Jeshi la Kenya lililopelekwa nchini Congo linatia aibu

Tusiwalaumu lakini hua nafikiri pengine hayo majeshi ya kulinda amani hua Wana maelekezo maalum, kwa sababu haiwezekani m23 waendelee kusonga mbele na wakati jeshi la kulinda amani Lina silaha bora kuliko wao

Kuna shida moja ya kupambana na waasi ambayo watu wengi hawajui kuendesha vita kuna sheria zake za kimataifa unavyo pigana inakulazimu kufuata sheria hizi sheria majeshi yote rasmi ya nchi hutakiwa kuzifuata lakini waasi na makundi ya kigaidi hayafuati sheria sasa kupigana na mtu asie fuata sheria papo hapo kuna raia wa kawaida ndani yake ni ngumu kumdhibiti kwa mfano huruhusiwi kupiga raia lakini waasi kuna wakati wakitingwa wanavua nguo za kijeshi wanajichanganya na raia hutakiwi kutumia nguvu kupita kias kuna haki za binadamu ni ngumu mno
 

Nchi ili iwe imara na Rais awe imara na nguvu kwenye uendeshaji na uongozi wa nchi ni lazima kuwe na vitengo vya ujasusi vilivyo imara na vinautii nidhamu uaminifu mkubwa na siri kwa Rais sasa Congo wanashida kwenye vitengo vya usalama huwezi panga jambo na wasaliti ukafanikiwa maana Rais hawez fanya kila
 
Hapo kwenye point yako... makundi yanayomilikiwa na magenerali wa kondo.... hapo ndipo kwenye tatizo. Unakumbuka tulipowafanyizia m23 mpaka Kagame akammaindi Kikwete? Kilichofuata tulipoteza baadhi ya vijana wetu, na kinachofanyika ni kwamba kuna watu waliopamoja nao wanauza mchongo ili wapigwe. Kwa hiyo vibaraka wa hao makamanda ndo tatizo ukifanya kweli lazima wakuuze kwa waasi. Ila ukiwa kama KDF hamna shida
 

Asee! Sikujua kama vita ya kagame na kikwete chanzo ni hiki!
 
M23 wakiwashiwa moto kichanga na kdf na kupigwa utasikia wanajidai wameamua kukabidhi mji huo na kutaka kuandaa makabidhiano.
M23 wanacheza na akili za watu na wanajifanya wajanja sana. Ukweli wao ni jeshi la rwanda ya kagame anayejidai na watutsi wenzake wao hawashindwi kitu.
Dawa yao hawa ni kuwapiga. Shida hakuna wa kuwapiga maana jeshi la congo fardc ni mdebwede. Nina hakika kdf wakiamua kuwapiga hao watutsi wa m23 watakimbilia rwanda.
 
Exactly...

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Enzi za nyerere mlipigwa migufuli midomoni congo hapo vipi.
 
Niliamini kenya wana jeshi hadi nilivowashuhudia wanaiba juice westgate
 
hawa wazungu Jaribu kuharibu amani ktk nchi zao, dakika kadhaa tu tayari wamerekebisha amani jeshi zito linashushwa kwenye eneo la tukio. ila wakija Africa yan wanafanya utani tu, ivi unapiganaga na mtu wa misituni miaka nenda rudi, mtu silaha zenyewe duni, nyinyi wazungu mnakila aina ya silaha lakin mnashindwa kuwadhibiti
 
Halafu wakirudi home wanapewa medali daaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…