Wa sasa hivi hawajafika hata 5000 , wanapigana tuu pale pale kivu.
Hata hao munisco wakiamua kuwafukuza wanaweza vizuri,
Shida ya munisco na wao WANAyao huko congo.
Hakuna mtu atoke huko ajekukusaidia kivita, no.
 
Kupigwa inawezekana , ishu ni kuviziana anatuu,
Mbona Mars nyingi wanapigana na kuacha siraha na kukamatwa na jeshi la kongo.
Miezi mittal nyuma walipigana mapaka luteni kanali mmoja wa rwanda waliuwawa na jeshi la congo na baadhi wa wanajeshi wa rwanda, walikimbia mpaka mpaka mpakani mwa uganda kichapo KULIKUWA vikubwa.
 
Tanzania walikuwepo mpk jeshini walikimbizwa.
 
Usisumbuke sanaa mkuu, hao KDF wali pigwa ambush na wavaa kubazi aisee askari wengi wa kdf wwalipotea kule kismayo
Hilo mbona analijua sana, sema ndo hivyo inajitahidi kukwepa ukweli.
 
Sasa hoja zenu za kusema Kenya walipigwa ambush ziko excluded kwenye hii fact. Kwanini KDF iwe dhaifu kisa ilipigwa ambush ila JW ikipigwa ambush utetezi uwe "hata Navy SEALs wanapigwa ambush"
Ni kheri umetambua ya kuwa ambush ni kawaida ila sasa ukipigwa ambush alafu mkashindwa kujitetea ndio shida


Pe Kismayo ile ambush ilikuwa ni ushindi kwa wavaa kubazi coz ilikuwa ktk base yenu na haikuwa njiani ........ Tena base ya kdf ilikuwa full
 
Kenya wanajeshi Zuli tuu uwezo wa kuwapiga m23 wanao , ila ni uwamuzi wao kuamua kuondoka au kupigana.
Huwa siwaelewi watu humu kulinganisha uwezo wa nchi dhidi ya nchi kwa kulinganisha performance ya nchi dhidi ya waasi.

Uturuki hii hapa ina makundi ya kigaidi kama YPG na PKK ila huwezi taja jeshi lolote la Afrika linaloweza ipiga Uturuki na Uturuki imeshindwa kuyamaliza hayo makundi.
Israel ina makundi hasimu kama Hezbollah na Hamas haijawahi wamaliza ila huwezi sema inazidiwa na labda Greece au Jordan kisa hazipambani na makundi ya wahuni.
Russia hii imewapiga ISIS na waasi wengine ila miezi zaidi ya tisa haijamalizana na Ukraine ambayo waasi wa Donetsk na Luhansk waliishinda.
Uwezo wa jeshi dhidi ya jeshi haupimwi tu kwa performance dhidi ya kundi la waasi. Kuna sababu nyingine tofauti.

Ukitazama defense procurement ya majeshi ya West Africa kama Chad na Mali miaka ya siku hizi unaona kabisa ni anti terror weapons ndio wananunua. Nigeria hao kwenye budget ya 2023 Buhari ashasaini Army ipewe fixed wing aircrafts pamoja na kwamba Air Force yao ilipinga vikali sana
Hii ni bada ya kuona Air Force ina ndege nzito kama JF-17 ambazo ni unnecessary na zina high cost of maintenance na pia coordination inachelewa.

Wale washagundua huwezi pigana na gaidi kwa vifaru na masilaha mazito sana. M23 hawana air base au meli au kambi yenye majengo eti ndio ukapige hivyo unahitaji silaha nyepesi zinazobebeka kupigana nao. Silaha zinazotumika na mbinu kwao ni tofauti sana na zitakazotumika ukiambiwa kutoka Ngome andaa shambulizi kwenye bandari ya Mombasa kuharibu meli inayoshusha silaha.

Marekani imelazimika kutengeneza ndege nyingine ya ground attack inayotumia teknolojia waliyotumia mwisho vita ya pili ya dunia. Wanatengeneza Sky Warden, wameona ni gharama kubwa kutumia A-10 Warthog sijui F-16 kwenda kupiga kibanda cha mbao cha gaidi jangwani.

M23 au waasi hapo DRC hakuna mwenye MANPADS, hakuna anti tank rifles wala missiles, hakuna heavy machine guns sanasana utakuta waliambulia kuiba PKP Pecheneng chache ndio wanajidai nazo. Utawaona na RPG chache, yani wako local sasa ukiwatumia kama mlinganyo wa uwezo wa jeshi dhidi ya jeshi utajidanganya.

Counter terrorism na counter insurgency ni tofauti mno na high intensity warfare ambapo unakutanisha peer to peer enemies. Kama mtu hataki na hapa basi aendelee na uzalendo feki ila uzalendo na kujitoa mhanga kwa Wajapani WW2 hakukufua dafu mbele ya uhalisia wa Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…