Jeshi la Magereza lakanusha taarifa za Tundu Lissu kugoma kula

Jeshi la Magereza lakanusha taarifa za Tundu Lissu kugoma kula

Jeshi la Magereza nchini Tanzania limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amegoma kula chakula akiwa gerezani na kwamba mawakili wake watatu wamezuiwa kumuona.

Akitoa taarifa kwa umma, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi, amesema taarifa hizo si za kweli na zinalenga kupotosha umma.

Mbezi amesema Lissu yupo salama na hajaanza mgomo wa kula chakula kama inavyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, amesema mawakili wa Lissu wanaendelea kumuona kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Jeshi la Magereza limewataka wananchi kupuuza taarifa hizo na kujiepusha na kusambaza habari zisizothibitishwa, likionya kuwa usambazaji wa taarifa za aina hiyo unaweza kuwa kosa la kisheria.
Kauli hiyo ya Jeshi la Magereza imekuja siku nne baada ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dk. Rugemeleza Nshala, kueleza kuwa Lissu...
Chanzo : Magereza



Pia soma: Lissu atangaza mgomo wa kula chakula kuanzia Jumatatu, 26/10/2026
Siasa imesha athiri mpaka taasisi nyeti
 
Maisha ya kutumwa tumwa shida sana.
Ukiwa umetoka familia masikini, elimu ya kuungaunga pamoja na kutokuwa na akili, werevu, busara na hekima, kunapelekea kuamini kuwa bila ya mtu/watu/kikundi fulani, huwezi kuishi vyemaa.

Ndio hapa tunapata machawa na walamba makalio ya wenye nafasi, na tunapa watumwa aka machawa.
 
Jeshi la Magereza nchini Tanzania limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amegoma kula chakula akiwa gerezani na kwamba mawakili wake watatu wamezuiwa kumuona.

Akitoa taarifa kwa umma, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi, amesema taarifa hizo si za kweli na zinalenga kupotosha umma.

Mbezi amesema Lissu yupo salama na hajaanza mgomo wa kula chakula kama inavyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, amesema mawakili wa Lissu wanaendelea kumuona kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Jeshi la Magereza limewataka wananchi kupuuza taarifa hizo na kujiepusha na kusambaza habari zisizothibitishwa, likionya kuwa usambazaji wa taarifa za aina hiyo unaweza kuwa kosa la kisheria.
Kauli hiyo ya Jeshi la Magereza imekuja siku nne baada ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dk. Rugemeleza Nshala, kueleza kuwa Lissu...
Chanzo : Magereza



Pia soma: Lissu atangaza mgomo wa kula chakula kuanzia Jumatatu, 26/10/2026
Stupid,

Hivi wanatuonaje ?
 
Kamwe siwezi amini mamlaka n serikali ya chura aka kizimkazi. Kama JIWE tuliambiwa kua yupo hai na fiti pia anachapa kazi. Kumbe kafa kitambo tu.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Stupid,

Hivi wanatuonaje ?
Dkt. Willibrod Slaa amewahi kutoa madai kwamba chama cha CHADEMA kina matukio ya ndani ya utekaji na kujiteka wenyewe ili kuchafua serikali au kupata huruma ya kisiasa, madai ambayo aliyasisitiza katika kitabu chake kiitwacho Nyuma ya Pazia na kwenye mijadala mbalimbali ya kisiasa.
 
kwahiyo tuseme huyu wakili nshala yuko juu ya sheria?,kama kaeneza taarifa ya uongo akiwa na nia ovu ya kuzua taharuki,kwanini hachukuliwi hatua,,au anaogopwa
Yaani mimi niseme wewe umegoma kula nichukuliwe hatua Nchi ya wadumavu hii..
 
Kwamba leo na jana amefakamia minyama na wali, ila nyumbu wanaamini yuko kwenye swaumu
 
kwahiyo tuseme huyu wakili nshala yuko juu ya sheria?,kama kaeneza taarifa ya uongo akiwa na nia ovu ya kuzua taharuki,kwanini hachukuliwi hatua,,au anaogopwa
Kuamua kula au kutokula ni maamuzi yako binafsi, wewe ukiamua na mimi nikisema umeamua kutokula, kifungu gani cha sheria nishtakiwe ?
Nikisema umeamua kutokula ni kuzua taharuki ?
Mbona hata huko Ulaya na US kuna wafungwa wanaamua kutokula na hawakatazwi, ila mpaka ikifika wametepeta, halafu serikali inachukua hatua ya kuwalisha kwa mirija ili wasikwepe vifungo kwa kujiwahisha kufa
 
Mbona sasa hivi hamlaani? Au kwa kuwa wakati ule, hakuwa kutoka kundi lenu?
Tumelaani sana tu na pia runapinga unnecessary commotions ambazo zinaumiza watoto wa masikini mnaowatumia kama chambo
 
Ananitishia nisiseme kuwa lissu hali kha hii nchi ni ya democrasia sio dictatorship na lissu angekaa benin angepata haya yote .

Usijiaminishe kuwa adui ni atakuwa rafiki siku zote simba si rafiki yake zebra huu ni uongo simba hukaa na simbaa tu.
Jingine aisee lissu alikuwa anamdharau sana kwa huyu mama rejeeni midahalo yake alifikia mahali hata mimi naona aibu .

Hakuwa anamipaka na heshima kwa kiongozi wa nchi hata msemeje nilijua itafika huku nilikuwa nahesabu siku .

Ukipewa second chance usiteleze kuwa na mipakaa . Ulishindwa kuongea matatizo ya nchi mpaka unaanza kusema mama abduli yule hana kitu sijui hili lile kila mahali huogopi na huyu mama ni rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania sio wa kijijini kwenu hata mwenyekiti au diwani tunawaheshimu .

Dada na kaka zetu tunawaheshimu tundu lissu alijisahau .
kwa lissu alivuka mpaka japo sipendi hali yake tunaomba tu amtoe na kumpa onyo na arudi benin huko akapaze sauti ndani kwake lissu anamdharau sana . Sana
 
Back
Top Bottom