SI KWELI PreGE2025 Jeshi la Magereza lasema Lissu hajapotea, bado linamshikilia kwenye gereza la Keko

SI KWELI PreGE2025 Jeshi la Magereza lasema Lissu hajapotea, bado linamshikilia kwenye gereza la Keko

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Jeshi la Magereza lasema limemhamisha Lissu kutoka Keko kwenda Ukonga
Screenshot 2025-04-22 120417.png
 
Tunachokijua
Mnamo tarehe 18, Aprili 2025 ilitolewa taarifa kwa umma na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Wakili Ali Ibrahim Juma, Mawakili, Familia, na wanachama kwa nyakati tofauti, walifika katika Gereza la Keko ambapo Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu anashikiliwa lakini hawakuwanikiwa kumuona baada ya kuambiwa hayupo katika gereza hilo na kutokutokupewa kwa taarifa rasmi ya wapi alipo.

Madai
Kumeibuka taarifa inayosambazwa mtandaoni inayodaiwa kutolewa na Jeshi la Magereza inayokanusha kuwa Tundu Antiphas Lissu, amepotea akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Magereza na kwamba anaendelea kushikiliwa katika Gereza la Keko, Dar es Salaam.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia vyanzo vyake vya kuaminika umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haijatolewa na jeshi la Magereza Tanzania.

Aidha barua hiyo inayoonesha kusainiwa na Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi si ya kweli ni ya kutengenezwa kwani haijachapishwa katika kurasa rasmi za jeshi la magereza bali imekanushwa kuwa si taarifa ya kweli na kuomba wananchi waipuuze.

"Jeshi la magereza linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa kuna taarifa inayo sambaa kwenye mitandao ya kijamii, taarifa hiyo sio sahihi tunaomba wananchi waipuuze"​
20250419_100134.jpg

Jeshi la Magereza nchini limekanusha taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya Kijamii Jana Aprili 18, 2025 ikieleza kuwa Mwenyekiti wa @ChademaTz Mhe. Tundu Lissu yupo salama na bado anashikiliwa kwenye Gereza la Keko Jijini Dar Es salaam.


Jambo TV leo Aprili 19, 2025 tumeitafuta idara ya habari ya Jeshi la magereza ambapo moja ya maofisa habari kutoka Jeshi hilo amesisitiza kuwa taarifa rasmi ya Msemaji wa Jeshi la magereza Elizabeth George Mbezi ni ile aliyoitoa Jana alipokuwa akizungumza na Chombo kimoja cha habari akisema kuwa anafuatilia SAKATA hilo la kutoonekana kwa Tundu Lissu kama ilivyoelezwa na baadhi ya Maofisa na wanachama wa Chadema, akiwasihi Wananchi kuwa na utulivu wakati wakisubiri taarifa kamili ya Jeshi hilo.


Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema kilitoa taarifa yake Ijumaa Aprili 18, 2025 inayodai kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu ametolewa mahabusu na kupelekwa mahali kusikojulikana.


Lissu amekuwa akishikiliwa mahabusu katika gereza la Keko lililopo jijini Dar Es Salaam toka alipofunguliwa mashtaka ya uhaini juma lililopita. Katika taarifa yake Chadema imelitaka jeshi la Magereza, mamlaka husika na vyombo vya dola kutoa taarifa wazi na haraka kwa umma kuhusu mahali alipopelekwa Tundu Lissu.

My take: kama wañakanusha, watueleze alipo?!
 
Mnampotezea mtu muda wake kwa sababu za kijinga tu. Hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom